Marais wastaafu wakacha sherehe Dodoma

Marais wastaafu wakacha sherehe Dodoma

Kazitunayo

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2013
Posts
3,784
Reaction score
3,205
Marais hawa wastaafu hawajaonekana katika tukio hili la kiistoria pamoja na waziri mkuu mstaafu Sumaye pia hajaonekana Dodoma..

Hii ni kusema hawajaridhika na mchakato ulivyopelekwa au wapo nje ya nchi?

============

Benjamin-Mkapa.jpg

Benjamin Mkapa

NA JONAS MUSHI, DAR ES SALAAM

RAIS mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa na Rais mstaafu wa Zanzibar, Aman Abeid Karume hawakuonekana katika sherehe za makabidhiano ya Katiba inayopendekezwa zilizofanyika jana mjini Dodoma.

Kutokuwapo kwao katika sherehe hizo, kunakwenda tofauti na tangazo lililotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Rehema Nchimbi aliyesema viongozi wote wastaafu wamealikwa na watakuwapo.

Pamoja na kutokuwapo kwa viongozi hao, haikutolewa taarifa yoyote hadi mwisho wa shughuli hizo.

Mbali na Mkapa na Karume, pia wajumbe wote wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba pamoja na Mwenyekiti wake Jaji Joseph Warioba hawakuwapo katika sherehe hizo.

Kutokana na hali hiyo pia Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, naye kuwepo katika sherehe hizo.

Kutoonekana kwa vigogo hao huenda kukaibua mjadala mzito kwa wananchi kutokana na uzito wa tukio la jana la kukabidhiwa Katiba inayopendekezwa kwa Rais Jakaya Kikwete na Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein.
CHANZO: Mtanzania
 
Acha umbea sumaye alikuwepo, na pia unafikiri hawa wazee hawana majukumu mengine kitaifa na kimataifa??? Shughuli ya leo ilikuwa ndogo sana.
 
Acha umbea sumaye alikuwepo, na pia unafikiri hawa wazee hawana majukumu mengine kitaifa na kimataifa??? Shughuli ya leo ilikuwa ndogo sana.

ndogo kwako na mzazi wako..
ebu yataje majukumu ya kitaifa unayoyajua we binti?
 
Marais hawa wastaafu hawajaonekana katika tukio hili la kiistoria pamoja na waziri mkuu mstaafu Sumaye pia hajaonekana dodoma..
Hi ni kusema hawajaridhika na mchakato ulivyopelekwa au wapo nje ya nchi


Acha ushakunaku na ushambenga kiroboto msaga sumu Sumaye alikuwepo mwanzo mwisho...

Kuhusu mkapa na karume wamewakilishwa vyema wala kutokuwepo kwao hakumaanishi hawajaridhia....

mtalala nje kwa habari za kuokoteza mbulumundu wafitini nyie
 
wale wazungu wanaotupaga misaada ya vyandarua walikuwepo?
 
Waziri Mkuu Mstaafu Sumaye na Lowasa walikuwepo acha uongo wako hapa na walikaa karibu .....
 
Mkapa nimemuna Kabia. ila hakuwepo kwenye high table. angalia Kikwete anaingia utamuona.

Mkapa hakuwepo...umemfananisha...mkapa angekuwepo angekaa na mwinyi.....usibishe kitu kilicho obvious
 
Back
Top Bottom