Mapolisi wa kituo cha mabatini kijitonyama wanakula ganja;mkuu wa polisi anawalinda;mwema unajua hil

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,149
Wana ndugu hii ni kashfa ya aibu na kweli
Kwa waliosikia jana kipindi kimoja toka clouds kuna kijana mmoja aitwae Rasta ambae amekuwa akiwauzia karibia wala ganja na unga wote pale kijitonyama;huyu kijana amepnagasha nyumba ya mmama mmoja pale kijitonyama..kutokana na tabia mbaya za huyu kijana mama akusita kutaka kumfukuza sasa mama alienda polisi kulalamika kijana anakuja na kundi la watu wanavuta ganja nyumban kwake

Gafa kijana akaitwa na mkuu wa polisi na kuonywa na kuachiwa matokeo yake akatangaza anaenda kuwacharanga mapanga watoto wa yule mama ;alipofika akakuta yule mama akamrushia panga bahat akakwepa likampata mikononiameshonwa nyuzi 15...alipoona amedondoka akakimbia..baada ya hapo mama akapelekwa hospital na huko ndipo waandishi walipopata uhuni na uchafu wa mabatini

Alipohojiwa mama alisema kwanza nashukuru kwa kuja kuniona jamani nani kawaambia..akaombwa aelezee kisa halisi wakati huo wananchi wa kijitonyama wanamtafuta huyo kijana aitwae marasta
Mama akasema kwa kweli nawaambia hawa mapolisi wanasema wako kwa ajili ya kulinda wananchi lakini ndio wanashiriki hawa kutumaliza..ndugu zanguni m nimempangisha kijana aitwae marasta sikuwa najua kama anauza unga na BANGI..akaanza kunletea watu wa ajabu ajabu......,nikaenda kituo cha polisi gafla nikakuta watu ambao wanakuja kwa hapo kijana wamevalia manguo ya polisi;

Nikaomba kuongea na mkuu wa kituo cha polisi;akaniweka kama masaa mawili..baadae nikamweleza kuna vijana na wasiwasi nao wanauza bangi kwangu naomben msaada wenu niwaondoe niwarudishie hela zao..mku wa kituo ch apolisi mabatiniakamuuliza nani wakina marasta??akajibu hao hao ....akamwambia nenda nyumban nitawaita niwashugulikie..kwa kweli imechukua mwezi wa sita ajafanya lolote na mbaya zaidi kijana huyo kumbe ikifika usiku anawapelekea POLISI WA MABATINI Ganja.aka Bangi

Ndipo waandishi wakaogopa na kwenda kuuliza kwa MKUU WA UPELLELEZ ambae akutoa ushirkiani..wakaelekea amjini na kukutana na Mkuu mmoja wa polisi nimesahau jina lake akadai amesikia hiyo taarifa na huyo rasta wanamtafuta akakiri amesikia kuna mapolisi wanaishi kula ganja usiku lakini sijui kama ni kweli naomba mnipe muda...kumbuka MKUU WA POLISI MABATINI NAE AKAOMBA MUDA MIEZI SITA LEO HUYUHUYU MAMA ANAKATWA MAPANGA NA YULE ALIEMUOGOPA

JESHI LA POLISI MNALINDA WAHALIFU NI SAWA...NA KAMA MMEANZA KULINDA KWA KUVUTA BANGI JAMANI HIZO BASTOLA SI IPO SIKU MTATUFYATULIA...HILI TATIZO LIKO VITUO VYA KAWE ,MBEZI MWISHO,NA WAKUU WA POLISI WAMEKUWA WAKIFIKIA KUWATISHIA WANAOLETA KESI ZAO..HAYA MAMBO LAZIMA YAMALIZWE VINGINEVYO SERIKALI MTAISHIA KUZIKA MAREHEMU WASIO NA HATIA

MKUU AFANDE MWMA TUNAOMBA UCHUNGUZI JUU YA HILI IKIWEZEKANA MTU AWAJIBISHWE NA SIO UPUUZI WA KUHAMISHWA UWEZI AMISHA MUUWAJI UNATARAJI NINI???MLITUAMBIA MNACHUNGUZA WALIOIBA EPA NA WEWE UKASHIIRIKI KWENYE KAMATI MPAKA LEO AKUNA MAJIBU SIJUI NA HUU ITAKUWAJE???HOPE UHAI N MUHIMU KULIKO TUME YA EPA
 
Hahaaa...ukitaka uvunjike mibavu itokee tenda ya kwenda kuchoma bangi..........inagombaniwa kuliko ya kwenda kukamata wahalifu

Ila Polisi wetu bwana, yaani sensitive case kama hii ya mtu kutimiza wajibu wake wa "Polisi Jamii" mnaichukulia kirahisi namna hii na kumrudisha jamaa kilaini? Je angemuua huyo mama mngefanyaje?,......Mnajidai kuwa active kuzima sauti za wanyonge wanapodai haki kwa kutumiwa na wanasiasa halafu wajibu wenu wa msingi mnauweka rehani....

 
Kawaida polisi wa bongo wanawajua waalifu wote na ndiyo maana wanakwambia toa chochote mali yako itapatikana!!!Kinachotakiwa ni kutengeneza mfumo mpya wa polisi ili lijinasue na kashifa hizi!!
 
Nikaomba kuongea na mkuu wa kituo cha polisi;akaniweka kama masaa mawili..baadae nikamweleza kuna vijana na wasiwasi nao wanauza bangi kwangu naomben msaada wenu niwaondoe niwarudishie hela zao..mku wa kituo ch apolisi mabatiniakamuuliza nani wakina marasta??akajibu hao hao

Ndugu zanguni hilo jibu la mkuu wa kituo limentisha na kunikumbusha mbali sana sana...mwaka juzi tulikuwa na gari mbili na washikaji tunatoka kula nyama gafla mwenzetu wa mbele alikuwa na watu 3 wakatihiwa na bastola pale morocco wakatolewa na kuachia gari baada ya dk kadhaa wakatupigia gari imeibiwa atukua mbali sana tukakimbilia pale morrocco..tukawaeleza yaani alie kuwa zamu aliwauliza jamaa wakoje mwenzake wa pemben akajibu hao watakuwa wakina marasta na masawe wa kinondoni nimeona gari zao zinazunguka sana upande wetu toka saa kuminambili...nilishtuka sana tukamweleza mkuu wa polisi akatupa jamaa wa defender..tukiwa ndan jamaa wakawa wawazi jamani kuhangaika kutafuta gari ni garama mna laki tano tuhangaike tukawamabia tuna tatu ..tulizunguka nao mara wakaanza kuwaita wenzao kwenye redio kuwaeleza huku gari yetu iko pale OSTERBAY POLISI...TULIENDA MASAKI TUKAZUNGUKA TUKATOKEA NAMANGA TUKAINGIA MITAA YA PLAZA TUKIWA TUNAKATA NJIA YA ROSE GARDEN JAMAA MMOJA AKAWAITA AKWAULIZA RANGI NA NAMBA ZILE ZILE ZA GARI YETU AKASEMA WAKO WAMEIPAKI HAPA KIJITONYAMA ILA MSIJE KWA KASI TUANGALIE KAMA WATAINGIA NDAN ,,NADHAN WALISHAWAONA MPKA SABA TUKAIFWATA GARI AWAKUWA WAMECHUKUA CHOCHOTE..TUKARUDI POLISI WAKATAK KUANDIKISHA TUKAWAMBIIA AHASANTEN NA KUWAPA TATU YAO MOTO TUKAONDOKA NA GARI

NINI MAANA YAKE HAW WAALIFU SI WAPYA HAPA MJINI SIJUI MIKOA MIINGINE LAKINI WANAJULIKANA MPAKA NA AFANDE KOVA MWEMA NA WENGINE WOTE,,TATIZO NI WANAPOWAKAMATA WAANASHINDWA KUWAWAJINBISHA KWA NINI SIJUI ..TUMUULIZE MKUU WA POLISI KANDA YA DAR ES SALLAAM

WITO
WANANCHI PAMOJA NA POLISI KUSHIRIKIANA NA WAAHALIFU NAOMBA TUSIKAE KIMYA TUKISHINDWA MTUMIE HATA MSG MWENZIO MWENYE UWEZO WA KUFIKISHA UPUMBAVU WA POLISI..JAMAN NI WANAUMIZA MOYO SANA..HASA KAWE SIJUI ANALINDWA NA UGANGA GANI..YAANI ANADIRIKI KUKUINGIZA NDAN ANAKUPA WAZI LETA KIASI KADHAA HAPA HAMNA KESI..ALAFU WAMUACHIA KESHO YAKE UKIMKAMATA WANAKUULIZA WEWE SI TUMEMUACHIA WE UNATAKA KESI GAN TENA.....WAMESHIBA NA RUSHWA NA WAKUU WA POLISI AWAWATEMBELEI HATA SIKU MOJA..M NASHANGAA SANA
 
Hahaaa...ukitaka uvunjike mibavu itokee tenda ya kwenda kuchoma bangi..........inagombaniwa kuliko ya kwenda kukamata wahalifu

Ila Polisi wetu bwana, yaani sensitive case kama hii ya mtu kutimiza wajibu wake wa "Polisi Jamii" mnaichukulia kirahisi namna hii na kumrudisha jamaa kilaini? Je angemuua huyo mama mngefanyaje?,......Mnajidai kuwa active kuzima sauti za wanyonge wanapodai haki kwa kutumiwa na wanasiasa halafu wajibu wenu wa msingi mnauweka rehani....


Si unakumbuka walimkimbiza mama mmoja na gari Mwanza ;alikuwa na viroba 30...vya ganja tena ya morogoro mwana asikwambie mtu inanukia mpaka basi wanavyodai..akawarushia viboraba wasianze kupigana adharan mmoja akaona noma akavua na nguo akarudi na za nyumban watu wakawaita mapolisi wenzao mpaka leo akuna kesi na kwenye faili vile viroba vilipotea...Upuuzi mtupu hawa watu

Wacha hilo kuna Vile vidonge vya madawa ya kulevya vilikamatwa kule tunduma mnakumbuka jamaa wakachukua wakadai wanaleta dar vilikuwa 80 vikafika 50,..na ktk 50 kukakutwa 20 vimwekwa unga wa ngano na mahindi yaani mixer unaweza jua kwa nini mkuu wa polisi kitengo cha madawa ya kulevya ni Tajiri kuliko....
 
uzur rasta kakamatwa leo na ypo kituoni na sio kituo cha mabatin kaz anayo anajifanya chiz kumbe mzm
 
PDIDY NAKUPONGEZA KWA KUWA MUWAZI KATIKA KUFICHUA UHALIFU KATIKA JAMII...... TUWE WAZI HIVI HIVI KUFICHUA MAOVU KEDEKEDE YANAYOITAAFUNA JAMII YETU....!
TUANDIKE HUMU BILA KUFICHA NA BILA MUMPAKAZIA MTU (and we will have our rewards)
 
Siku hizi police ni kazi ambayo vijana huenda baada ya kuona ni wavivu na hawawezi kupambana na maisha. Mwishowe ndo huu wa rushwa na kushobokea hata mia tano. Huwa wanatembea usiku na saloon nyeupe hivi pale sinza wakijifanya wanatafuta wazururaji kumbe wanaangalia mtu katoka kustarehe anakwenda kwake wanamkamata ili awaachie hata buku tano. Wanajua vijana wa sinza wengi middle class, mambo safi, wakati wao choka mbayaaa, Wivu tu unawasumbua.
 
Back
Top Bottom