Mapya CHADEMA, video zaidi zanaswa

Mapya CHADEMA, video zaidi zanaswa

utaifakwanza

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2013
Posts
14,193
Reaction score
2,815
Video zaidi zakabidhiwa polisi, Mwigulu Nchemba afunguka, asema kulikuwa na vijana sita waliandaliwa kumteka, mmoja akampelekea taarifa ...Amzungumzia Ludovick!

Tukio la kukamatwa na kufikishwa mahakamani mkurugenzi wa ulinzi wa CHADEMA Wilfred Lwakatare limezidi kuibua mambo mengine mapya yaliyofichika...

Habari za uhakika toka vyombo vya ulinzi na usalama zinaeleza kuwa mbali na video inayomuonyesha Lwakatare akipanga mipango ya kigaidi ya kudhuru watu mbalimbali wakiwemo waandishi wa habari, video nyingine zimekabidhiwa huku zikionyesha makada wa chama hicho wakiwa katika vikao vya siri.

Video hizo zinawaonyesha watu wengine ambao hawajafahamika wakiwa katika mikakati hiyo ambao wamerekodiwa bila wao kujijua...

Source: Mtanzania - Jumapili.
 
Chama cha magaidi wabaya sana kwenye hili taifa
 
Video zaidi zakabidhiwa polisi, mwigulu nchemba afunguka,asema kulikuwa na vijana sita waliandaliwa kumteka, mmoja akampelekea taarifa...amzungumzia ludovick......tukio la kukamatwa na kufikishwa mahakamani mkurugenzi wa ulinzi wa chadema wilfred lwakatare limezidi kuibua mambo mengine mapya yaliyofichika...habari za uhakika toka vyombo vya ulinzi na usalama zinaeleza kuwa mbali na video inayomuonyesha lwakatare akipanga mipangi ya kigaidi ya kudhuru watu mbalimbali wakiwemo waandishi wa habari, video nyingine zimekabidhiwa huku zikionyesha makada wa chama hicho wakiwa katika vikao vya siri..video hizo zinawaonyesha watu wengine ambao hawajafahamika wakiwa katika mikakati hiyo ambao wamerekodiwa bila wao kujijua... Source; mtanzania jumapili.

Hicho chanzo chenyewe kishakuwa bias na hivyo kimepoteza umaana wa kuitwa chombo huru cha habari,
kipumzike kwa amani
 
CHADEMA ni kama zimwi linalo afuta wa kumla kila siku wao ndio wauaji
 
Hahahahahahahahah
Mwigulu alitaka kutekwa na nani?
 
Last edited by a moderator:
tumechoka na mipango yenu ya kishamba.!
 
Kama hawajafahamika utasemaje sasa ni makada wa chadema ilihali unasema 'video zinaonyesha watu wengine ambao hawajafahamika' au wewe umewafahamu?
Mzee umekurupuka, soma vizuri taarifa yake ili uchague vizuri. Tunakutegemea sana kwa hoja
 
Hadi 2015 tutashuhudia mengi ya kushtua
 
mmh! Video azionekani vizuri, sasa wamejuaje kama ni wana wa CHADEMA kama? Daaa..! Ma movie ya kuchonga hayo na wanajichimbia kaburi
 
Mwigulu alipata habari za watu wanamipango ya kumteka, kwanini asingetoa taarifa Police? Huyu Mwigulu ndiye aliyepigiwa simu za vitisho na wabunge wa CHADEMA na alizibaini namba zao, mbona hao wabunge hawajashitakiwa? Mwigulu ni suspect # 1, kama Police watafanya kazi zao kitaalaam
 
Mzee umekurupuka, soma vizuri taarifa yake ili uchague vizuri. Tunakutegemea sana kwa hoja

Hapana sijakurupuka mkuu,hebu rudia tena kuisoma habari yake kama utamwelewa! Au mkuu labda sijaona vizur,anaposema video zinawaonyesha makada wa chama....halafu huko mbele anasema ambao hawajajulikana...sasa alijuaje ni makada wa chama ilihali 'hawajajulikana'?soma hapo anaposema na watu wengine sita...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom