PreGE2025 Mara: Matukio yanayojiri kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

PreGE2025 Mara: Matukio yanayojiri kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
4,783
Reaction score
14,975

WanaJF,​

Mada hii itakuwa na 'Updates' za Matukio kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Urais, Ubunge na Udiwani 2025 kama yanavyotujia kutoka kwenu kutoka mkoa wa Mara. Ukiwa na taarifa yoyote ambayo ni ya eneo hili tafadhali usisite kuweka.

Mara.jpg

Mkoa wa Mara uko Kaskazini Magharibi mwa Tanzania, una historia tajiri na ya kipekee inayohusisha makabila mbalimbali, harakati za uhuru, na urithi wa kihistoria wa ukanda wa Ziwa Victoria. Mkoa huu hukaliwa na makabila ya Wakuria, Wajita, Waluo, Wazanaki, Waisenye, na Wagusu

MUHTASARI WA MAENEO YA UTAWALA, MKOA WA MARA
Katika muhtasari wa maeneo ya utawala, mkoa huu una halmashauri ambazo zimegawanyika katika mamlaka za miji na wilaya.

Idadi ya Watu
Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 yanaonesha kuwa idadi ya watu katika Mkoa wa Mara ni 2,372,015; wanaume 1,139,511 na wanawake 1,232,504, yenye jumla ya wilaya 7.

Idadi ya Majimbo ya Uchaguzi
Mkoa wa Mara una jumla ya Majimbo ya uchaguzi Kumi
  • Jimbo la Musoma Mjini
  • Jimbo la Musoma Vijijini
  • Jimbo la Rorya
  • Jimbo la Butiama
  • Jimbo la Bunda Mjini
  • Jimbo la Bunda
  • Jimbo la Serengeti
  • Jimbo la Tarime Mjini
  • Jimbo la Tarime Vijijini
  • Jimbo la Mwibara
HALI YA UCHAGUZI MKUU 2020

Hayati John Magufuli kupitia CCM alipata kura nyingi, akishinda kwa zaidi ya asilimia 80.

Katika Ubunge, CCM ilifanikiwa kushinda majimbo yote, huku CHADEMA ikipoteza baadhi ya ngome zake muhimu kama jimbo la Tarime Mjini, Tarime Vijijini, Bunda

Kwa upande wa udiwani, CCM pia ilishinda kata nyingi, na kufanya mkoa wa Mara kuongozwa zaidi na chama tawala kwenye ngazi zote za kisiasa.

Kama ilivyo kwa udiwani sehemu kubwa nchini, pia kwa mkoa wa Mara Vyama vya Upinzani vilipata changamoto za wagombea wao kuenguliwa kutokana na matatizo ya kisheria au kutokidhi vigezo

Updates
January
February
March
April
May
June
July
August
September
October

Kamati Kuu CCM yatangaza rasmi majina ya watia nia Ubunge 2025​

  • MKOA WA MARA

    (i) JIMBO LA BUNDA


    1. Boniphace Mwita Getere
    2. Lazaro William KANDORE
    3. Daud Rukiko MAYEJI
    4. Aloyce Msafiri MUSIKA
    5. Sulusi John NYIKERA
    6. Moses Wambura RYAKITIMBO

    (ii) JIMBO LA BUNDA MJINI

    1. Kambarage Masato WASIRA
    2. Ester Amos BULAYA
    3. Robert Chacha MABOTO
    4. Joseph Daud BULUBA
    5. Exavery Mfungo RUGINA

    (iii) JIMBO LA MWIBARA

    1. Charles Mugata KAJEGE
    2. Kangi Alphonce LUGOLA
    3. Wilson Maregesi MUKAMA
    4. Mbuke Makanyaga MAJULA
    5. Idd Mabala YAZID
    6. Emmanuel Makalle BUSANYA

    (iv) JIMBO LA BUTIAMA

    1. Jumanne Abdallah SAGINI
    2. Baraka Tyery MANYI
    3. Dr. Wilson Mahera CHARLES
    4. Manyerere Jackton NYERERE
    5. Frank Magesa MAHEMBA

    (v) Jimbo la Musoma Mjini

    1. Mgore Miraji KIGERA
    2. Dr. Eliud ESSEKO (Mkorea)
    3. Juma Mokili JUMA
    4. John Kyabwene BWANA
    5. Philbert Korogo SASITA
    6. Mashaka Nelson BISWALO


    (vi) Jimbo la Musoma Vijijini

    1. Prof. Sospeter Mwijarubi MUHONGO
    2. Kenedy Gerson CHIGURU
    3. Daud Zakayo MAJINGE
    4. Aspernas Magina MTARANGA
    5. Evarist Pascal MAGANGA
    6. Dr. Mbeba BENJAMINI
    7. Bernard Ibrahimu MERUMBA

    (vii) Jimbo la Rorya

    1. Jafari Wambura CHEGE
    2. Sango Issaya Gungu KASERA
    3. Nyihita Wilfred NYIHITA
    4. Peter Leonard SARUNGI
    5. Nchama Clifford WAMBURA

    (viii) Jimbo la Serengeti

    1. Dr. Amsabi Jerermiah MRIMI
    2. Mery Daniel JOSEPH
    3. Michael Peter MAHENDE
    4. Paulo Kingímbe CHACHA
    5. Deogratias Bernard CHACHA
    6. Dr. Stephen Kebwe KEBWE

    (ix) Jimbo la Tarime Vijijini

    1. Mwita Mwikwabe Mwikwabe WAITARA
    2. Nyambari Chacha NYANGWINE
    3. Simon Kemor CHACHA
    4. Deodatus WAIKAMA
    5. Edward Mgelea MACHAGE

    (x) Tarime Mjini

    1. Jackson Ryoba KANGOYE
    2. Michael Mwita KEMBAKI
    3. Esther Nicholas MATIKO
    4. Said Kisyer CHAMBIRI
    5. Robert Mkirya CHACHA
    6. Mussa Ryoba DEUS
    7. Machare Heche SUGUTA
ZINGATIA: Mikoa yote ina mada yake ya 'Update' ili kuweka wepesi katika ufuatiliaji.
 
Back
Top Bottom