Hofu ya CCM ya Magufuli 2020 ni Hatari kwa nchi

Zitto

Former MP Kigoma Urban
Mar 2, 2007
1,551
2,000
HOFU ya CCM ya Magufuli ni Hatari kwa Nchi yetuKwa wiki moja sasa kumekuwa na mjadala mkali nchini kuhusu Tamko lililotolewa na Makatibu Wakuu wastaafu wa CCM Kanali Abdulrahman Kinana na Luteni Yusuf Makamba kuhusu mtu anayeitwa Cyprian Musiba. Wana CCM hao wameandika malalamiko yao kwa Baraza la Wazee wa Chama chao ili hatua zichukuliwe. Katika hali ya kawaida hili lilipaswa kuwa jambo la CCM na kushughulikiwa na chama hicho wenyewe. Hata hivyo jambo hilo limechukua mkondo wa kitaifa na haswa usalama wa watu na usalama wa Taifa.Tamko la Kanali Kinana na Luteni Makamba limeujulisha Umma mipango dhalimu ya kubumba kesi za uhaini kwa Wanasiasa waandamizi nchini kutoka Chama Tawala na Vyama vya Upinzani. Pia baadhi ya wana harakati ambao Bwana Musiba amekuwa akiwataja kuwa ni watu hatari kwa nchi ni miongoni mwa wahanga wa mipango hiyo. Kina Kinana wametibua mpango huo ndio maana wafuasi au wanaojiita wanaomwunga mkono Rais Magufuli wametaharuki na wanajaribu sana mipango yao iendelee. Shabaha ya kesi ya uhaini ni kuhakikisha ama mwaka 2020 hapatakuwa na uchaguzi au uchaguzi ufanyike wakati wanasiasa wote waandamizi nchini wakiwa magerezani au wasiwepo kabisa.Baadhi ya wanasiasa wameanza kujiokoa kwa kujiegemeza upande wa wenye mamlaka. Hata wale ambao kwa muda sasa wamekuwa ni tumaini la Wananchi kwa kuwa wakosoaji wakuu wa Serikali wamerudi nyuma na kutoa kauli za kujikosha . Kwa mfano mtu ambaye amekuwa akikosoa vikali Serikali kule mwanzo nia ilikuwa ni kumnyima uhalali Rais Magufuli ? Mbona wakati wa Uongozi wa Rais Jakaya Kikwete alikuwa anashambuliwa sana na Wazee kama vile Mzee Butiku, Warioba nk lakini hatukusikia haya? Kitu gani ‘special’ wakati huu? Nadhani huu Ni wakati kwa wapenda demokrasia wote kutoogopa na kuwa pamoja.Sisi wengine tunajua kitambo kuwa CCM imeshafika mwisho wake. Bahati mbaya sana CCM ya Magufuli inataka kuondoka na nchi yetu. Tusikubali. Tumesoma kuwa kabla ya Wazee hao wastaafu wa CCM kuandika, waliomba ushauri na Mzee Pius Msekwa akawaambia ‘jibuni Mapigo’. Ina maana Msekwa naye anataka kuua Chama chao? CCM ianguke yenyewe na ituachie nchi yetu.Hofu ya Watawala kuhusu 2020 isihatarishe nchi yetu. Mipango ya Kesi ya Uhaini iachwe mara moja. Ukosoaji ndani au nje ya vyama vya Siasa kamwe haiwezi kuwa uhaini. Acha demokrasia ishamiriZitto Kabwe

18/7/2019
 

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,520
2,000
-HOFU ya CCM ya Magufuli ni Hatari kwa Nchi yetu

Kwa wiki moja sasa kumekuwa na mjadala mkali nchini kuhusu Tamko lililotolewa na Makatibu Wakuu wastaafu wa CCM Kanali Abdulrahman Kinana na Luteni Yusuf Makamba kuhusu mtu anayeitwa Cyprian Musiba. Wana CCM hao wameandika malalamiko yao kwa Baraza la Wazee wa Chama chao ili hatua zichukuliwe. Katika hali ya kawaida hili lilipaswa kuwa jambo la CCM na kushughulikiwa na chama hicho wenyewe. Hata hivyo jambo hilo limechukua mkondo wa kitaifa na haswa usalama wa watu na usalama wa Taifa.

Tamko la Kanali Kinana na Luteni Makamba limeujulisha Umma mipango dhalimu ya kubumba kesi za uhaini kwa Wanasiasa waandamizi nchini kutoka Chama Tawala na Vyama vya Upinzani. Pia baadhi ya wana harakati ambao Bwana Musiba amekuwa akiwataja kuwa ni watu hatari kwa nchi ni miongoni mwa wahanga wa mipango hiyo. Kina Kinana wametibua mpango huo ndio maana wafuasi au wanaojiita wanaomwunga mkono Rais Magufuli wametaharuki na wanajaribu sana mipango yao iendelee. Shabaha ya kesi ya uhaini ni kuhakikisha ama mwaka 2020 hapatakuwa na uchaguzi au uchaguzi ufanyike wakati wanasiasa wote waandamizi nchini wakiwa magerezani au wasiwepo kabisa.

Baadhi ya wanasiasa wameanza kujiokoa kwa kujiegemeza upande wa wenye mamlaka. Hata wale ambao kwa muda sasa wamekuwa ni tumaini la Wananchi kwa kuwa wakosoaji wakuu wa Serikali wamerudi nyuma na kutoa kauli za kujikosha . Kwa mfano mtu ambaye amekuwa akikosoa vikali Serikali kule mwanzo nia ilikuwa ni kumnyima uhalali Rais Magufuli ? Mbona wakati wa Uongozi wa Rais Jakaya Kikwete alikuwa anashambuliwa sana na Wazee kama vile Mzee Butiku, Warioba nk lakini hatukusikia haya? Kitu gani ‘special’ wakati huu? Nadhani huu Ni wakati kwa wapenda demokrasia wote kutoogopa na kuwa pamoja.

Sisi wengine tunajua kitambo kuwa CCM imeshafika mwisho wake. Bahati mbaya sana CCM ya Magufuli inataka kuondoka na nchi yetu. Tusikubali. Tumesoma kuwa kabla ya Wazee hao wastaafu wa CCM kuandika, waliomba ushauri na Mzee Pius Msekwa akawaambia ‘jibuni Mapigo’. Ina maana Msekwa naye anataka kuua Chama chao? CCM ianguke yenyewe na ituachie nchi yetu.

Hofu ya Watawala kuhusu 2020 isihatarishe nchi yetu. Mipango ya Kesi ya Uhaini iachwe mara moja. Ukosoaji ndani au nje ya vyama vya Siasa kamwe haiwezi kuwa uhaini. Acha demokrasia ishamiri

Zitto Kabwe
18/7/2019
 

TADPOLE

JF-Expert Member
Nov 18, 2015
1,476
2,000
stone anatakiwa ajitafakari kuna kitu anakilea kwa mikono miwili na hicho ndicho kinachoamsha hasira za magamba wenzie..kitu hicho ni uwepo wa ndugu alhaji Bashite...akijua anapokosea hasaa suluhu inaweza kupatikana lakini ushauri kwa nyie wapinzani 2020 ndio mwaka wa kuitoa ccm madarakani maana vita ya panzi ni furaha ya kunguru msipoweza hapo wewe mweshimiwa jepesi na wapinzani wengune hakika tukutane ahera tu maana hakuna namna
 

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Oct 20, 2014
9,759
2,000
Isemwe ukweli tu, makundi hasimu na wenye mitazamo tofauti ndani ya CCM yamekuwepo toka enzi za Mwalimu.
Tofauti iliyopo saa ni kushindwa kwa Mwenyekiti kuyabalance makundi hayo kwa kuyapa vyeo, nyadhifa na hata kuyakusanya kwa dinner pamoja.

Kutumia mabavu si suluhisho maana hiyo italeta mtafaruku mbaya aidi.
Hivi kuna ubyaa gani Mwenyekiti akiwaita wale anaotofautiana nao ndani ya CCM, wakakaa pamoja, pasuliana ukweli behind closed doors na kutoka na tamko la Umoja?

Yanayoendelea yataliangamiza Taifa na Umoja wake kama tunavyolifahamu.
 

Volatility

JF-Expert Member
Aug 22, 2018
3,128
2,000
Lakini busara itumike, huyu bwana magufuri wote tayari tunajua yuko tayari kuua watu ilimradi analotaka yeye liwe, sasa hii hofu yake inavyoongezeka ndio raia wengi zaidi uhai wao unakuwa matatani.

Nashauri, kama inawezekana ahakikishiwe kuwa rais mpaka 2025 akili yake itulie, nashauri tu.
 

respect wa boda

JF-Expert Member
Nov 14, 2013
4,538
2,000
Shida ya wewe ndugu yangu Zitto ni kuweka mada mezani kisha unatokomea kusikojulikana..

Nadhani ingekuwa vyema unapoweka au kuanzisha mjadala then kaa tuudadavue kwa pamoja siyo kuturushia tu halafu unapotea.. ukifanya hivyo unakuwa huna tofauti na yule bongo muvi aliyewarushia fedha waandishi kisha kabaki pembeni akiangalia wanavyovunjiana vifaa vyao vya thamani..

Anyway narudi kwa hoja yako soon... Acha vijana tuufaidi uwezo wako wa kudadavua mambo usibane..!!

BACK TANGANYIKA
 

IGWE

JF-Expert Member
Feb 3, 2011
9,323
2,000
....mkitishiwa mtaogopa tu
....wapinzani wa TZ ni waoga pengine kuliko wapinzani wa nchi yoyote Africa
...kukaa sana CCM madarakani sio kwamba ni bora sana kuliko vyama vingine Africa vilivyoanguka NO...ni aina ya viongozi wa upinzani tulionao Tanzania -...mnataka kuonewa huruma na ccm .pathetic
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom