Maporomoka Uganda yahofiwa kuuwa watu 300 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maporomoka Uganda yahofiwa kuuwa watu 300

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Mar 4, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 4, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,770
  Likes Received: 4,911
  Trophy Points: 280

  [​IMG]
  Chama cha Msalaba Mwekundu nchini Ugabda kimesema watu zaidi ya mia tatu wanahofiwa kufariki dunia kufuatia maporomoko ya ardhi yaliyotokea ...
  mashariki mwa nchi hiyo.
  Maporomoka hayo yaliyotokana na mvua kubwa, yamesababisha uharibifu mkubwa katika eneo kubwa lenye milima la Bududa, huku vijiji vitatu vikiarifiwa kufukiwa na udongo.

  Shirika la Msalaba Mwekundu linaarifu kuwa makundi ya uokoaji yanatumia vifaa vya mkononi kuchimba tope kwa lengo la kuitoa miili ya watu.

  Hata hivyo waokoaji wamepata miili hamsini pekee, huku wakiendelea kuwatafuta manusura.
  Jeshi la taifa la Uganda nalo linatarajiwa kujiunga na juhudi za uokoaji.

  Waziri anayehusika na kukabiliana na majanga nchini Uganda, amesema mazishi ya watu waliofariki dunia yanatarajiwa kufanyika leo.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...