Elections 2010 Mapungufu ya sera ya elimu bure


Mtu Mmoja,

..kwanza hakuna kitu kama "elimu bure" au "afya bure." huduma zote hizo kwa namna moja au nyingine zinagharimiwa na kodi wanazolipa wananchi, na vyanzo vingine vya mapato ya serikali.

..suala la "elimu bure" maana yake ni kuondoa michango na ada za shule ambazo zinatoka moja kwa moja mifukoni mwa wazazi.


..hoja kwamba wakati wa Mwalimu kulikuwa na wanafunzi wachache kuliko wakati huu haina uzito. pamoja na wanafunzi kuongezeka, walipa kodi nao wameongezeka, na serikali ya sasa hivi ina vyanzo vingi vya mapato kuliko wakati wa Mwalimu Nyerere. wakati wa utawala wa Mwalimu hatukuwa na migodi sita ya dhahabu kama ilivyo sasa hivi.

..kinachopaswa kufanyika ni kurudisha uzalendo na nidhamu ya matumizi serikalini. Mwalimu aliongoza nchi akiwa na baraza la mawaziri dogo kuliko hili la sasa hivi. tena mawaziri wake walikuwa na elimu ndogo kuliko hawa tulionao sasa hivi. kwa msingi huo hakuna sababu yoyote ile kwa serikali ya JK kushindwa ku-deliver kulingana na matarajio ya wa-Tanzania.


..Tanzania sasa hivi tumo katika 5 bora ya wazalishaji wa dhahabu. sielewi kwanini elimu yetu ni gharama[ya kulipia], na kiwango cha chini, kuliko jirani zetu wa Kenya na Uganda, ambao hawajabarikiwa kuwa na rasilimali kulinganisha na sisi.

..kama Kenya na Uganda wameweza , kwanini Tanzania tushindwe?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…