Mapya Yaibuka Sakata La Escrow

Mapya Yaibuka Sakata La Escrow

chakii

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2013
Posts
21,704
Reaction score
28,969
Kashfa ya Escrow imeibuliwa upya bungeni baada ya wabunge kudai kuna kampuni ya Simba Trust inayomiliki asilimia 50 za kampuni ya Pan Africa Power (PAP), ambayo inadaiwa kuhusika katika ufisadi wa uchotwaji wa zaidi ya Sh.bilioni 300 katika akaunti ya Tegeta Escrow.

Hayo yaliibuliwa jana bungeni na Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni wakati wa kuwasilisha hotuba yake ya kambi hiyo kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya mwaka 2015/2016 ya Wizara ya Viwanda na Biashara.

Msemaji wa kambi hiyo, Mbunge wa Ole (CUF), Rajab Mbarouk Mohamed, alisema wakati umma wa Watanzania unataka kuelewa wamiliki wa kampuni ya Simba Trust lakini katika hali ya kushangaza Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela), umegoma kutoa majina ya wamiliki wa kampuni hiyo.

Kambi rasmi ya upinzani tunaitaka serikaliieleze kwanini taasisi hii ya Brela iliyo chini ya wizara hii bado inakataa kutoa majina ya wamiliki wa Simba Trust, imekuwa kamailivyokuwa makampuni yaliyohusika na uchotaji mabilioni ya Epa na fedha za mradi wa Meremeta,¡± alisema.

Mnyaa alisema hatua ya Brela kukataa kutoa majina ya wamiliki wa kampuni hiyo kuna unganisha na dhana kwamba wamiliki wa kampuni hiyo ni viongozi wandamizi wa serikali ya CCM.

Alisema matatizo ya kiutawala yaliyopo katika sekta ya umma nchini yamesababisha sekta ya viwanda kushindwa kujiendesha kiushindani.

Aliongeza kuwa Shirika la Umoja wa Mataifa la na Elimu, Sayansi na Utamaduni (Unesco), limebainisha kuwa viwanda vingi vinaendeshwa kwa hasara kutokana na kuwapo kwa gharama kubwa za uzalishaji, tija ndogo, riba kubwa za kibenki,tatizo la umeme na urasimu.

Mnyaa alisema licha ya kwamba Shirika la Viwango Tanzania (TBS), lipo lakini takwimuzinaonyesha kuwa Tanzania inaongoza kwakuwa na bidhaa feki kwa ukanda mzima wakusini na mashariki mwa Bara la Afrika.

Tukio la hivi karibuni kampuni ya UNI-METAL EAST AFRICA Co iliingiza bandarini mabati feki 100,000 na TBS ikakamata mabati feki 15,000 tu na 75,000 yaliyobaki yalikuwa tayari yameingia kwenye mzunguko na Watanzania walikuwa wameshanunua mabati hayo,¡± alisema.

Awali Dk. Kigoda alisema serikali imeandaautaratibu ambao utawezesha kuwapatia wafanyabishara wadogo maarufu wamachinga leseni maalum ili watambuliwe na kuondokana na adha ya kunyanyaswa katika maeneo wanayofanyiabiashara zao.

Dk. Kigoda alisema moja ya mikakati ya wizara katika kipindi cha 2015/2016 ni pamoja na kufufua viwanda vilivyobinafsishwa ambavyo havifanyi kazi kikamilifu kikiwamo kiwanda cha matairi cha General Tyre cha jijini Arusha na kiwanda cha nguo Urafiki.

CHANZO:
NIPASHE
 
Subirini baada ya uchaguzi...yatafahamika tu.
Lowasa mwenyewe kaja kuilezea richmond baada ya miaka saba
 
Sasa hawa wanataka naniihii apange safari nyingine ya kwenda kupima akili ....kweh kweh kweh...
 
Subirini baada ya uchaguzi...yatafahamika tu.
Lowasa mwenyewe kaja kuilezea richmond baada ya miaka saba

Yule nae saundi tu. Kina mwakyembe walienda mpaka huko USA kunakodhaniwa kua ofisi ya Richmond na hawakukuta cha ofisi wala nini.

"Kingmaker" ana hesabu kali sana, maana ngoma ilivyohama mpaka kuja kufikia kwa Dowans ya Kina Hillary Chlinton na Obama ni Mungu tu ndio anajua.
 
Wapinzani wameshaishiwa sera. Mbona hata kwenye mikutano yao hawaelezi namna watakavyoedeleza pale wenzao walipofikia? Hawasemi wanatarajia kujenga barabara ngapi, Mashule mangapi, Hospital ngapi, wataborashaje maisha ya mtu wa chini kama mkulima, nini kipaumbele chao wakipata madaraka, watanuifashaje mtanzania kutokana na rasilimali za nchi, je mikakati yao ya maendeleo ikoje kodi wanazolalamikia kuwa hazikusanywi watatumia mbinu gani mbadala kuzikusanya (maana wanapinga mfumo wa EFD na kusapoti wafanyabiashara kugomea kulipa kodi) je nchi wataiendesha kwa mgawanyo upi wa mapato na matumizi, yale wanayowakataza wananchi wasichangie (eg maabara) watapataje kuendeleza mashule n.k, Haya hawayaelezi! Kila kukicha ni Escrow! Well, hili tumeshalisikia, so what is the way forwad? Mi ninaona hawana sera zaidi ya kulala na kuamka wakitafuta kashfa bila plan ya kumuendeleza mtanzania, kifupi upinzani umefeli, wanatumia matatizo madogomadogo ya watanzania kama mtaji wa kuingia ikulu bila plan za maendeleo.
 
Upinzani wa tanzania bana hakuna hoja za maana za kuwasaidia watanzania badala yake kudandia vitu vilivyokosa hata uthibitisho wa hoja.
 
Kujenga barabara ni sera au matokeo ya sera, nilifikiri ujenzi na mengineyo ni ahadi
 
Kwani bungeni ni mahali pa kuomba kuchaguliwa kuongoza nchi?
 
Yule nae saundi tu. Kina mwakyembe walienda mpaka huko USA kunakodhaniwa kua ofisi ya Richmond na hawakukuta cha ofisi wala nini.

"Kingmaker" ana hesabu kali sana, maana ngoma ilivyohama mpaka kuja kufikia kwa Dowans ya Kina Hillary Chlinton na Obama ni Mungu tu ndio anajua.

Watu wanazungumzia hela taslimu ya ESCROW iliyoibiwa toka benki kuu wewe unazungumzia Richmond ambayo mitambo yake haikununuliwa kwa hela ya serikali. Mtambo wa Richmond ulinunuliwa kwa pesa za wawekezaji.Wao ndio walioata hasara.
 
Upinzani wa tanzania bana hakuna hoja za maana za kuwasaidia watanzania badala yake kudandia vitu vilivyokosa hata uthibitisho wa hoja.

.......Daah, Wee zuzu nini!!.

Hivi masuala ya EPA, Richmond, Operesheni Tokomeza, Escrow na upuuzi mwingine wa CCM si mlisema hivyo hivyo kuwa Wapinzani hawana hoja na baadae mkaishia kufukuza Mawaziri kutoka katika nafasi zao au mlitumia uthibitisho na hoja zipi kutimuana katika nafasi za uongozi?
 
Atakuwa zuzu huyo...
 
Back
Top Bottom