Invisible
JF Admin
- Feb 26, 2006
- 16,285
- 8,364
Kujulikana ni jambo la kawaida katika jamii, lakini jambo la msingi ni kuangalia unajulikana kwa mambo gani.
Kama ni kujulikana tuu, hata Adolf Hilter, Iddi Amini Dada na Bokasa wanajulikana, lakini wanajulikan akwa mambo gani, ndilo jambo la msingi.
Katika nchi zetu za Kiafrika, imezoeleka kuona viongozi wa juu wanapochanguliwa tuu wanakimbilia nchi za Ulaya na Marekani wakidai wanaenda kujitambulisha.
Hilo ni jambo jema, lakini je, kuna umuhimu sana wa kwenda kujitambulisha? Kuna vitu ambavyo vinaweza vikamfanya kiongozi ajulikane, hata kama hajajitambulisha. Na kwa kawaida, mtu hujulikana kwa yale mambo makubwa aliyofanya, si kwa kujitambulisha tu.
Ni wazi kuwa viongozi kama Nelson Mandela na Mwalimu Nyerere wanajulikana duniani kote, kwa kupigania na kutetea haki za Waafrikam kutafuta uhuru na kupinga unyonyaji katika bara la Afrika.
Jambo la kujiuliza ni kwa mbona viongozi wa Ulaya na Marekani wanapochanguliwa hawaji Afrika ili waje wajitambulishe kama viongozi wetu wanavyofanya, lakini bado wanajulikana?
Isitoshe, kama rais atatembelea kila nchi kwa muda wa siku tatu kwa lengo la kujitambulisha, itachukuwa miaka miwili kuzimaliza. Ingependeza kama viongozi wetu wangetulia nyumbani wakawatumikia wananchi wao kuliko kutembea huku na kule wakidai wanajitambulisha.
Kujitambulisha ni vyema lakini uchapa kazi wako, sera nzuri, kusimamia masilahi ya nchi na maendeleo kwa wananchi kunaweza kumfanya kiongozi ajulikane na akumbukwe hata kama hayuko madarakani.