Mapya yaibuka mbio za urais 2015

Mapya yaibuka mbio za urais 2015

Geeky

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2013
Posts
307
Reaction score
181
Siku nne baada ya Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye kueleza kuwa amekata rufaa Kamati Kuu (CCM) kupinga adhabu ya onyo aliyopewa kwa kuanza mapema kampeni za urais, wenzake watano waliokumbwa pia na adhabu hiyo wamesita kufanya hivyo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, baadhi yao walidai hawajapewa barua za onyo kwa kudaiwa kufanya kampeni za urais wa 2015 kabla ya muda wake.

Sumaye na wanachama wenzake, Edward Lowassa, Bernard Membe, Stephen Wassira, William Ngeleja na January Makamba walitiwa hatiani kwa kuanza kampeni mapema, hivyo kupewa onyo linalokwenda sambamba na kutowania nafasi yoyote ndani ya chama kwa miezi 12.

Hata hivyo, juzi Sumaye alipotakiwa na gazeti hili kueleza alikata rufaa hiyo kwa kutumia kanuni ipi, alisema mpaka sasa hajapata mrejesho wowote kwa sababu kanuni hazielezi ni muda gani anatakiwa kuwa amepewa taarifa kuhusu rufaa hiyo.

Kauli hiyo ya Sumaye ilipingwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye ambaye alisema mwanachama yeyote lazima akate rufaa kwa kutumia kifungu cha kanuni husika, ili ajue rufaa yake itasikilizwa ngazi ipi ya uongozi.

Makamba ambaye ni Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia alisema atatoa msimamo wake kama atakata rufaa ama la, baada ya kupokea barua inayoonyesha tuhuma zinazomkabili ndani ya CCM.

Kamati Ndogo ya Nidhamu inayoongozwa na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Philip Mangula ndiyo iliyowatia hatiani vigogo hao ambao wote kwa pamoja wamekuwa wakidaiwa kuutaka urais.

Akizungumza na gazeti hili katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma jana, Makamba alisema hadi sasa hajapokea barua kutoka ndani ya chama inayoonyesha anachotuhumiwa.

"Sijui yeye (Sumaye) amepata barua ya kumwonyesha anachotuhumiwa, mimi sijapewa barua kwa hiyo siwezi kusema kuhusiana na uamuzi nitakaochukua," alisema Makamba na kuongeza;

"Hayo ni maneno tu ya magazeti, kimsingi sina ninachotuhumiwa, magazeti yaliandika Makamba amwaga pikipiki kwa waendesha bodaboda Mwanza, kimsingi nilichofanya pale ni kuwaunganisha waendesha bodaboda na kampuni inayouza pikipiki hizo, mimi sikulipa fedha zangu."

Wassira alipoulizwa iwapo atakata rufaa kuhusu uamuzi huo alisema; "Nimekubali yaishe."

Kwa upande wake, Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa kupitia msaidizi wake, alisema hana maoni kuhusiana na uamuzi huo.

Naye Mbunge wa Sengerema na aliyewahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, alikataa kuzungumzia jambo hilo kwa madai kuwa yeye siyo msemaji wa chama.

"Mimi siyo msemaji wa chama. Kama unavyofahamu chama chetu kina wasemaji wake ambao ndiyo wanaotakiwa kuzungumzia mambo hayo," alisema Ngeleja.

Februari 20 mwaka huu, Membe aliipongeza CCM kwa kuwapa adhabu wasaka urais akiwamo yeye mwenyewe na kusisitiza kuwa kila chama lazima kifuate utaratibu wa kupata viongozi wake.

source : mwananchi
 
Duh!! Kumbe mapovu yote ya kina NAPE hawajatoa barua zozote kwa hao watuhumiwa naona walikuwa wanaudanganya Umma na inawezekana hata yaliyojadiliwa huko sio yaliyosemwa kwenye vyombo vya habari.
 
CCM haina ujasiri wa kumwandikia mtu kama Lowassa barua , ni waongo mpaka mbele ya umma kwamba wameandikishwa barua kumbe hakuna kitu kama hicho.....
 
Mara nyingi NAPE amekuwa kama kibuyu kilichovunjika ambacho mtoto hupuliza kuwaita Komba bila mafanikio.
 
Hivi mchakato wa kugombea uraisi thithiemu huanza mwezi wa ngapi vile? Kutegemeana na hesabu, kama wameamua kuwabana kweli, afu waseme adhabu itaanza kuanzia barua ziliposainiwa, wanaweza kuula wa chuya.

Imagine mchakato uwe unaanza machi 2015, afu hawa barua wapewe May 2014. Ukijumlisha 12 months, adhabu itaisha April 2015. Wanakuwa wameenguliwa kisailensa.

Hawajagundua tu, bora wadai barua zao mapema, wanaweza poteza nafasi zao za kugombea, wee waache washunule tu.
 
Hiyo ilikua political posturing tu,sema huyu sumayi ni kichwangumu kuelewa,sasa anataka kukuza mjadala.
 
Ngeleja acha woga yaani hata issue zako unataka chama ndio kikusemee? au umekariri kila kitu sio msemaji? hahahahaha
Hata mim kanishangaza sana, yani uthuma binafsi asemewe na chama..huyu jamaa ni mtambo, sasa kama hawezi hata kujieleza huo urais atauweza!
 
EL ndo jembe hapa, mtafurukuta weee lkn kugombea rais lazima yumo tu tena kwa kijani hiyo2.........
 
Wassira tulia hivyohivyo maana wewe ndio chaguo la wengi. Huna doa.
 
Filamu zisizo na ukomo zinaendelea ndani ya CCM.
 
barua zimetumwa kwa post, kwa hiyo bado hazijafika, au hamjui shirika letu la posta lilivyo-ovyo? barua kwenda bunda/ruvuma/bumbuli/monduli/kateshi/sengerema haiwezi kufika ndani ya mwezi mmoja.
 
Back
Top Bottom