Mapishi ya maandazi

....Nafikiria kuweka asali badala ya sukari, je kuna aliyewahi kujaribu na kunaweza kuwa na reaction yoyote ? Isijekuwa makemikali yakachanganyika na kutengeneza haidrojen oksaidi na kujikuta unajamba 24/7 mpaka ikweta inawaka moto ...ingawa eti kuna bazungu wanatuzuga eti hewa itokanayo na mashuzi inasaidia kutibu magonjwa ! Hawa si wanakula fishi n chips, au popkoni, wakafanye utafiti wa yale matumbo yanayoshindiliwa viporo vya maaragwe, vizazi vitamu na kushushiwa na mtindi.....halaf catalyst ya karanga za kuchemsha teh teh teh teh :)
 
Wanaukumbi.

MAHITAJI



Unga wa ngano kl 1
Sukari kikombe 1 cha chai
Hamira kijiko 1 kikubwa
Chumvi kijiko 1 kidogo
Mayai 3
Blue band vijiko 3 vikubwa
Baking powder kijiko 1 kidogo
Hiliki ½ kijiko cha chai
Maziwa ½ lita/tui la nazi/maji
Mafuta ya kuchomea maandazi














MATAYARISHO.



·Weka unga kwenye bakuli kubwa alafu weka sukari,chumvi,hiliki,hamira,baking powder,Changanya vizuri kwa kutumia vidole
·Changanya mchanganyiko wako na mayai kisha blue band endelea kuchanganya mchanganyiko wako
·unaweza ukaweka maziwa/tui la nazi au maji,unatumia kimoja wapo utachopenda kutumia
·Endelea kukanda unga wako hadi liwe donge laini
·Alafu yakate madonge makubwa makubwa unaweza ukatoa madonge matano,unaweka unga kwenye kibao cha kusukumia chapatti na kuanza kulisukuma donge moja moja hakikisha haliwi jembamba sana wala nene sana
·Baada ya hapo waweza kata kata shape yoyote unayoipenda na kuweka vipande vyako kwenye sinia au ungo ambao utakuwa umenyunyuzia unga kwa chini
·Yaweke sehemu yenye joto ili yaweze kuumuka kwa muda wa nusu saa yatakua yameumuka tayari
·Weka kikaango chako kwenye moto kisha weka mafuta yakishachemka unaanza kuchoma maandazi yako hadi yawe na rangi ya brown


Maandazi yako yatakua matamu na laini pia…,waweza nywea chai, supu, mchuzi mzito, maharage.

Hamira kijiko 1
Halafu baking powder kijiko 1
Kama sijaelewa ??!
 
Ni matamu kwa kweli nimejaribu
 

Attachments

  • 1405706118672.jpg
    1405706118672.jpg
    71.3 KB · Views: 544
Supu ya samaki ilihusika
 

Attachments

  • 1405706324428.jpg
    1405706324428.jpg
    46.4 KB · Views: 487
ANDAZI.jpg
Ngano 1 kg
Tui la nazi 800 ml
Sukari 120 gr
Hamira 20 gr
Iliki Grinded 10 gr
mafuta vijiko vitatu vikubwa
 
Aiseee hii kitu nilikuwa naitafuta kuliko maelezo,nimechoka kula mikate kila siku.
Nalog off
 
Samahani wapendwa wangu!!
Hivi unapokanda maandazi ni ada kukandia maji ya moto au baridi ili yawe laini?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom