Mara ya kwanza kuingia kwenye Freemason Lodge - True Story

Hizi CD mnazozinunua zitawadanganya sana kuhusu FREEMASON... wenye freemason yao wanawachekeni sana kwa dharau wakiona ni jinsi gani watu wanakosa akili kufuatilia mambo yasio na msingi.

Natamanigi sana kuwaambia watu kuacha kufuatilia huu ujinga. Hizi ni njama za wazungu kuendelea kuchelewesha maendeleo Africa.

Watataka muendelee kutumia muda wenu kujadili issue zisizo add value na kuwatoa kwenye reli. Matokeo yake siku upo unakata roho unagundua kwamba uelewa ulioutafuta kuhusu kujua freemason haujakusaidia chochote kufanya maisha yako yawe bora na utimize lengo la muumba hapa duniani maana unagundua hakuna cha msingi ulichokijua zaidi ya kujaza ubongo wako na mambo ya kijinga na ukasahau kufanya ambacho kimekuleta duniani --> (kuboresha)

Huu mda unaoutumia ku google kuhusu freemason ama uki google wasanii ambao ni Freemason ungeweza kabisa kutosha kutengeneza wazo la kufungua mgahawa wa juice na vitafunwa kwa huo mshahara wako wa muhindi wa laki tano.

Freemason thing inaweza kuwa ni kweli na mimi nakubali lakini as a person from Tanzania. Does it add any value by just want to know about it?

TUACHE HUU UPUMBAVU ONCE AND FOR ALL
This is the best comment ever in jf. God bless you

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nawasalimia ndugu zangu wana JF. Katika harakati zangu hizi za kitafiti, mwaka 2008 niliweza kuingia kwenye Lodge ya Freemason.
Niliomba mara nyingi sana niweze kujiunga na ndugu zetu. Lakini mwaka 2008 nilifanikiwa baada ya kukaribiswha na Dr. Hans Van Dirck. Ndugu zangu walijuzwa, hata mke wangu kipenzi naye alifahamishwa kuhusu jambo hili.

Kabla ya kukaribishwa nilisomewa mashart kama nitaweza kuyafuata. Shart kubwa kabisa ni kwamba: You must believe in a Supreme Being.
Ilikuwa mida ya Jioni saa 12 hivi nikiwa nyumbani kwangu nilipigiwa simu. Niliipokea simu hiyo, mtu huyo alikjitambulisha jina lake, na akaniambia kuwa mida ya saa tatu usiku ninatakiwa kufika kwenye Lodge ya Freemason iliyopo Posta Dar es salaam kwaajili ya utambulisho.

Nilifurahi sana na kuanza kujiandaa wakati huo. Mida ya saa mbili tayari nilikuwa nimeshafika Posta. Mapigo yangu ya moyo yalidunda kidogo kidogo. Kisha nilianza kuelekea sehemu husika. Nilifika getini na kujitambulisha kama nilivyoambiwa. Nilikaribishwa na kuingia ndani reception na kuandikisha jina langu. Nilikaribishwa na kupelekwa kwenye chumba kimoja kwaajili ya kusubiri muda ufike.

Kwenye chumba kile kulikuwa na chakula, vinywaji, matunda nk. Nilikaribishwa kupata chakula. Baadae watu wengi tu walianza kuingia wakiwa wamevalia nguo za kufanana. Yaani Makoti meusi yenye alama kwenye mabega huku kiunoni wamefunga kitambaa chenye rangi nyeupe na nyekundu.

Nilielekezwa kuenda kwenye chumba cha kubadili nguo ili niweze kuvyaa nguo kwaajili ya ritual. Nilienda kwenye chumba hicho, kilikuwa kimesheheni nguo mbalimbali na masanduku ya kung'aa. Nilioneshwa sehemu ambayo nguo zipo. Nilienda kuchukua nguo inayonienea na kisha kutoka.

Tuliingia kwenye chumba cha ibada. Ndani ni ukumbi mkubwa wenye viti vizuri. Mbele kulikuwa na altar (Madhabahu) kubwa iliyopambwa na marumaru, vito na madini mazuri. Juu ya madhabahu hiyo kulikuwa na kitabu kikubwa, mishumaa saba ilikuwa ikiwaka na kitambaa kilichochorwa maumbo kadhaa. Nilielekezwa sehemu ya kukaa.

Mtu mmoja(Master) aliingia watu wato waliinama na kusema maneno kadha wa kadha, huku wakiwa wamesimama. Na mimi nilifuatisha taratibu hizo.

Ibada ilianza Master alifungua kitabu na kusoma maneno kadhaa kisha wengine walirudia maneno hayo. Baadaye jina langu liliitwa na nikaambiwa niende mbele. Nilifungwa kitambaa kwenye macho yangu na kuanza kusomewa maagano. Nilitakiwa kujibu ndio au hapana katika maagano niliyokuwa ninasomewa. Baada ya kusomewa maagano hayo nilipigwa muhuri kwenye bega langu la kulia. Kisha kitambaa kikafunguliwa kwenye macho yangu. Nilielekezwa kwenda kwenda kwenye chumba kingina. Na ndani ya chumba hicho kulikuwa na kibwawa kidogo. Nikaambiwa hili ni bwawa la utakaso ninatakiwa nipite kwenye kibwawa hicho na kuzwamishwa mara saba. Nilifanikiwa kupita kwenye kibwa hicho na kutokewa upabde wa pili. Baada ya hapo niliambiwa You are Welcome.

Niliambiwa sasa nitaanza mafunzo ya how to be a Man. Na niliambiwa kuwa we want to build you to be a better man for better world.

Karibuni kasana. Kama kuna mtu mwenye swali.

kidogo wewe ndio mtu wa kwanza kuandika jambo lenye ukweli ukweli juubya ufreemasons, nalo ni kuwa, they make men to be better men for the world

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizi CD mnazozinunua zitawadanganya sana kuhusu FREEMASON... wenye freemason yao wanawachekeni sana kwa dharau wakiona ni jinsi gani watu wanakosa akili kufuatilia mambo yasio na msingi.

Natamanigi sana kuwaambia watu kuacha kufuatilia huu ujinga. Hizi ni njama za wazungu kuendelea kuchelewesha maendeleo Africa.

Watataka muendelee kutumia muda wenu kujadili issue zisizo add value na kuwatoa kwenye reli. Matokeo yake siku upo unakata roho unagundua kwamba uelewa ulioutafuta kuhusu kujua freemason haujakusaidia chochote kufanya maisha yako yawe bora na utimize lengo la muumba hapa duniani maana unagundua hakuna cha msingi ulichokijua zaidi ya kujaza ubongo wako na mambo ya kijinga na ukasahau kufanya ambacho kimekuleta duniani --> (kuboresha)

Huu mda unaoutumia ku google kuhusu freemason ama uki google wasanii ambao ni Freemason ungeweza kabisa kutosha kutengeneza wazo la kufungua mgahawa wa juice na vitafunwa kwa huo mshahara wako wa muhindi wa laki tano.

Freemason thing inaweza kuwa ni kweli na mimi nakubali lakini as a person from Tanzania. Does it add any value by just want to know about it?

TUACHE HUU UPUMBAVU ONCE AND FOR ALL
Naunga mkono hoja ..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watanzania wapumbavu sana mtu akishajua tu kutamka neno freemason inakuwa shida,hata hao watu kina diamond sijui kina nani wanaodaiwa kuwa freemasons ni uzushi tu watu walio freemasons ni watu wakubwa sio vikina diamond
 
Back
Top Bottom