Mapya kuhusu watumishi wa umma kwenda kusoma kwa ajili ya kupanda madaraja na vyeo

kiujumla serikali ya awsmu ya tano imefeli vibaya sana katika kuboresha maslahi ya wafanya kazi. kilichobaki ni kupiga tu chenga na blahblah....hii ni hatari sana kwa kweli......

Point of correction, si kwamba serikali haitoi huduma hizo bali haina uwezo wa kifedha wa kutoa huduma hizo. Mnapenda sana political correctness kama wao wanavyofanya. Serikali hii ni maskini wahedi, wasikudanganye. Hawana uwezo wa kuboresha maslahi ya wafanyakazi. Hata kulipa mishahara ya sasa inawatoa josho (Unajua bajeti ya mishahara ya watumishi wa umma ni asilimia ngapi ya pato lote la mwezi la serikali?). Tuwage wakweli. Serikali haipandishi madaraja, hailipi malimbikizo, haiajiri, haipeleki watumishi mafunzoni na wala haiongezi mishahara kwa sababu HAINA FEDHA za kufanya hivyo. Msema kweli ni mpenzi wa Mungu.
 
mie sitilii maanani tamko la waziri ambaye ni si mwajiri wangu na ni mwanasiasa na si mtaalamu bali nasubiria waraka rasmi kutoka kwa Katibu Mkuu wa Utumishi au wizara yangu ambao ni wataalamu na waajiri wangu. haya matamko nishayazoea na sio njia ya kutoa maelekezo katika utumishi wa umma labda kwenye familia
 
Back
Top Bottom