Moshi. Mbunge wa Moshi Vijijini na Mjumbe wa Nec ya CCM, Dk Cyrill Chami, amewaomba walimu zaidi ya 2,700 wamuombee Waziri mkuu mstaafu, Edward Lowassa, ili ndoto yake iweze kutimia.
Wakati Dk. Chami akiwaomba walimu hao, mtandao wa marafiki wa Lowassa Kanda ya Kaskazini, juzi walikuja na staili mpya ya kumshawishi Mbunge huyo wa Monduli agombee nafasi ya Urais.
Staili hiyo mpya imekuja wakati CCM ikiwa imempiga stopu kuendelea na utaratibu wake wa kupokea makundi ya watu wanaomshawishi kugombea urais na yeye (Lowassa) kuridhia na kuwaomba wananchi wasubiri maelekezo ya CCM.
Marafiki hao ambao ni wanafunzi wa vyuo vikuu mkoani Kilimanjaro, walikwenda kitengo cha damu salama Kanda ya Kaskazini kuchangia damu kama njia ya kutambua na kuenzi upendo wa Lowassa.
Tukio hilo la wanafunzi hao kwenda katika kitengo hicho, kilitanguliwa na tukio la mkutano mkuu wa Chama cha Akiba na Mikopo (Saccos) ya Walimu Moshi Vijijini kufanya mkutano wao mkuu. Katika mkutano huo, Dk Chami aliyekuwa mgeni rasmi, aliwaambia amekwenda pale akiwa na salamu kutoka kwa Lowassa kwamba anawapenda sana walimu. Anasema anawapenda na anawakumbuka sana na anawaomba mmuombee ili ndoto yake na ile safari yake (bila kuitaja) itimie, alisema Dk Chami na walimu hao kulipuka kwa vigelegele.
Katika tukio la uchangiaji wa damu, wanafunzi zaidi ya 100 wa vyuo vikuu mkoani Kilimanjaro, walitumia tukio hilo kumuunga mkono Lowassa wakimsihi atangaze nia ya kuwania Urais 2015.
Mratibu wa marafiki wa Lowassa, Noel Nnko, alisema wanafunzi hao wameamua kuchangia damu kumuunga mkono kada huyo kwa vile wao hawana uwezo wa kutoa fedha za kuchangia fomu.
Chanzo: Mwananchi
Lowassa anashawishiwa kwa lipi, wakati inajulikana wazi kwamba Urais anautaka kwa udi na uvumba, tangu mwaka 1995? Maigizo mengine bhanaaaaa!!!!!!

Ndoto aote lowasa walimu ndio wamuombe ili hiyo ndoto iweze kutimia!!!
Ujinga mwingine unalemea sana.
Rais alisema watu waweza shawishiwa kugombea urais 2015 so Lowasa anaendelea kushawishiwa na wadau mbali mbali. Lowasa is NON STOP kwa presidency contest this year.
Mi nadhani kwa CCM ndo jembe la ng'ombe kwani kigezo no 1 ni kuwa joka kuu la makengeza. Sasa katika mafisadi mbadhani nani mbabe. Ngoja na Chenge aibuke siku ya kuchukua fomuLowassa ni Fisadi mkuu nchi hii ndiyo maana alijiuzulu, Hivyo ufisadi ni ugonjwa mbaya sana kuliko hata huo alionao wa Kutetemeka. Aachane na mambo ya urais kwani bado ni mchafu sana, Nchi yetu itakuwa rehani tukiendelea ku entertain haya maigizo ya Lowassa
Hata Kikwete 2005 tuliambiwa ni mgonjwa sana, hayo ni magonjwa ya kupakaziwa tu. Wewe unaweza kutueleza ugonjwa wa Lowasa?!Lowassa ni mgonjwa sana, tusitake kuingia gharama ya kuchagua Rais mara 2
Ndoto aote lowasa walimu ndio wamuombe ili hiyo ndoto iweze kutimia!!!
Ujinga mwingine unalemea sana.
Hata Kikwete 2005 tuliambiwa ni mgonjwa sana, hayo ni magonjwa ya kupakaziwa tu. Wewe unaweza kutueleza ugonjwa wa Lowasa?!