Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 71,277
- 105,478
Wadogo zangu walikuja kunitembelea likizo, kama ilivyo ada kila mwaka miaka hii ya karibuni...I dont feel like he is offering anything that is not known, or he is setting any record straight.
..sina uhakika kama kitakuwa kizuri kama kitabu cha Mzee Mtei au Conrad Mselle ambao ni watata kidogo na walikuwa na "makaburi ya kufukua."
Cc Kiranga
Basi wakaniuliza, kaka mkubwa tukuletee zawadi gani? Swali tata sana hili.
Nikaomba waniletee asali ya Tanzania na kitabu cha Mkapa.
Kitabu kilikuwa "out of print", zikapigwa simu mpaka kikapatikana, nikaletewa.
Nikakisoma kwa hamu, kwa kituo. Kwa jicho la mtu anayeijua familia ya Mkapa si kwa kupitia magazeti na siasa, bali kama mtu niliyekua na watoto wa familia Upanga.
Kusema kweli, Mzee Mkapa katupiga chenga tu na hiki kitabu. Ni muhimu kukisoma, lakini kwa caliber ya muandishi kama yeye, alichofanya kwenye kitabu hiki ni kutoa muhtasari wa mambo machache tu, na hata hayo kayaongelea kijuu juu tu.
Mfano, alivyoelezea jinsi alivyoingizwa kingi kwenye issue ya EPA, yani ukisoma unaona kabisa hapa mshua anatumia kitu kinaitwa "plausible deniability". Mkapa ni mtu meticulous sana, sana tu, na si mtu wa kudanganywa kitoto vile.
Ila, naona kaona afadhali apate fedheha ya kujifanya alikuwa mjinga, kuliko kupata lawama ya kwamba alikuwa "fisadi".
Ni kitabu kizuri kama unataka kujua historia ya maisha ya awali ya Mkapa, ingawa hata kwenye familia nako ameshindwa hata kumtaja Peter kama mtoto wake wa kufikia, ukisoma utafikiri Nick na Stephan ndio watoto pekee, lakini kama unataka kujua mambo kwa undani, Mkapa kabakisha maneno mengi sana kuliko aliyoandika. Kuanzia alivyokuwa anamwambia Nyerere kwamba Kambona anamsengenya, na Nyerere akiwa haamini anam dismiss Mkapa, mpaka ukweli kuhusu alivyokubali kupiga dili la EPA.
Kabla ya kusoma kitabu cha Mkapa, nilikuwa nasoma kitabu cha balozi wa serikali ya Marekani chini ya Obama hapo UN, Samantha Power, kinaitwa "The Education of An Idealist: A Memoir". Ukisoma wenzetu wanavyozama katika kueleza maisha yao na maamuzi waliyochukua wakiwa madarakani, halafu ukasoma kitabu cha Mkapa, utaona kitabu cha Mkapa kimejaa habari za "danganya toto, kula kunde, nyama mbichiii".
The book is full of plausible deniability, omissions,obfuscation, conveniently late conversions to being a democrat, the list goes on.
In short, the book is an insults to our collective intelligence.