Mdakuzi mkuu
JF-Expert Member
- Dec 27, 2016
- 212
- 719
Habari wanaJF!
Waziri wa Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mh Anjellah Jasmine Mbelwa Kairuki, P.O.Box 34368 Dsm alisema kwamba, ili watumishi wa umma wapande vyeo na madaraja, ni lazima kwanza wapitie mafunzo maalumu ya kiuongozi katika Vyuo vya Utumishi wa Umma; Mbeya, Singida, Uhazili -Tabora, Tanga, Magogoni na Mtwara.
Ikumbukwe kwamba, madaraja na mishahara havijapanda kwa watumishi wa umma ili kujirithisha na zoezi la uhakiki wa watumishi hewa ambao mpaka sasa wanakadiriwa kuwa 19,000.
Maswali ya kujiuliza kuhusu hao watumishi wa umma ambao wanatakiwa kupitia hayo mafunzo maalum:
1. Gharama za kusoma mafunzo hayo ni shilingi ngapi na zinagharamikiwa na nani?
2. Muda wa mafunzo hayo ni miaka mingapi na majukumu ya kiofisi yatakuwa yakifanywa na nani pindi watu wapo masomoni?
3. Mitaala ya kufundishia imeandaliwa na nani, lini na kwa tafiti/research ipi?
4. Muhula wa masomo kwa awamu ya kwanza unaanza lini na utaanza kwa kuchukua watu wangapi, wa ngazi ipi na wa taasisi zipi za serikali?
5. Mtumishi atakayefeli mafunzo hayo atarudia mafunzo au kudisco?Na hela ambazo atakuwa amezitumia je?
6. Watumishi wa umma wenye miaka 2,3,4 wastaafu, nao wanaenda kula shule?
Swala la uhamisho kwa watumishi wa umma bado tu? Mke wangu amehamishiwa Dodoma, mm nipo Mtwara Halmashauri, mateso matupu ndoa yangu inavunjika.
Asanteni kwa kunisikiliza