Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,500
Wagombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha ACT Wazalendo, wamewasili mjini Unguja kwa ajili ya utambulisho kwa wanachama na wananchi wa kisiwa hicho.
Luhaga Mpina mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania na Othman Masoud anayewania urais Zanzibar wamewasili leo Jumamosi Agosti 9, 2025 wakitokea jijini Dar es Salaam, baada ya kumalizika kwa mkutano mkuu maalumu uliowapitisha kuwania nafasi hizo.
Wajumbe wa mkutano mkuu wa ACT Wazalendo, uliofanyika Agosti 6, 2025 jijini Dar es Salaam, walimpitisha Mpina kwa kura 559 sawa na asilimia 92.3 dhidi ya mshindani wake Aaron Kalikawe aliyepata kura 46 sawa na asilimia 7.7
Wakati Othman aliyekuwa mtiania pekee alipigiwa kura za ndio 606 sawa asilimia 99.5 ya kura zote zilizopigwa.
Mpina na Othman wamesindikizwa na mgombea mwenza wa umakamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, Fatma Fereji, Kiongozi wa ACT Wazalendo, Dorothy Semu, Makamu Mwenyekiti wa chama hicho (Bara), Isihaka Mchinjita na Katibu Mkuu, Ado Shaibu.
Viongozi hao baada ya kuwasili mjini hapa watafanya metembezi katika barabara mbalimbali kuanzia eneo la Malindi, Darajani, Kisiwandui, Kisonge hadi Michenzani ambako watazungumza na wananchi.