PostGE2025 Mara nyingine mipango ya CCM siielewi

PostGE2025 Mara nyingine mipango ya CCM siielewi

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

comrade_kipepe

JF-Expert Member
Joined
Jun 25, 2019
Posts
6,465
Reaction score
11,535
Kuna namna wanafanya vitu kwa mihemko, kuna watu kabisa wanaonekana hawakua na kesi lakini wakawapa kesi ya uhaini bila kujua hao watu ndio wanawatengeneza kua wapinzani wao.

Mtu wanajua kabisa hana kesi na hana madhara, yanini kumpaisha na kumbrand maana mwisho wa siku atatoka maana kesi hamna na akitoka anakua washamtengeneza kua mpinzani wao.

Mfano huyu jamaa Mika Chavala wengi tulikuwa hatumjui lakini CCM ndio wametulazimisha tumjue, jamaa umaarufu wake umeongezeka maradufu akiwa nyuma ya nondo! Kajiongezea kijiji kirahisi sana, kaonekana shujaa wakati hata haikutakiwa iwe hivyo.

Mi naona kabisa CCM inajitengenezea maadui na wakosoaji kila kukicha, kuna waliokua hawampendi lisu, lakini wanapompitisha lissu anazidi kujipatia wafuasi, wengine wanakua wafuasi wake kwasababu tu ya kumuhurumia anayopitia.

Yani mipango ya ccm mara nyingine siielewi kabisa.
 
Acha wajikaange kwa mafuta yao wenyewe, wakiiva wataliwa!
 
Sasa kama kiongozi mkuu wao ndio yuko vile unafikiri watakuwa wanafanya yap!?
 
Back
Top Bottom