Marais wenye elimu ndogo barani Afrika

Marais wenye elimu ndogo barani Afrika

Huku kwetu waliamua Rais lazima awe na degree
Sasa wanakoelekea watasema lazima awe na Phd

Kiuhalisia wasomi ndio wanaozidi kuitupia nchi hii kwenye korongo la ufukara, udini, ukanda na ukabila.
Viongozi wengi wasomi wa TZ hutumia elimum zao kufisadi na sio kusaidia jamii $CHENGE$
 
Heshima kwenu wadau,

Moja kwa moja tuungane kwenye mada tajwa hapo juu

Wakati nakua, niliamini kwamba ili mtu awe rais anapaswa kuwa na Elimu kubwa kuliko wale wote anaowaongoza kama sivyo, basi walau awe ana Elimu ya juu yoyote ya chuo kikuu. SASA NIMEKUWA, NA KUKUTA MAMBO TOFAUTI NA UELEWA WANGU WA AWALI.

Afrika ni moja ya mabara yanayoongelewa vibaya kwenye nyanja mbali mbali ikiwepo uchumi mbovu, demokrasia duni, tamaduni zilizopitwa na wakati n.k Leo embu tuangalie Marais wenye Elimu ya chini barani Afrika

1. Jacob Zuma
Huyu ni moja ya kati ya Marais wanaongoza nchi yenye uchumi mkubwa Africa, katika nchi ya Afrika ya Kusini. Zuma hajawahi kusoma hata chekechea, kwa maana nyingine Zuma hakusoma kabisa katika Maisha yake. Hii ni moja kati ya hoja kubwa inayotumiwa na wapinzani wake kumsulubu kisiasa.

2. Salva Kiir
Rais wa Taifa changa kuliko Mataifa yote duniani, Sudan ya Kusini. Aliacha shule mapema kutokana na hali ya vita huko Sudan. Alikuwa rais kwa tiketi ya vuguvugu la SPLM, awali likiongozwa na John Garang na sasa yeye akiwa rais wa Taifa kamili la Sudan ya Kusini.

3. Omary al-bashir
Rais wa Sudan, rais mwingine mwenye Elimu ya chini kabisa ambaye Elimu yake kubwa anayojivunia ni ya jeshi aliyoipata katika Chuo cha Jeshi Misri na baadae Sudan. Amekuwa akipata wakati mgumu sana kuonesha vyeti vyake kuthibitisha Elimu yake.

4. Paul Kagame
Rais wa Rwanda aliyeacha shule akiwa sekondari kwasababu ya kujikuta akipigana Shuleni sana na wanafunzi wengine ambao walikuwa hawaiongelei vizuri Rwanda huko Uganda. Wengine wanataja kufiwa na Baba yake kama sababu ya kutofika mbali kielimu. Mafunzo ambayo aliyopata baadae ni ya kijeshi na si Elimu ya kawaida tunayoisoma Wananchi wa kawaida.

5. Ismail Omar Guelleh
Huyu ni rais wa Djibouti Taifa dogo lenye unasaba na Ethiopia na Somalia. Rais huyu amesoma mpaka 'high school' na baada ya hapo akajiunga na mafunzo na kisha kujiunga rasmi na wavaa suti na miwani nyeusi wa Somalia na baadae kupata mafunzo ya wavaa suti na miwani nyeusi kutoka Ufaransa.

Note: Ukiondoa Afrika Kusini wenye mfumo thabiti wa kikatiba, nchi zote zilizobaki zenye Marais wenye Elimu ndogo zimekuwa zikitumia nguvu nyingi kuliko akili kwenye utawala.
Kwan kusoma ndo nini???!!
 
Hivi elimu ni nini? Hata ukihitimu
std 7 si una elimu tayari au mimi ndiyo sielewi
 
Sergio 5
Hivi unaweza ukawa kachero halafu shule huna?
Ukachero wa zuma ulikuwa tofauti kidogo, yeye kazi yake ilikuwa kuleta fujo mitaani na watoto wenzie then anapelekwa lupango! Siku akiwa anafanya fujo mitaani unakuta wazee wa ANC wamemuandika mwili mzima...akifika lupango wale wafungwa wanasima harakati zinazoendelea mtaani.

Na siku anatoka anaandikwa tena mwili mzima harakati na mipango ya lupango. Akifika mtaani wanamsoma maandishi. Kwa hiyo alikuwa kama conduit ku pass na ku exchange info ndani na nje ya lupango. Alianza akiwa mtoto so hakupata muda wa kupata formal education.
 
Back
Top Bottom