Marais Museveni na Magufuli wakubaliana kujenga bomba la mafuta

Cicero

JF-Expert Member
Jan 20, 2016
2,924
3,073
Katika mazungumzo hayo pamoja na mambo mengine wamekubaliana kujengwa kwa bomba la kusafirisha mafuta kutoka Bandari ya Tanga nchini Tanzania hadi nchini Uganda.

Rais Museveni amemtembelea Rais Magufuli katika Ikulu ndogo ya Arusha leo jioni mara baada ya kuwasili hapa nchini akitokea nchini Uganda, ambapo hapo kesho atahudhuria Mkutano Mkuu wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, utakaofanyika katika Hoteli ya Ngurudoto Jijini Arusha.

Akizungumza baada ya viongozi hao kufanya mazungumzo ya faragha, Rais Magufuli amesema wamekubaliana kutekeleza mradi huo wa bomba la kusafirisha mafuta kutoka Tanga hadi Uganda, kwa manufaa ya nchi zote mbili na nchi nyingine za Afrika Mashariki.

Amesema bomba hilo litakuwa na urefu wa kilometa 1,120 na kwamba mradi huo utazalisha ajira za watu zaidi ya 15,000.

Rais Magufuli ameongeza kuwa pamoja na kujengwa kwa bomba la mafuta, pia wamezungumzia kuongeza biashara ndani ya nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki, kujenga viwanda na kuzalisha ajira zaidi kupitia sekta mbalimbali za uzalishaji mali.

Aidha, Rais Magufuli amesema katika Mkutano huu nchi wanachama watajadili maombi ya nchi ya Sudan Kusini kupata uanachama ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Amebainisha kuwa, kwa Sudan Kusini kuwa mwanachama Jumuiya ya Afrika Mashariki, itakuwa na uwezo wa kufanya biashara katika eneo lenye takribani watu milioni 150 na hivyo kupata manufaa makubwa zaidi.

Kwa upande wake Rais Yoweri Kaguta Museven pamoja na kuunga mkono yaliyosemwa na Rais Magufuli amempongeza kwa kasi yake nzuri aliyoanza nayo katika uongozi, na amesema ni matumaini yake kuwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, sasa zitakuwa katika nafasi nzuri ya kwenda kwa kasi ya Rais Magufuli katika maendeleo.

Chanzo: EATV
 
Big news, that little debate is over finally......Magufuli moving with 'magufuli speed', hehe Museveni himself!
 
Walikosa jambo la maana la kujadili wakatunga huo upuuzi..reli ya tanga hadi musoma walishamaliza kujenga?
 
Asante kwa kuniita huku Cicero hongera zenu kama itatendeka, fahamu sisi ni manyangau wa kibepari na huwa hatuna majungu kwenye ushindani wa biashara. Sisi sio kama nyie Watanzania ambao huwa mnalialia kwa kila jambo. Biashara haina mambo ya undugu, ni mikakati na maslahi na ikitokea umeshindwa kimikakati basi unakubali na kuachia.

Hili la bomba ikitokea hatimaye imeishia kujengwa kupitia Tanga, basi tutawapa hongera na kufanya mengine yanayotuhusu. Lakini kwa sasa bado tupo uwanjani na mumefunga bao la kwanza na la pili, sisi kama manyang'au tutafanya yetu kimikakati, tutaibuka na mbinu nyingine hadi tumburuze Museveni kwa pua, akigoma hadi mwisho basi tunaanchia bila hard feelings.

Mojawapo wa miikakati yetu itakua ni kuanza ujenzi wa bomba lenyewe maana tayari tuna mafuta, sasa hapo tunatumia huo ujenzi kumtongoza maana ataona kazi inafanyika tayari sio zile ngonjera za Wabongo. Nyie mikakati yenu eti mnafuata mambo ya undugu kwa kumkumbushia Museveni kwamba mlimsaidia kunyakua madaraka. kazi kweli, mnapenda sana kuchanganya biashara na undugu ambapo haziendani, sasa hivi hiyo route yenu ndio inafaa kwa kweli tukipiga mahesabu, na badala kuwa wajanja mtumie huo ukweli, mnaongea mambo ya undugu wenu na Museveni.
 
Walikosa jambo la maana la kujadili wakatunga huo upuuzi..reli ya tanga hadi musoma walishamaliza kujenga?
iko

Tanga -Arusha iko hatua ya detailed engineering design na Arusha - Musoma, Spurs Minjingu (Engaruka) iko kwenye feasibility study .....hii siyo barabara ya Tanroads
 
Reli ya Kati
Bandari ya Bagamoyo
Kiwanda cha gesi mtwara
Bomba la Mafuta toka Uganda

Trilion kadhaa zinahitajika, na sio za kitoto..
 
Asante kwa kuniita huku Cicero hongera zenu kama itatendeka, fahamu sisi ni manyangau wa kibepari na huwa hatuna majungu kwenye ushindani wa biashara. Sisi sio kama nyie Watanzania ambao huwa mnalialia kwa kila jambo. Biashara haina mambo ya undugu, ni mikakati na maslahi na ikitokea umeshindwa kimikakati basi unakubali na kuachia.

Hili la bomba ikitokea hatimaye imeishia kujengwa kupitia Tanga, basi tutawapa hongera na kufanya mengine yanayotuhusu. Lakini kwa sasa bado tupo uwanjani na mumefunga bao la kwanza na la pili, sisi kama manyang'au tutafanya yetu kimikakati, tutaibuka na mbinu nyingine hadi tumburuze Museveni kwa pua, akigoma hadi mwisho basi tunaanchia bila hard feelings.

Mojawapo wa miikakati yetu itakua ni kuanza ujenzi wa bomba lenyewe maana tayari tuna mafuta, sasa hapo tunatumia huo ujenzi kumtongoza maana ataona kazi inafanyika tayari sio zile ngonjera za Wabongo. Nyie mikakati yenu eti mnafuata mambo ya undugu kwa kumkumbushia Museveni kwamba mlimsaidia kunyakua madaraka. kazi kweli, mnapenda sana kuchanganya biashara na undugu ambapo haziendani, sasa hivi hiyo route yenu ndio inafaa kwa kweli tukipiga mahesabu, na badala kuwa wajanja mtumie huo ukweli, mnaongea mambo ya undugu wenu na Museveni.
Haujui kwamba na sisi tunawapandishia gesi huko kwao?? Kwenu keshaona hana la kupata mana mafuta yenyewe anayo mengi kuliko nyie
 
Ningeshangaa sana hili bomba lingepitishiwa kenya, ingawa wakenya wamefanya fujo zooote lipitishiwe kwao
ila kilomita 1200 kwa 1600, tofauti ni kubwa sana!

Tanzania inabidi tutumie fursa za kigografia vzr kuleta maendeleo ya haraka kwa watu wetu
 
Hii taarifa naisoma lakini siielewi. Uganda wamegundua mafuta na plan iliyopo ilikuwa ni kusafirisha mafuta kutoa Ugand kuja tanga ili ku export lakini leo naona imekuwa vice versa au ni macho yangu yananidanganya?
 
Vice versa kivipi? Iko hivyo kama ulivyosema
 
Hii ndio africa museveni has already gotten away with stealing the election
African politics, hamna wa kumkemea mwenzake sababu wote ni chungu kimoja tu, sasa hebu sema, Museveni, Nkurunziza na Pombe wote wako madarakani kwa nguvu za dola sasa hapa nani atamkaripia mwenzake?

We acha tu.
 
Asante kwa kuniita huku Cicero ho haina ujenzi wa bomba lenyewe maana tayari tuseveni kwamba mlimsaidia kunyakua madaraka. kazi kwe......u, na badala kuwa wajanja mtumie huo ukweli, mnaongea mambo ya undugu wenu na Museveni.
kagongwe mbele huko..
 
nchi hii ni shida mipango mingi utekelezaji akuna, Mara bomba la gesi kutoka Tanzania hadi Kenya
 
Back
Top Bottom