Marais wenye elimu ndogo barani Afrika

Marais wenye elimu ndogo barani Afrika

BUSARA ZANGU

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2013
Posts
778
Reaction score
1,269
Heshima kwenu wadau,

Moja kwa moja tuungane kwenye mada tajwa hapo juu

Wakati nakua, niliamini kwamba ili mtu awe rais anapaswa kuwa na Elimu kubwa kuliko wale wote anaowaongoza kama sivyo, basi walau awe ana Elimu ya juu yoyote ya chuo kikuu. SASA NIMEKUWA, NA KUKUTA MAMBO TOFAUTI NA UELEWA WANGU WA AWALI.

Afrika ni moja ya mabara yanayoongelewa vibaya kwenye nyanja mbali mbali ikiwepo uchumi mbovu, demokrasia duni, tamaduni zilizopitwa na wakati n.k Leo embu tuangalie Marais wenye Elimu ya chini barani Afrika

1. Jacob Zuma
Huyu ni moja ya kati ya Marais wanaongoza nchi yenye uchumi mkubwa Africa, katika nchi ya Afrika ya Kusini. Zuma hajawahi kusoma hata chekechea, kwa maana nyingine Zuma hakusoma kabisa katika Maisha yake. Hii ni moja kati ya hoja kubwa inayotumiwa na wapinzani wake kumsulubu kisiasa.

2. Salva Kiir
Rais wa Taifa changa kuliko Mataifa yote duniani, Sudan ya Kusini. Aliacha shule mapema kutokana na hali ya vita huko Sudan. Alikuwa rais kwa tiketi ya vuguvugu la SPLM, awali likiongozwa na John Garang na sasa yeye akiwa rais wa Taifa kamili la Sudan ya Kusini.

3. Omary al-bashir
Rais wa Sudan, rais mwingine mwenye Elimu ya chini kabisa ambaye Elimu yake kubwa anayojivunia ni ya jeshi aliyoipata katika Chuo cha Jeshi Misri na baadae Sudan. Amekuwa akipata wakati mgumu sana kuonesha vyeti vyake kuthibitisha Elimu yake.

4. Paul Kagame
Rais wa Rwanda aliyeacha shule akiwa sekondari kwasababu ya kujikuta akipigana Shuleni sana na wanafunzi wengine ambao walikuwa hawaiongelei vizuri Rwanda huko Uganda. Wengine wanataja kufiwa na Baba yake kama sababu ya kutofika mbali kielimu. Mafunzo ambayo aliyopata baadae ni ya kijeshi na si Elimu ya kawaida tunayoisoma Wananchi wa kawaida.

5. Ismail Omar Guelleh
Huyu ni rais wa Djibouti Taifa dogo lenye unasaba na Ethiopia na Somalia. Rais huyu amesoma mpaka 'high school' na baada ya hapo akajiunga na mafunzo na kisha kujiunga rasmi na wavaa suti na miwani nyeusi wa Somalia na baadae kupata mafunzo ya wavaa suti na miwani nyeusi kutoka Ufaransa.

Note: Ukiondoa Afrika Kusini wenye mfumo thabiti wa kikatiba, nchi zote zilizobaki zenye Marais wenye Elimu ndogo zimekuwa zikitumia nguvu nyingi kuliko akili kwenye utawala.
 
Hili swala la elimu, ki msingi ni very tricky. Unaweza ukakuta mtu ana elimu ndogo lkn kwenye uongozi akafanya vizuri km, waziri mkuu wa zamani wa Uingereza Bw. Winston Churchill.

Akina Laurent Gbagbo (Prof) au Dr. Mwai Kibaki, hakuna chochote cha maana sana walichofanyia mataifa yao, japo kufeli kwa ujumla kwa viongozi wa Kiafrika kunaweza kuwa ni kwa sababu za ki historia na ki mfumo zaidi kuliko swala la elimu.
 
Zuma si alikuwa kachero wa chama cha ANC kipindi wanapingana na makaburu?
 
ni wengi sana, lakini wana akili kuliko wale walioenda shule. aibu tupu.
 
Heshima kwenu wadau,

Moja kwa moja tuungane kwenye mada tajwa hapo juu

Wakati nakua, niliamini kwamba ili mtu awe rais anapaswa kuwa na Elimu kubwa kuliko wale wote anaowaongoza kama sivyo, basi walau awe ana Elimu ya juu yoyote ya chuo kikuu. SASA NIMEKUWA, NA KUKUTA MAMBO TOFAUTI NA UELEWA WANGU WA AWALI.

Afrika ni moja ya mabara yanayoongelewa vibaya kwenye nyanja mbali mbali ikiwepo uchumi mbovu, demokrasia duni, tamaduni zilizopitwa na wakati n.k Leo embu tuangalie Marais wenye Elimu ya chini barani Afrika

1. Jacob Zuma
Huyu ni moja ya kati ya Marais wanaongoza nchi yenye uchumi mkubwa Africa, katika nchi ya Afrika ya Kusini. Zuma hajawahi kusoma hata chekechea, kwa maana nyingine Zuma hakusoma kabisa katika Maisha yake. Hii ni moja kati ya hoja kubwa inayotumiwa na wapinzani wake kumsulubu kisiasa.

2. Salva Kiir
Rais wa Taifa changa kuliko Mataifa yote duniani, Sudan ya Kusini. Aliacha shule mapema kutokana na hali ya vita huko Sudan. Alikuwa rais kwa tiketi ya vuguvugu la SPLM, awali likiongozwa na John Garang na sasa yeye akiwa rais wa Taifa kamili la Sudan ya Kusini.

3. Omary al-bashir
Rais wa Sudan, rais mwingine mwenye Elimu ya chini kabisa ambaye Elimu yake kubwa anayojivunia ni ya jeshi aliyoipata katika Chuo cha Jeshi Misri na baadae Sudan. Amekuwa akipata wakati mgumu sana kuonesha vyeti vyake kuthibitisha Elimu yake.

4. Paul Kagame
Rais wa Rwanda aliyeacha shule akiwa sekondari kwasababu ya kujikuta akipigana Shuleni sana na wanafunzi wengine ambao walikuwa hawaiongelei vizuri Rwanda huko Uganda. Wengine wanataja kufiwa na Baba yake kama sababu ya kutofika mbali kielimu. Mafunzo ambayo aliyopata baadae ni ya kijeshi na si Elimu ya kawaida tunayoisoma Wananchi wa kawaida.

5. Ismail Omar Guelleh
Huyu ni rais wa Djibouti Taifa dogo lenye unasaba na Ethiopia na Somalia. Rais huyu amesoma mpaka 'high school' na baada ya hapo akajiunga na mafunzo na kisha kujiunga rasmi na wavaa suti na miwani nyeusi wa Somalia na baadae kupata mafunzo ya wavaa suti na miwani nyeusi kutoka Ufaransa.

Note: Ukiondoa Afrika Kusini wenye mfumo thabiti wa kikatiba, nchi zote zilizobaki zenye Marais wenye Elimu ndogo zimekuwa zikitumia nguvu nyingi kuliko akili kwenye utawala.
Hawa wenye akili kubwa wametufikisha wapi?
 
Rasmi na isiyo rasmi ! Zote ni elimu
Ni kweli mkuu, kuna Elimu rasmi na isiyo rasmi. Lakini mimi nimeongelea kwa Muktadha wa Elimu rasmi, Elimu inayothibitishwa kwa kutunukiwa cheti.

Ukiongelea Elimu rasmi na isiyo rasmi basi hakuna mtu ambaye hana Elimu dunia hii isipokuwa watoto wachanga.

Kwahiyo kwa Muktadha wa Elimu (ile maana ambayo ikitajwa wote tunaelewa hivyo) bado hoja ya kutokwenda shule hao wakuu itasimama
 
Vipi kuhusu wakuu wa mikoa wenye elimu ndogo? Nadhani huyu wa kwetu atakuwa anashika nafasi ya kwanza Duniani!!!
 
Kwangu ni bora raismwenye shule ndogo kwa sababu nzuri ambaye ana utendaji mzuri, kuliko rais mwenye shule kubwa kwa sababu mbaya ambaye ana utendaji mbaya.

Mtu kama Lula da Silva wa Brazil hakusoma sana, hana hata degree, lakini ni kwa sababu alianza kufanya kazi akiwa mdogo kusaidia familia yao masikini na akajiingiza katika uongozi wa vyama vya wafanyakazi huko akapata elimu nzuri ya practical kuliko degree ya darasani, akaja kusaidia kuondoa Wa Brazilwengi sana katika umasikini.

Ukiangalia historia ya mtu kama Harry Truman, rais wa Marekani, hakupata nafasi ya kupata degree lakini alipigana vita kuzuia ufashisti na akatumikia sana kwenye ubunge.

Ukiangaliamtu kama Sizonje kasoma mpaka Ph.D lakini hata hiyo Ph.D, kaitafuta kwa sababu alikuwa anabishana na mtu wizarani, Ph.D si ya kutafuta elimu, ya kutakakushinda ubishi kujionesha anajua zaidi. Na kazi yake, kauli zake, zinamuonyesha hana elimu licha ya kupata Ph.D.

Give me a Harry Truman or Lula da Silva over Magufuli any day of the year.
 
Back
Top Bottom