Maprofesa wachambua ubanaji matumizi

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
12592689_1025817157482742_6286188498729608904_n.jpg
 
Mzunguko wa pesa kuwa mdogo si tu unasababishwa na serikali kubana matumizi lakini pia kubana wala rushwa na wezi.Hebu chukulia mtu anakwapua Bandarini au TRA bilioni moja.Hizi pesa akizichukua mara nyingi haweki benki anaenda nazo mitaani kuzitumbua na mahawara na vimada na kunywesha watu baa nzima,kufanya shopping ya nguvu nk hela zinamwagika mitaani kama mtiririko wa mto rufiji.

Unakuta mzunguko wa hela mkubwa lakini hela za wezi na wala rushwa ndio zimesababisha mzunguko mkubwa.Ukiwabana.Unakuta baa ziko tupu,changudoa wanalia njaa wanalalamika mzunguko wa hela mdogo.

Magufuli hatua anazochukua za kuthibiti mzunguko wa hela kwa kubana matumizi ya serikali na kubana wezi na wala rushwa kutasaidia muda si mrefu kudhibniti mfumuko wa bei kwa bidhaa mbali mbali.Mfano bei za nyumba za kupanga zitashuka.Wezi na wala rushwa walikuwa wakipanga nyumba nzima kupangishia hawara zao kwa bei yoyote.Sasa hivi kwa kubanana huko kwa Magufuli jeuri ya wenye nyumba kuropoka bei yoyote ile ya kupangisha itaondoka sababu watu wana mapato ya halali.Bei za viwanja pia itashuka .Watu walikuwa wakitaja bei yoyote wakijua kuna wezi na wala rushwa wawezao nunua bei yoyote tunakoenda hata mtu wa kipato cha kawaida aweza pata kiwanja maeneo maarufu.

Hoteli pia zitashusha bei sababu mpangaji mkuu serikali hayupo itabidi wachague hoteli zao walale panya na mende au washushe bei wapate wateja watu wa kawaida.Bei za ada za shule zile zitozazo hela za kuua mtu watashusha vinginevyo watakosa wanafunziAda shule za private zile kubwa kubwa zitashuka muda si mrefu kwenye utawala wa Magufuli

Naunga mkono hatua za Magufuli sababu ni sahihi katika kudhibiti mfumuko wa bei kwa kudhibiti mzunguko mkubwa wa pesa mitaani.Na hii itakuwa ni kwa faida kwa watanzania walio wengi.Wachache wataumia lakini wengi watafaidi mfumuko wa bei ukishuka.

Magufuli kaza buti shikilia hapo hapo.
 
Back
Top Bottom