Marafiki Wawili

Zero IQ

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2016
Posts
13,985
Reaction score
25,200
Marafiki wawili*(Elias na Ben)* walikuwa wanatembea mtaani akatokea mwanamke akarusha busu kwa mmojawapo kupitia dirishani katika jengo la ghorofa tatu.

Wakaanza kujadiliana kama ifuatavyo:

*Ben:* Muone yule mrembo amenirushia busu

*Elias:* tafadhali achana na huyo mwanamke, usimjali..

_(baadae yule mwanamke akamuashiria aende)_

*Ben:* yule mwanamke ameniita!

*Elias:* Rafiki yangu, usiende. Nakutafadhalisha.

*Ben:* Kwa nini unaniambia nisiende Wakati mrembo kama yule ananiita? Huo ni wivu

*Elias:* Ben, Ninakutafadhalisha tena, usiende, tafadhali usiende kule _(akihisi kutotiliwa maanani)_

_(Rafiki yake alimpuuza na alienda kwa yule mwanamke, mwanamke alishuka kukutana naye na wakapanda juu. Ghafla wakiwa wanataka kuanza taratibu za kula uroda, wakasikia mlio WA gari getini)_ .. [emoji344][emoji344]

*Lady:* _(akiangalia kupitia dirishani)_
Oooh! Yule ni mume wangu!!

*Ben:* Mama yangu !
Nipo matatani, kweli ? ..!!

*Lady:* Usiwe na khofu, jifanye kuwa Dobi na anza kupiga pasi hizo nguo

(akimuonyesha lundo la nguo)

_(Ben alitumia masaa matano kukamilisha kunyoosha zile nguo kwa sababu yule mume hakutoka tena siku ile)_

_(Siku iliyofuatia Ben alikwenda kwa Rafiki yake)_

*Ben:* Kaka, unaweza kuamini Jana nimepiga pasi nguo kwa masaa matano???

*Elias:* Lakini nilikwambia usiende. Nguo zote hizo ulizonyoosha, *Nilizifua Mimi Juzi!!*
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

*When an experienced person speaks ... [emoji101]you must listen..!*
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…