Marafiki wa Isaac, aliyekuhumiwa kwa kumtukana Rais, wamchangia mil 4.5 ya faini

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
Marafiki wa Isaac Habakuk pamoja na wadau ambao hawakupendezwa na hukumu dhidi yake ya kwenda gerezani miaka 3 au kulipa faini ya milioni 7 kwa kudaiwa kumtukana Rais Magufuli kupitia mtandao wa Facebook kwa kutumia neno bwege wamemkabidhi jumla ya shilingi milioni 4.5 kwa ajili ya kulipa faini kuepuka kifungo gerezani.

Akikabidhi fedha hizo Jijini Arusha mchana wa leo, mwakilishi wa marafiki hao, Ndg Ephata Nanyaro amesema fedha hizo zimekusanywa kutoka kwa marafiki mbalimbali ambao wametafutana kwa njia ya simu na kila mmoja kuchangia kuanzia sh 500 na kuendelea mpaka zikafika kiasi hicho.

Fedha hizo ni makusanyo ya michango ya makundi mawili, moja likiratibiwa na Ephata Nanyaro na lingine likiratibiwa na Malisa Godilistern, wote wanachama wa Chadema na ambao hutumia mitandao ya kijamii kueleza mawazo yao kuhusu mambo mbalimbali.

Nanyaro amesema wameamua kufanya harambee ya kumchangia kijana mwenzao aepukane na dhahama ya kutotumikia kifungo kwasababu kwa jinsi sheria ya makosa ya mtandao ilivyo, kila mwananchi yuko hatarini kupelekwa gerezani kwa sheria hiyo kwasababu inavifungu ambavyo vinakiuka msingi mkuu na uhuru wa binadamu kuwaza na kujieleza.

Ameviasa vyombo vya Serikali vinavyosimamia sheria, hususani Jeshi la Polisi kutimiza wajibu wao kwa weledi huku wakisimamia sheria zinavyoelekeza tofauti na kitendo alichoeleza hakikustahili na sio haki kumuweka Isaac kizuizini kwa muda wa siku 28 bila dhamana wala kumfikisha Mahakamani kwa kosa ambalo halina kitisho cha hatari.

Akifafanua zaidi, Nanyaro ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Leveolosi ya Jijini Arusha amesema Isaac ataepuka kifungo kwa kulipa faini ya sh milioni 7 kwa awamu mbili ambao mpaka sasa amekwishakabidhiwa hizo milioni 4.5 na michango mingine inaendelea huku ahadi zikivuka kiwango hicho.

Nae Isaac alipopewa fursa ya kuzungumza amewashukuru sana watu wote ambao wamejitolea kumchangia na kueleza kuwa wameonesha upendo wa kipekee na moyo wa ajabu katika kadhia inayomkabili. Amewasihi kuendelea na moyo huo kwa kusaidia na wengine wanapokuwa na uhitaji.
IMG-20160617-WA0063.jpg
IMG-20160617-WA0062.jpg
IMG-20160617-WA0065.jpg
 
kweli watu wa arusha wanajiamini sana nimeamini.

Wabarikiwe na kuongezewa waliomchangia kijana wa watu.

Vipi na siye watanzania tulioitwa malofa?
Watuhumiwa watafikishwa mahakamani au kuna ambao wapo juu ya sheria.

Hii nimichango ya wana Arusha na Watanzania wote walioguswa na hili
 
Mimi binafsi japo nalaani sana sheria hii ya mitandao, lkn huyo kijana alitumia neno kali ambalo sio neno la heshima kwa mtu yeyote awe mzazi, au kwa jamii yetu ya kiafrika. Hivyo natoa wito kwetu vijana, pamoja na kukerwa kote ila tuangalie sana lugha tunayotumia tukizingatia maadili, heshima, busara na hekima.

Pili kwa kuwa tunajua kabisa huyu "ngosha" wa magogoni hapendi kukosolewa, nadhani ingekua busara kutumia lugha nzuri yenye staha. Kutumi lugha ya heshima hakupunguzi wala kuondoa ujumbe tunaopenda kumfikishia.

Mwisho kabisa, tusimpe sababu ya kutufunga kwa gharama nafuu kiasi hiki. Niwapongeze sana waliochangia kwa moyo wao.
 
Mimi binafsi japo nalaani sana sheria hii ya mitandao, lkn huyo kijana alitumia neno kali ambalo sio neno la heshima kwa mtu yeyote awe mzazi, au kwa jamii yetu ya kiafrika. Hivyo natoa wito kwetu vijana, pamoja na kukerwa kote ila tuangalie sana lugha tunayotumia tukizingatia maadili, heshima, busara na hekima.

Pili kwa kuwa tunajua kabisa huyu "ngosha" wa magogoni hapendi kukosolewa, nadhani ingekua busara kutumia lugha nzuri yenye staha. Kutumi lugha ya heshima hakupunguzi wala kuondoa ujumbe tunaopenda kumfikishia.

Mwisho kabisa, tusimpe sababu ya kutufunga kwa gharama nafuu kiasi hiki. Niwapongeze sana waliochangia kwa moyo wao.
Msimeno unatakiwa kukata pande zote
 
Nakubaliana na wewe mkuu, lkn tukumbuke hizi sheria kandamizi watungiwa wapinzani wa watawala. Hilo halina ubishi... Wapinzani na wahanga wanapaswa kulijua hilo na kutoruhusu kufungwa na kulipishwa fine kwa garama nafuu namna hii.

Kwangu mimi, nitamuelewa na kumchangia yule atakaetoa nyaraka na kuibua uozo wa serikali kwa maslahi ya umma. Kwakua sheria inakataza na yeye kwa uzalendo akajitoa mhanga basi hyo anastahili kuchangiwa lakini sio kwa kuita watu mabwege....Too cheap!
 
Hajatukana,ndio maana hata huyo Naibu wenu wa Spika alitumia maneno kwa mbunge "wewe bwege acha ubwege" na hakuombwa hata mwongozo. Katika kamusi hilo neon sio tusi.
Mbewe lile jina lake. Fuatilia matukio yake huwa anajiita hivyo.
 
Back
Top Bottom