Mara yangu ya kwanza kumtia machoni Iddi Simba 1980s

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,857
30,205
MARA YANGU YA KWANZA KUMTIA MACHONI IDDI SIMBA 1980s

Ilikuwa miaka ya 1980 tuko nyumbani kwa marehemu Bi. Mruguru bint Mussa, mama yake Ally Sykes Mtaa wa Lindi.

Pametokea msiba Bi. Mariamu, shangazi yake Bwana Ally Sykes amefariki.

Watu wamejazana mtaa umefungwa wanasubiri muda wa mazishi.

Bwana Ally mwenyewe kakaa jamvini kazungukwa na jamaa zake wa Gerezani, wamekukuja kuungananae katika msiba wa shangazi yake.

Watu ni wengi sana.

Bwana Ally yeye mwenyewe ni mzishi sasa leo limemfika ndugu zake wamemwitika kwa wingi sana, wamekuja kumzika.

Bwana Ally kuniona ananita nende nikakae nae mbele.

Basi nanyanyuka pale nyuma nilipokuwa kwa unyonge maana umma mzima unaniangalia watu wanajiuliza huyu anaeitwa mbele pale ana umuhimu gani?

Katika lile jamvi alokuwa Bwana Ally ni “nani aliye nani katika mji wa Dar es Salaam,” Waingereza wanasema “Who is Who,” wenyewe watoto wa Gerezani na Dar es Salaam wametanda.

Iddi Simba alikuwa amekaa jirani ya Ally Sykes.

Amevaa nguo zilizomkaa vyema kapendenza na miwani yake.

Sasa Bwana Ally anawanadia watu, “Nyie mnamjua huyu? Mtoto wa Said pale Kipata mwandishi hodari sana…”

Utambulisho umekwisha nakaa pembeni Ally Sykes na Zuberi Mtemvu wanashambuliana kwa maneno.

Bwana Ally kalalamika kuhusu hali ya nchi mambo hayendi vyema.

Zuberi Mtemvu kadakia anawashahidisha watu, “Jamani mnasikia Ally analalamika ati mambo hayendi sawa…”

Mtemvu anaangua kicheko cha kejeli huku akitingisha kichwa.

Watu sasa weshakuwa hadhir wanasubiri Mtemvu atasema kitu gani?

“Huyu Ally na marehemu kaka yake Abdul (Mungu amrehemu) walikuwa wanashirikiana na Nyerere kukipiga vita chama changu kife, leo Ally huyu huyu keshageuka ati nchi imeharibika…”

Wasikizaji wanacheka wengine wanamuunga mkono Bwana Ally wengine Zuberi Mtemvu.

Bwana Ally hakubali kushindwa anarudisha kombora, “Ala kumbe Congress bado mko hadi leo nilidhania tulishakumalizeni.”

Vicheko.

Mzee mmoja kwa mbali anaita, “Ally sikiza bwana, Congress tupo sana. Congress ni mwamba usiovunjika.”

Vicheko vinaendelea.

Hii “Congress ni mwamba usiovunjika,” ni maneno yaliyokuwa katika nyimbo ya Congress wakati wa harakati za kudai uhuru.

Watu wametulia Bwana Ally akafahamu kuwa Mtemvu alikuwa hamjui Iddi Simba na pale akawatambulisha.

Nilishangaa sana vipi miamba hii yote ya Gerezani isifahamiane.

Hapo nami ndipo nikamfahamu Iddi Simba ingawa jina lake lilikuwa maarufu katika vyombo vya habari kila inapotajwa East African Development Bank iliyokuwa na makao makuu yake Kampala Uganda.

Kuanzia hapo Mzee Iddi Simba kila tutakapokutana atakuwa na la kunieleza.

Mzee Iddi Simba alikuwa na kawaida kila akimaliza kusali Dhuhr Msikiti wa Manyema hatoki atakenda kukaa nyuma ya msikiti na jamaa zake watamfuata pale.

Nami hii ndiyo ilikuwa fursa yangu ya kusalimiananae kila nikiswali Msikiti wa Manyema na hapo utamkuta kakaa na rafiki yake kipenzi Muharam Kocha.

Napenda kuhitimisha kwa kueleza kisa kimoja.

Anur Suleiman alipata kuwa Mkuu wa Mkoa Mwanza katika miaka ya 1970/80.

Huyu bwana alikuwa anajenga msikiti sikumbuki kama ni kwao Bukoba au Mwanza.

Akaleta vitabu vya risiti kwa ajili ya kuchangisha nami nikapewa kimoja nichangishe hapa Dar es Salaam.

Basi siku hiyo nikamkuta Mzee Iddi Simba kakaa kwa Daddy huyu alikuwa fundi cherehani maarufu Kariakoo karibu na Saigon ya zamani, Mtaa wa Sikukuu.

Katika maisha yangu hadi hii leo sijawahi kuchangisha kitu chochote nikapata fedha nyingi kama nilizopata katika mchango huu kiasi hata yule aliyenipa kitabu kile alipigwa na butwaa.

Nikamfuata Mzee Iddi Simba kakaa pale kwenye benchi na vijana wa Saigon mtu akikwambia ukubwa wa mtu huyu na hadhi yake utakataa utajiuliza pale anafanya nini?

Mzee Iddi Simba akanisikiliza kisha akabaki kimya hakunambia chochote nami nikaondoka.

Nilidhani hakutaka kunipa mchango.

Baadae kidogo akanifanyia ishara nimfuate.

Fedha alizonipa kama mchango wake wa msikiti zilinishtua na naamini wale waliokuwa wakitaka kuchanga wanataka kwanza waangalie nani na nani washachanga bila shaka mchango ule uliwatia motisha angalau na wao watoe kingi wamkaribie Iddi Simba.

Allah amfanyie wepesi mzee wetu safari yake na amsamehe.

Amin.

IDDI SIMBA 2010.jpeg

PICHA: Mzee Iddi Simba na Mheshimiwa Mussa Azzan Zungu katika futari ya Saigon mwaka wa 2010
 
Hivi wazee wa upande wa pili wa kikristo huwa huna story zao??
3 Angels,
Haya usomayo kutoka kwangu ndiyo mazingira niliyokulia katika Dar es Salaam ya 1950s kuelekea 1960s.

Dunia yangu yote ilikuwa Mtaa wa Kipata, Livingstone, Kiungani kwa bibi, shangazi na wajomba.

Hizi ndizo kumbukumbu zangu nyingi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pumzika kwa amani mzee wetu IDDI SIMBA.

Kuna kisa kimoja nimepata kukisikia kutoka kwake mwenyewe kuwa chanzo cha VITA YA KAGERA. Yeye alitakiwa kuwa chambo cha vita kuanza mara moja kipindi hicho yeye alikuwa anaishi KAMPALA kama Rais wa EAST AFRICA DEVELOPMENT BANK.

Kisa hiki mpaka IDDI AMIN alimfanya mateka Mzee Simba akiwa nyumbani kwake mtaa wa NTINDA VIEW JIJINI KAMPALA. Kuna sehemu nimeruka (Pana muhusu Nyerere) panaogofya sana juu ya IDDI SIMBA.

Mzee wangu Mohamed said ujapata kuckia icho kisa? Nidokeze PM kwa uhakika zaidi.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Pumzika kwa amani mzee wetu IDDI SIMBA.

Kunakisa kimoja nimepata kukisikia kutoka kwake mwenyewe kua chanzo cha VITA YA KAGERA. Yy alitakiwa kua chambo cha vita kuanza mara moja kipindi icho yy alikua anaishi KAMPALA kama raisi wa EAST AFRICA DEVELOPMENT BANK.

Kisa hiki mpaka IDDI AMIN alimfanya mateka mzee simba akiwa Nyumbani kwake mtaa wa NTINDA VIEW JIJINI KAMPALA. Kuna sehemu nimeruka (Pana muhusu nyerere) panaogofya sana ju ya IDDI SIMBA. Mzee wangu Mohamed said ujapata kuckia icho kisa?.

Nidokeze PM kwa uhakika zaidi.

Sent from my iPhone using JamiiForums
Kawombe,
Hicho kisa sijakisikia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Alikuwa tajiri sana huyu, bilionea mkubwa sana, alianzisha taasisi ya kutoa mikopo ya riba PRIDE TANZANIA, amesaidia watu wengi kwenye mikopo yake
 
Allah ampe kauli thaabet Mwamba katika Miamba ya Jiji la Dar es salaam

Huyu Gwiji Barua yake ya Kujiuzulu Mkapa alimkubalia kwa Masharti kuwa kujiuzulu kwake kuanze baada ya kwenda kuwakilisha Nchi kwny Mkutano wa Mabeberu huko Ng'ambo

Mzee Mkapa sio mzuri wa kuhudhuria Misiba n ukiomuona kahudhuri jua kaguswa na akagusika

Zengwe la kashfa ya Sukari alisukiwa na Genge la Wasaka Urais ambao hawakuupata

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mohamed Said anazungumzia Watu wa eneo la Kariakoo na Viunga vyake ambako ndio eneo alilokulia

Nanyi Zungumzieni watu wa Maeneo yenu

Mkomunist Nsa Kaisi tunamsafirisha muda huu kwenda Mbeya, sasa Msisubiri Mohamed Said amzungumzie, nyie wa Mbeya uwanja wa Jf ni huru, tuwekeeni historia ya Wazee wenu
Hivi wazee wa upande wa pili wa kikristo huwa huna story zao??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
3 Angels,
Haya usomayo kutoka kwangu ndiyo mazingira niliyokulia katika Dar es Salaam ya 1950s kuelekea 1960s.

Dunia yangu yote ilikuwa Mtaa wa Kipata, Livingstone, Kiungani kwa bibi, shangazi na wajomba.

Hizi ndizo kumbukumbu zangu nyingi.

Sent using Jamii Forums mobile app
For someone like yourself who was able to rise out of your impoverished Swahili ghetto existence, cross the seven seas and had a chance to meet plenty of great minds of all races and religious persuasions. You only ever rush to pay tribute with your signature tales whenever some Muslim person, however insignificant the person, passes away, all the while making sure to sneak in the Sykes name, at whatever cost, in-between the lines.
 
Nonsense. You are just a narrow minded fool, and and nobody's buying this flimsy excuse as an explanation for your entrenched religious bigotry, specially for someone like yourself who was able to rise out of your impoverished Swahili ghetto existence, cross the seven seas and had a chance to meet plenty of great minds of all races and religious persuasions. You only ever rush to pay tribute with your signature tales whenever some Muslim person, however insignificant, passes away.
Mbona hapa wewe ndio umeonekana mpumbavu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Allah ampe kauli thaabet Mwamba katika Miamba ya Jiji la Dar es salaam

Huyu Gwiji Barua yake ya Kujiuzulu Mkapa alimkubalia kwa Masharti kuwa kujiuzulu kwake kuanze baada ya kwenda kuwakilisha Nchi kwny Mkutano wa Mabeberu huko Ng'ambo

Mzee Mkapa sio mzuri wa kuhudhuria Misiba n ukiomuona kahudhuri jua kaguswa na akagusika

Zengwe la kashfa ya Sukari alisukiwa na Genge la Wasaka Urais ambao hawakuupata

Sent using Jamii Forums mobile app
Urais waliupata. Usitishwe na akina Mzindakaya, yeye alikuwa anacheza timu ya ushindi nyuma ya pazia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hasira zote hizi ni kwa kuwa kamzungumzia Mzee wake Iddy Simba kuna lingine?

Mohamed Said ni mtu wa Dar es salaam na anazungumzia watu wa Dar es salaam wa zama hizo ambao wengi ni Waislam,
Ni sawa na kumlaumu Mwandishi Mkongwe Dr Harrison Mwakyembe akianza kutuletea Taazia za Wazee wake wa Kyela ukahoji mbona wote ni Wakristo wakati unajua population kubwa ya watu wa kule ni Wakristo

Toka nje ya Box utafakari na kutafakuri Kijana kabla ya ku panic

Kila mtu azungumzie Watu anaowajua, mnataka alete Taazia ya kina Nsa Kaisi, Daniel Moi sijui Ndesamburo ataanzia wapi, huu ni ukumbi wa wote, nanyi tuleteeni story za Wazee wenu hamjakatazwa, sie Wasomaji tutasoma na kuchangia
For someone like yourself who was able to rise out of your impoverished Swahili ghetto existence, cross the seven seas and had a chance to meet plenty of great minds of all races and religious persuasions. You only ever rush to pay tribute with your signature tales whenever some Muslim person, however insignificant the person, passes away, all the while making sure to sneak in the Sykes name, at whatever cost, in-between the lines.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hasira zote hizi ni kwa kuwa kamzungumzia Mzee wake Iddy Simba kuna lingine?

Mohamed Said ni mtu wa Dar es salaam na anazungumzia watu wa Dar es salaam wa zama hizo ambao wengi ni Waislam,
Ni sawa na kumlaumu Mwandishi Mkongwe Dr Harrison Mwakyembe akianza kutuletea Taazia za Wazee wake wa Kyela ukahoji mbona wote ni Wakristo wakati unajua population kubwa ya watu wa kule ni Wakristo

Toka nje ya Box utafakari na kutafakuri Kijana kabla ya ku panic

Kila mtu azungumzie Watu anaowajua, mnataka alete Taazia ya kina Nsa Kaisi, Daniel Moi sijui Ndesamburo ataanzia wapi, huu ni ukumbi wa wote, nanyi tuleteeni story za Wazee wenu hamjakatazwa, sie Wasomaji tutasoma na kuchangia

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyu mzee tunamjua ni mdini na ajenda yake ya udni tunaijua, kwa hiyo kila kitu tunaweka kwenye context kubwa. Yeye kukulia Gerezani siyo sababu ya kuchagua nani wa kumtukuza au nani muhimu kwake sababu tu Waislamu kama vile watu wote wa maana aliokutana nao maishani mwake ni Waislamu watupu tokea alipozaliwa Gerezani hadi leo hii na uzee wake sijui umri gani. Kama huamini, pitia mabandiko yake yote ujiridhishe. Hata Marehemu iddi Simba sidhani kama walikuwa wana uhusiano wa karibu naye, ni basi tu, imetokea kwamba Marehemu alikuwa Mwanasiasa Mkongwe na muumini wa dini ya Kiislam, hapo Mzee Mohamed Said kaona fursa kaamua kuja na stories zake na bila kusita kupenyeza jina la Sykes humo humo.
 
Sasa taja Mtu wa Gerezani ambae hakuwa Mwislam ambae alipaswa kumzungunzia na yeye hakumzungumzia!

Inawezekana Wewe ndie mdini na unamtazama kwa mlengo wa Udini na ndio sababu unamuona Mdini

Kwanini nyinyi hamleti Taazia za Wazee wenu ambao Mohamed Said hataki kuleta?

Kwa hoja yako hapo juu unamaanisha huyo mzee Mohamed Said alizaliwa Gerezani na kukulia hapo tokea kichanga hadi kikongwe miongoni mwa Waislamu tu bila kukanyaga hata Upanga kwa Wahindi - sembuse majigambo yake ya kusafiri mabara karibia yote duniani ? Mzee ambaye anadai kasoma shule ya wamisionari Saint Joseph's School? Halafu unaandikaje taazia ya mtu ambaye anakiri mwenyewe hawakufahamiana kihivyo sababu tu ni Muislamu wa Gerezani? Mfano mdogo, walimu wake enzi hizo Masista wa Kizungu wa St Joseph's School, nadhani wengi kama siyo wote, watakuwa washafariki zamani lakini sijawahi kuona akiwakumbuka kwa mchango wao katika elimu yake.
 
Back
Top Bottom