Marafiki wa kudumu wanaisaidia nini tanzania kama si kunyonya? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Marafiki wa kudumu wanaisaidia nini tanzania kama si kunyonya?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by sammosses, Oct 27, 2012.

 1. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #1
  Oct 27, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Sifa kubwa ya Marekani ni kutokuwa na maadui na marafiki wa kudumu zaidi ya kuangalia maslahi kwa taifa lao,hali hiyo ndiyo maana utaona Marekani ina pambana leo nchi fulani lakini kesho yake akawa rafiki yake.Urafiki wa nchi ni urafiki wa mashaka kwa kuwa umelenga maslahi yake binafsi bila kujali upande wa pili.

  Tanzania enzi za utawala wa awamu ya kwanza ilikuwa ni nchi inayofuata siasa ya kutofungamana na upande wowote,kiongozi wa awamu hiyo alikuwa ni mkweli kiasi cha kutengana na unafiki.Aliunadi msimamo huu uliopelekea taifa letu kuheshimika tofauti na hivi sasa taifa limegeuka taifa la omba omba.

  Alithubutu kuufia msimamo wake hata katika vikao vikubwa vya baraza la usalama la umoja wa mataifa,lakini taifa letu leo limepoteza sifa na msimamo wake ambao ulidumu kwa zaidi ya miaka 24 bila kutetereka.Nchi ilisimama kama taifa makini na hata zile nchi za NATO ziliheshimu misimamo ya viongozi wetu.

  Hatuna uhakika ni siasa gani ambazo tunazifuata na hatujui tumerithi toka kwa nani.Ardhi inafanyiwa batter system trade kwa kubadilishana na chandarua kwa kauli mbiu ya kampeni ya kutokomeza malaria.Mfumo vagrant wa siasa umesababisha nchi kuwa bendera fuata upepo.

  Leo hii nchi yetu ina jinasibu kuwa kisiwa cha amani na wingi wa weredi wa kuwakaribisha wageni ambao ndiyo walikuwa maadui wa nchi nyingi za kiafrika na Uafrika wetu.Lakini tuna nufaika nini na urafiki huu wa mashaka ikiwa rasilimali zetu zinapotea na kutoweka nchini petu.

  Hali tete ya mabadiliko ya nchi yamesabaishwa na uroho wa madaraka na tamaa ya kujilimbikizia mali kwa kuruhusu misitu yetu kufanya shamba la bibi na kupoteza uoto wa asili ambao ulisababisha hali ya hewa iliyoleta mvua zenye tija kiasi cha kuwa na top five nchini kwetu kwa mikoa ya hiyo ya nyanda za juu kusini kutoa chakula kingi na kujaza maghala yetu.

  Tunauza ardhi wakati nchi haina chakula cha kutosha na hata kilichoko nacho kinawekewa masharti.Mfumo huu vagrant wa kutokujua tushike wapi ndiyo ulipelekea rais wetu kuwa Vasco Da Gama na top begger country in the world.Hali hiyo leo imesababisha Waingereza kututingishia kiberiti kwa kutambua haki za ndoa ya jinsia moja kwa kuwa tumekuwa dhaifu na hatujulikani tumesimamia wapi zaidi ya kujali mkate wetu wa siku.

  Rais wetu wa kwanza J K Nyerere hakupenda kuchezewa hata na majirani zake ndo maana hayati rais Banda alishindwa kuitetea hoja yake dhaifu ya mpaka wa nchi ya Tanzania na Malawi.Ujasiri ule aliokuwa nao Nyerere leo umegeuka na kuwa udhaifu kwa serikali ya chama kile kile alichokiacha.

  Uchumi wetu umeingiwa na mdororo lakini kila siku tunakabidhi ardhi yetu kwa wageni ambao urafiki wao kwetu hauna tija wala mashiko.Mfumo wa kinyonyaji ulikwisha pita lakini cha ajabu leo uchumi wetu una nyonywa na katabaka fulani kawalafi wachache ambao wametujengea marafiki wa kudumu katika harakati za kuchuma vilivyo vyetu na kutuachia nchi yetu mashimo na mahandaki pasipokuwa na vita.
   
 2. F

  Fenb Member

  #2
  Oct 28, 2012
  Joined: Oct 18, 2012
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkubwa ukifikiri sn na ukajaribu kudadavua jinsi nchi inavyopelekwa unaweza kukaa chini ukalia sn. Cake ya nchi hii inaliwa na watu wachache sn na ambao hawafanyi kazi za kuendeleza nchi ndomaana inatuuma sn. Ukifanya kazi ukala angalau basi tutafumba macho. But hii mijitu ni kukusanya tu bila kufanya kazi yaani inaniuma kupita kawaida. Rasilimali zote tunagawa bila manufaa yoyote na bila uchungu ilimradi tu mtu apate chake. Iweje kama una akili timamu uweke mkataba wa miaka 100? For sure hii nchi imebaki na viatu na sio watu. Tumechokaaaaaa tufanye mabadiliko kwa kuchagua mtu sio chama. Tutafute kiongoz wa watu sio hawa wapuuzi wanaoshindwa kuongoza watuchagulie mtu wa kutuongoza wamemjuaje wakati wao wenyewe hawawezi kuongoza? tafakari chukua hatua.
   
Loading...