Mapya yaibuka kufungiwa kwa Dk. Mwaka; Yadaiwa kumesukumwa na maslahi binafsi

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,242
34,903
HATUA ya kituo cha tiba asili cha tabibu Dk. Juma Mwaka ‘Foreplan’ pamoja na vituo vingine viwili, kumesukumwa na maslahi binafsi, anaandika Regina Mkonde.

Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala nchini limelalamikiwa kuchukuwa hatua hiyo kutokana na kuwepo kwa msukumo wa binafsi ya baadhi ya watumishi wa baraza hilo na kwamba, sababu zilizotolewa ni za ‘kipuuzi’.

Pia imeleezwa kwamba, hatua hiyo ni juhudi za kurudisha nyuma ama kukwamisha kwa makusudi juhudi za waganga wa Tiba Asili.

Hayo yamesemwa leo na Mohamed Matokeo, Mwenyekiti wa Baraza la Waganga wa Tiba, Ushauri na Utafiti wa Dawa Asili Tanzania (Bawata) wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.

“Bawata tukiwa chombo huru cha waganga wa tiba asili, tunasikitika sana utendaji kazi unaofanywa na Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala ambacho ni chombo cha kiserikali kilichopewa mamlaka ya kusimamia taaluma hii na kuiendeleza,” amesema na kuongeza;

“Lakini baraza hilo limekuwa ni chombo kinachorudisha nyuma fani ya tiba asili hapa nchini, kwani limekuwa likikwamisha kwa makusudi juhudi za waganga wa tiba asili walioonesha ufanisi katika kutoa huduma ya tiba asili.

Imekuwa kawaida kwa baraza hilo kuitisha au kuwafungia waganga wa tiba asili na vituo vyao kwa sababu zinazoonekana ni za kibinafsi.”

Matokeo ametoa mfano wa tukio lililotokea jana la kufungwa kwa baadhi ya vituo vya tiba asili ambapo amesema kuwa, wahusika walifungiwa pasipo kupewa nafasi ya kujitetea na au kuhojiwa.

“Sisi bawata tunapinga hatua hii ya kiuonevu kwani wametoa maamuzi ya kuwafungia bila ya kuwahoji wahusika, tena hawa ni waganga halali kisheria wamesajiliwa na wanalipa kodi vizuri,” amesema.

Sharifu Karama, Katibu Mkuu Taifa wa Bawata amedai kuwa, kuna baadhi ya watumishi wa afya wanaojishughulisha na uuzaji wa dawa za tiba asili kwamba ndiyo wanaochochea kukandamizwa kwa masilahi ya waganga wa tiba asili nchini.

“Kuna baadhi ya watumishi wa afya wanauza dawa za tiba asili katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, ambapo kwenye jengo la serikali.

“Kutokana na hali hiyo, Bawata tunaamini kwamba, baraza la tiba asili na tiba mbadala linaongozwa na waganga wa kisasa na kwamba tuna taarifa kuwa, kuna baadhi ya viongozi wa baraza hilo nao wanauza dawa asili kwa hiyo wanalitumia baraza kutimiza hadhma yao,” amesema.

Hata hivyo, Foreplan ilianza kuwindwa na Hamis Kigwangala, Naibu Waziri wa Afya baada ya kufanya ziara ya kushtukiza tarehe 15 Desemba mwaka jana na kuibua maswali mengi.

Ziara hiyo ilihitimishwa kwa kutolewa siku saba za uchunguzi na kwamba, kinachofanyika sasa kinatajwa kuwa ni matokeo ya ‘dhamira’ iliyooneshwa baada ya ziara hiyo.
 
Ndiyo yale yale...

Tunasikia, tunasikia, tunasikia...

Kwa hiyo ukisikia ndiyo ukweli?

Kwa nini wasitafute kwanza majina ya hao baadhi ya watumishi wa afya au viongozi wa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala wanaojishughulisha na uuzaji wa dawa za tiba asili kwenye hospitali za serikali?

Utetezi wa aina hii hauwezi kusimama katika kipimo cha ukweli.

Hata mahakamani huwezi kusimama na kusema ninasikia, ninasikia huyu ni mwizi halafu mahakama ikakubaliana kwa kutumia kigezo hicho.
 
HATUA ya kituo cha tiba asili cha tabibu Dk. Juma Mwaka ‘Foreplan’ pamoja na vituo vingine viwili, kumesukumwa na maslahi binafsi, anaandika Regina Mkonde.

Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala nchini limelalamikiwa kuchukuwa hatua hiyo kutokana na kuwepo kwa msukumo wa binafsi ya baadhi ya watumishi wa baraza hilo na kwamba, sababu zilizotolewa ni za ‘kipuuzi’.

Pia imeleezwa kwamba, hatua hiyo ni juhudi za kurudisha nyuma ama kukwamisha kwa makusudi juhudi za waganga wa Tiba Asili.

Hayo yamesemwa leo na Mohamed Matokeo, Mwenyekiti wa Baraza la Waganga wa Tiba, Ushauri na Utafiti wa Dawa Asili Tanzania (Bawata) wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.

“Bawata tukiwa chombo huru cha waganga wa tiba asili, tunasikitika sana utendaji kazi unaofanywa na Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala ambacho ni chombo cha kiserikali kilichopewa mamlaka ya kusimamia taaluma hii na kuiendeleza,” amesema na kuongeza;

“Lakini baraza hilo limekuwa ni chombo kinachorudisha nyuma fani ya tiba asili hapa nchini, kwani limekuwa likikwamisha kwa makusudi juhudi za waganga wa tiba asili walioonesha ufanisi katika kutoa huduma ya tiba asili.

Imekuwa kawaida kwa baraza hilo kuitisha au kuwafungia waganga wa tiba asili na vituo vyao kwa sababu zinazoonekana ni za kibinafsi.”

Matokeo ametoa mfano wa tukio lililotokea jana la kufungwa kwa baadhi ya vituo vya tiba asili ambapo amesema kuwa, wahusika walifungiwa pasipo kupewa nafasi ya kujitetea na au kuhojiwa.

“Sisi bawata tunapinga hatua hii ya kiuonevu kwani wametoa maamuzi ya kuwafungia bila ya kuwahoji wahusika, tena hawa ni waganga halali kisheria wamesajiliwa na wanalipa kodi vizuri,” amesema.

Sharifu Karama, Katibu Mkuu Taifa wa Bawata amedai kuwa, kuna baadhi ya watumishi wa afya wanaojishughulisha na uuzaji wa dawa za tiba asili kwamba ndiyo wanaochochea kukandamizwa kwa masilahi ya waganga wa tiba asili nchini.

“Kuna baadhi ya watumishi wa afya wanauza dawa za tiba asili katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, ambapo kwenye jengo la serikali.

“Kutokana na hali hiyo, Bawata tunaamini kwamba, baraza la tiba asili na tiba mbadala linaongozwa na waganga wa kisasa na kwamba tuna taarifa kuwa, kuna baadhi ya viongozi wa baraza hilo nao wanauza dawa asili kwa hiyo wanalitumia baraza kutimiza hadhma yao,” amesema.

Hata hivyo, Foreplan ilianza kuwindwa na Hamis Kigwangala, Naibu Waziri wa Afya baada ya kufanya ziara ya kushtukiza tarehe 15 Desemba mwaka jana na kuibua maswali mengi.

Ziara hiyo ilihitimishwa kwa kutolewa siku saba za uchunguzi na kwamba, kinachofanyika sasa kinatajwa kuwa ni matokeo ya ‘dhamira’ iliyooneshwa baada ya ziara hiyo.

Hapana wacha wafungiwe wanadanganya watu, ni WEZI NA MATAPELI in short
 
Matapeli wakubwa hao.

BTW... hivi huyo Mwaka ni 'Dkt' by profession? If NO, ni yeye mwenyewe hujiita hivyo? au ni wananchi ndo humuita 'dkt' baada ya kukubali 'tiba' zake zimetukuka?

-Kaveli-
 
Kweli kigwa alikuwa ana bifu naye
Eti kisa anajiita dokta kama yeye aliyesoma miaka minne ya udokta na ndio maana wanasema anatumia usasa badala ya asili au walitaka asivae makoti kama wa Muhimbili
Mtu anayechagiza maendeleo kam a mwaka serikali ya visasi ni mwendokasi hatari
 
Hata sio kisasi ila kama una masilahi binafsi napita na zangu wale waliopata kuhudumiwa hapo hawakutamani kurudi tena kutokana magumashi hasa huyo MWAKA hao sijui
Sio Kila kitu tukimbilie uonevu
Ni sawa kabisa anastahili kufungiwa
Tena asitakiwe
 
Hawa Waganga tena ni wezi na wanacheza na afya na uhai wa watanzania...
Kwanza wangetakiwa washikwe na kufunguliwa mashtaka... sbb ni wezi na wahuni sana... Dawa moja inatibu magonjwa 220 na ni milioni 3 dose yake yote...!! Huu ni uongo, wizi, uhuni na ni kucheza na uhani na afya za watanzania...!!

Kwanini ni
1: Wizi... sbb dawa unapewa utumie miezi 18, dose milioni 3 - 5.. na huponi..!! badala yake wameweka energizers kibao ktk dawa hizi, utahisi nguvu, kumbe hakuna tiba... ni wizi huu, just kama mtu kanywa redbull

2: Uongo - sbb hakuna dawa moja inatibu magonjwa zaidi ya 220.. uongo sana huu

3: Wahuni, sbb wanacheza na afya na uhai wa Watanzania, wakijua hawatibu chochote na kuchukua hela kubwa..!!

4: Matapeli: sbb wanajitangaza kama biashara ya Coca cola, au Safari lager, Serengeti.. etc.. ndio utapeli mkubwa huo..

5: Wangetakiwa wafilisiwe mali zao na kuwashtaki mara moja.. kwani sio madaktari, ila wanajifanya madaktari wakubwa sana, matangazo yao hadi kero, wanasema wanatibu eti KILA UGONJWA..!! Kuna wakati nikawa nasema Mh. Rais Magufuli hawaoni hawa matapeli..?

Finally, serikali imesikia kilio cha wananchi, ingawa imechelewa sana.. Hawa ni watu hatari sana, wanacheza na maisha ya watanzania.. watu hatari sana hawa.. matapeli wakubwa kabisa..
 
Hata sio kisasi ila kama una masilahi binafsi napita na zangu wale waliopata kuhudumiwa hapo hawakutamani kurudi tena kutokana magumashi hasa huyo MWAKA hao sijui
Sio Kila kitu tukimbilie uonevu
Ni sawa kabisa anastahili kufungiwa
Tena asitakiwe

Hahaha mbona umepost kwa hisia au na wewe ulienda kutafuta mtambo wa kutengeneza watoto kwa dkt. Mwaka akakupiga za uso.
 
Waliofanikiwa kwa matatizo yao watasema sio matapeli Waliofanikiwa watakwambia ni matapeli! Suala wafuate sheria na kuendesha kwa utaratibu na sheria! Mambo yao binafsi waweke kando!! Kama kuna maelekezo toka wizarani ni mbaya sana!! Mwendokasi style
 
Matapeli wakubwa hao.

BTW... hivi huyo Mwaka ni 'Dkt' by profession? If NO, ni yeye mwenyewe hujiita hivyo? au ni wananchi ndo humuita 'dkt' baada ya kukubali 'tiba' zake zimetukuka?

-Kaveli-
Sio Dkt ni Tabibu ila wananchi waliofanikiwa kwa tiba zake ndio wakampa hilo jina.
 
Wengi wao ni matepeli wakubwa sana....dawa zao nyingi hazitibu ugonjwa bali zinaondoa dalili za ugonjwa hivyo mgonjwa atahisi nafuu kumbe tatizo bado lipo na kibaya kabisa kinachoniudhi kwao ni bei zao za ajabu kabisa....akijua unauwezo wa kulipa unaweza kulipishwa hadi milioni 3.
 
Kweli kigwa alikuwa ana bifu naye
Eti kisa anajiita dokta kama yeye aliyesoma miaka minne ya udokta na ndio maana wanasema anatumia usasa badala ya asili au walitaka asivae makoti kama wa Muhimbili
Mtu anayechagiza maendeleo kam a mwaka serikali ya visasi ni mwendokasi hatari
Daktari anasomea fani hiyo miaka 5+ na sio minne kama ulivyoandika. Daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake anaongeza tena miaka mitatu ili abobee kwenye fani hiyo.

Huwezi kuchagiza maendeleo kwenye vitu sensitive kama afya bila kuwa na weledi wa kutosha na ukaachwa tu. Mbaya zaidi, anatumia modern science katika tiba zake.
 
Back
Top Bottom