Maradhi ya Kiingereza

Makonyeza

Member
Feb 2, 2020
69
252
Mteja: Aisee vipi salama?
Mimi: nipo salama, lete habari
Mteja: Sasa bwana Wakili kumbe yule mteja uliyeniletea anaongea Kingereza?
Mimi: Ndiyo, ni Mzimbabwe, kwani tatizo nini?
Mteja: Aaaah, ungenambia mapema Kaka nijiandae, tumeshindwa kuelewana bwana, na Biashara yenyewe na yeye sitaki tena labda unitafutie mteja mwingine anayejua Kiswahili huyu atanidhulumu.

Niliishia kucheka tu

Kuna siku mteja wangu mmoja alikuwa anauza mali yake fulani, kiukweli ilituchukua muda mrefu sana kupata mteja, ila hatimaye nikampata mwenye kuhitaji bidhaa ile lakini mteja akahitaji kuonana na muuzaji ili ajiridhishe mambo kadhaa, nikawawekea utaratibu waonane wakati mimi nikiendelea na mambo yangu.

Siku ya pili nikapokea simu kutoka kwa yule mteja, sehemu ya mazungumzo yalikuwa kama nilivyoanza hapo juu. Sasa hii ni Ugonjwa hatari sana kwa Watanzania walio wengi, tena ni tatizo kuliko tunavyoliona.
Ugonjwa huu dalili zake ni hizi zifuatazo:

1. Mtanzania ukiongea Kiingereza unaonekana ndiye msomi zaidi.

2. Mtanzania asiyejua Kiingereza au anababaika kukitumia anaonekana kituko mbele za watu.

3. Mtanzania asiyejua Kiingereza yeye mwenyewe anajifanya kuwa duni (inferiority complex), anakosa kujiamini na a nahisi kufedheheka akikosea au akishindwa kuongea Kingereza mbele za watu. Huyu huyu hujitenga, akiona wanaosema Kiingereza wanakuja anajificha asionane nao.

Maradhi haya yanatibika kwa dawa tatu zifuatazo, kwanza kizungumze mara kwa mara bila woga, pili kiishi Kiingereza kwa kukisikiliza, kukisoma na tatu jifunze kwa kutumia kozi fupifupi.
Usikubali huu ugonjwa ukushambulie.

Usininukuu vibaya, sijasema kwamba ili tupande na kuvuna mpunga lazima tujue Kiingereza.

Lugha ni akiba ya maarifa, lugha ni rasilimali na fursa pia. Kiingereza, Kichina, Kifaransa, Kiarabu na Kiswahili ni lugha zinazohitaji wazungumzaji kwa wakati huu. Kuna fursa nyingi ndani yake, kazi kwako.
 
Back
Top Bottom