Mapishi ya wali wa biriani

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,268
33,040
WALI WA BIRIANI

Mchele kilo 1

Nyama kilo 1


Samli ½ kilo


Mbatata ½ kilo


Vitunguu maji kilo 1


Thomu gram 150


Tangawizi mbichi gram 150


Hiliki gram 50


Mdalasini gram 100

Mtindi painti 1

Siki kiasi


Majani ya nanaa fungu moja


Chumvi kiasi


Zaafarani kidogo (irowekwe kwa maji ya moto nusu kikombe cha kahawa)


Tungule ilosagwa


Tungule ya kopo


1 Menya vitunguu maji uvioshe uvikate. teleka sufuria utie samli, ikichemka tia vitunguu uvikaange bila ya kuvivuruga mpaka viwe vyekundu. Vichuje uvitoe

halafu vitandaze katika sinia.


2 Twanga mdalasini na hiliki mpaka viwe laini kama unga. Menya thomu uitwange pamoja na tangawizi mbichi.


3 Kata nyama vipande vikubwa kisha tia chumvi na vitu ulivyovisaga (yaani tangawizi mbichi na thomu) vile vile tia unga unga wa mdalasini na hiliki

pamoja na mtindi wa maji. Pika mpaka karibu nyama kuiva kabisa ndipo utie mbatata. Ukiona mbatata zimeshaiva tia siki.Usiache kukauka kabisa, bakiza

rojorojo. Tia maji katika sufuria na chumvi yakichemka tia mchele. Acha utokote, angalia kiini cha wali ukiona umeshaiva uchuje.


4 Angalia sufuria ya nyama na rojo lake lisiwe limekauka kabisa, lazima ziwe na maji kidogo. Chukua vile vitunguu ulivyovikaanga vikapoa uvinyunyuzie juu

ya masalo yote (usikoroge). Halafu utie mchele uliouchuja, nyunyuzia maji ya zaafarani juu ya wali wote halafu unyunyuzie samli ile uliyochuja kutoka

kwenye vitunguu ulivyovikaanga ienee juu ya wali wote. Kisha funika upalie makaa.


5 Wali ukishakuwa tayari utaupakua. lakini unapotaka kuupakua lazima kwanza uutoe wali wote mweupe uutie katika chombo chengine, halafu uyakoroge

masalo yachanganyike sawasawa kisha ndio uyatie juu ya wali katika kila sahani.
 
mkuu mbona vitu mingi hivo? vinapikwa kwene pipa nn? mpaka tunguli duuuu hii kitu ukila siku moko tu unakuwa mpemba wa buguruni.
 
  • Thanks
Reactions: amu

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom