Marais kutoka Pwani/Pemba wanatuokoa kila mara demokrasia inapominywa, huipa Nchi unafuu wa demokrasia, uchumi na amani

NetMaster

JF-Expert Member
Sep 12, 2022
1,454
4,853
N:B: >> Pwani inayozungumiwa ni mkoa, sio ukanda wa pwani unaojumuisha mikoa ya ziada ya Tanga, Lindi na mtwara.

Kigezo kikuu kwa marais hawa huwa ni utamaduni wao wa ustaarabu, ni utamaduni ambao kwa mikoa ya Pwani na Pemba ni sehemu ya maisha yao kabisa kwa muda mrefu, elimu, dini na teknolojia ni vitu vilivyokuja kuimarisha ustaarabu ambao ulishakuwa ni sehemu ya maisha yao, kuna maeneo vitu hivyo hivyo vimefika mda mrefu lakini bado suala la ustaarabu pana shida.

Haimaanishi kwamba wao wakiwepo mabaya yanapotea, La hasha!! kuna madudu kama ufisadi huwa yanaendelea lakini kwa kuwa huwa kuna uhuru wa vyombo vya habari kutoa taarifa bila kukiona cha mtema kuni, hapa ndio huwa tunasikia sana mambo kama ya escrow, rada, madeni, mifumuko ya bei, n.k. hata ile jeuri ya kuwa chama tawala na kusema wewe huguswi hata ukionea wengine inapungua, Mfano pale Mbeya kipindi cha kikwete 2015 kuna vijana wa Green Guard ya ccm walimpiga mpita njia kisa kavaa fulana za chadema, Polisi walipiga msako waliwatia adabu wale vijana bila kujali chama utu kabla ya siasa.

Tukija kwenye siasa za demokrasia, Kwa Nyerere kulikuwa na mfumo wa chama kimoja ila ni Mwinyi alituletea mfumo wa vyama vingi. Kwa mkapa aliminya upinzani ila Kikwete aliweza kuleta mafuriko ya wapinzani bungeni na hata mijadala ya katiba mpya iliruhusiwa.

Nae raisi wa sasa Samia Suluhu Hassan anaendelea kuproove kwamba marais wa kanda hizo wana nafuu.

• Ubinadamu: Baada ya shambulio la Lissu, Rais Samia bila kificho aliamua kuweka siasa pembeni akaenda kukutana na Lissu na kumjulia hali dhidi ya unyama aliofanyiwa.

Kuondoa vifungo yombo vya habari : Amefungulia vyombo vya habari ikiwemo magazeti na kuweka mazingira rahisi ya vyombo vya habari, hapo utawala uliopita kufungua hata youtube tv ulianzishwa utaratibu kulipia leseni ya milioni 2.

Uhuru wa maoni - Hata huu mfumuko wa bei watu wanaweza kuzungumzia wazi bila kuhofia defenda zitakuja kuwasomba, Mfano mdogo tu wa kujua thamani ya uhuru huu vuta picha awamu iliyopita hapo hata kusema "vyuma vimekaza" ilikuwa marufuku.

• Kutokomeza siasa za visasi: Wapinzani wengi waliofungwa kwa kesi za kubambikiwa na kukomolewa wameachiwa huru.

•Lugha na vitendo vya staha: Hata kama mtu kakosea kuna namna ya kudili nae, kumdhalilisha kwa kumtukana ni mjinga / mpumbavu ama matumizi ya nguvu ikiwemo viboko si vema.

• Amani: Nchi imerejea katika amani, watu wasiojulikana waliokuwa wanateka watu na kuwaua na kuwatelekeza fukweni kwa sasa ni kama wamepotea.

• Uchumi:

(a) Mzunguko wa pesa ni muhimu zaidi kuliko bei za vitu, leo hii hata sukari iuzwe elfu 1 kama hakuna mzunguko wa pesa watu watarudi kukamulia miwa kwenye chai, pamoja na changamoto ya bei kupanda hatuwezi kusahau kwamba kwa sasa mzunguko wa pesa umeongezeka sana unaosaidia watu wawezeze kumudu gharama za maisha.

(b) baada ya raisi kukemea matumizi ya mabavu na vitisho kwenye biashara, kwa sasa makampuni na wawekezaji wengi waliofunga biashara zao wameanza kurudi, mzunguko wa pesa unazidi kuongezeka. ukisanyaji wa kodi upo chini ya watu waliosomea taaluma, mambo ya task force yameyeyuka.

(c) Kwenye sekta ya ajira tumeanza kuona angalau ajira zimeanza kuwepo, waajiriwa wa serikalini wamepandishiwa mishahara, , waliosoma kwa mkopo wamepunguziwa makato kwenye mishahara,

• Kupungua kwa wakuu wa mikoa / wilaya wasio wastaarabu: Tuliwahi kuwa na viongozi waliokuwa na majigambo ya vyeo walivyonavyo kufikia kuanza kuchapa viboko wananchi, kutukana watu hadharani, dharau, kujiona miungu mtu, n.k. kwa sasa wamepungua.

Mikutano ya hadhara: Kaweza kuondoa vifungo vilivyowekwa dhidi ya vyama vya siasa vya upinzani kufanya mkutano
 
Na nizidi kukazia ni kwa kigezo cha Mikoa ya Pwani na Pemba.

Ni mikoa na sio ukanda mzima wa pwani wala dini.

Pwani na Pemba ndiko ustaarabu ulipozaliwa.
 
Sema WAISLAM ni watu makini na wenye hofu ya Mungu. Umezunguka sana.
Nimeshafanya uchunguzi wangu mkuu, wengine ni dini hizo hizo na ni wazee kabisa lakini ustaarabu umewapita kushoto, Hebu rejea tu hata kwa Mzee Makamba alichokua anaongea kikao kilichopita cha chama, tena sio mara moja.

Nazidi kukazia ni Mkoa wa Pwani na Pemba na sio dini ama kusema ni ukanda mzima wa pwani
 
Nimeshafanya uchunguzi wangu mkuu, wengine ni dini hizo hizo na ni wazee kabisa lakini ustaarabu umewapita kushoto,

Hebu rejea tu Mzee Makamba alichokua anaongea kikao kilichopita cha chama, tena sio mara moja.

Nazidi kukazia ni Mkoa wa Pwani na sio dini ama kusema ni ukanda mzima wa pwani
Makamba ni kiongozi?? Wakati wa uongozi wake alitenda mengi sana mazuri
 
Makamba ni kiongozi?? Wakati wa uongozi wake alitenda mengi sana mazuri
Asili huwa haijifichi mkuu, ni vipi unatamka mbele ya hadhara kauli kama zile kwamba "wazuri huwa hawafi" tena mbele ya wajane?

Kiufupi nimeshafanya research Yangu nimefikia muafaka kwamba Pwani na Pemba ndiko ulipozaliwa ustaarabu na kuufanya uwe sehemu ya maisha yao, yawezekana tunatofautiana kiwango cha ustaarabu lakini Pwani na Pemba ni vinara wa ustaarabu.

Kinachotufaa zaidi ni kuwa na viongozi wenye ustaarabu bila hata kujali elimu zao na dini zao,
 
Tunazidi kujionea na wala hatusimuliwa, Tanzania ustaarabu ulianzia Pwani na kusema kweli ni moja kati ya vitu vya kujivunia kwenye siasa.

Pindi wawapo hata uchumi unaimarika, mzunguko wa pesa unakuwa mkubwa hivyo kupunguza hata makali ya bei kupanda, sote ni mashahidi kile kipindi cha Mwinyi na Kikwete pesa ilikuwepo, na hata sasa vyuma vimeanza kulegea si kama awamu iliyopita.

Tukija kwenye siasa za demokrasia, Kwa Nyerere kuwa na mfumo wa chama kimoja ni Mwinyi alituletea mfumo wa vyama vingi. Kwa mkapa kuminya upinzani, Kikwete aliweza kuwatendea haki wapinzani na kweli kwenye chaguzi zikawajaza bungeni n ahata mijadala ya katiba mpya iliruhusiwa.

Nae raisi wa sasa Samia Suluhu Hassan anaendelea kuproove kwamba marais wa kanda hizo wana nafuu.

• Ubinadamu: Baada ya shambulio la Lissu, Rais Samia bila kificho aliamua kuweka siasa pembeni akaenda kukutana na Lissu na kumjulia hali dhidi ya unyama aliofanyiwa.

Uhuru wa kujieleza: Amefungulia vyombo vya habari ikiwemo magazeti na kuweka mazingira rahisi ya vyombo vya habari, hapo utawala uliopita kufungua hata youtube tv ilianzishwa kodi ya milioni 2.

• Kutokomeza siasa za visasi: Wapinzani wengi waliofungwa kwa kesi za kubambikiwa na kukomolewa wameachiw huru.

•Lugha na vitendo vya staha: Hata kama mtu kakosea kuna namna ya kudili nae, kumdhalilisha kwa kumtukana ni mjinga ama matumizi ya nguvu kama kumchapa hadharani sio ustaarabu

• Amani: Nchi imerejea katika amani, watu wasiojulikana waliokuwa wanateka watu na kuwaua na kuwatelekeza fukweni kwa sasa ni kama wamepotea.

• Uchumi: Kiuchumi nako pesa imeanza kuonekana, Biashara nyingi zimeanza kurejea, hii hutoa fursa pia kwenye ajira.

Mikutano ya hadhara: Kaweza kuondoa vifungo vilivyowekwa dhidi ya vyama vya siasa vya upinzani kufanya mkutano
Nyerere, Mkapa na Magufuli katika uongozi wao walishatumia neno 'mpumbavu' katika hotuba zao.

Ni kielelezo cha majivuno na kushindwa kujishusha pia ni ishara ya kukosa uvimilivu ndani ya nafsi zao.

SSH hutakuja kumsikia akitukana tusi lenye uzito kama lilivyo bila ya kutafuna maneno laini kwa ajili ya kufikisha ujumbe mzito.
 
Nyerere, Mkapa na Magufuli katika uongozi wao walishatumia neno 'mpumbavu' katika hotuba zao.

Ni kielelezo cha majivuno na kushindwa kujishusha pia ni ishara ya kukosa uvimilivu ndani ya nafsi zao.

SSH hutakuja kumsikia akitukana tusi lenye uzito kama lilivyo bila ya kutafuna maneno laini kwa ajili ya kufikisha ujumbe mzito.
Nyerer alishamchapa Spika samwel sita Viboko akiwa chuoni,

Mkapa katika hotuba alishasema watanzania ni wajinga, Magufuli havihesabiki
 
Back
Top Bottom