m.agape
Senior Member
- Dec 7, 2012
- 141
- 79
Habari wana jukwaa.
Najitokeza kwenu kuomba mafunzo ya upishi wa kisamvu.
Nimekula kisamvu kwenye sherehe kitamu sana
Nifunzeni nipate kukipika mwenyewe nyumbani.
Asanteni
Recipe ya mama yangu.
Mahitaji
1: kisamvu kilichotwangwa na vitunguu saum, (waweza blend kama huna kinu) vikombe 2
2: vitunguu maji viwili vikubwa.
3: mafuta kidogo
4: karanga zilizosiginwa (sagwa na kulainika) 3/4 kikombe.
5: chumvi kwa ladha.
Hatua
1: chemsha kisamvu kwa maji mengi mpaka kiive (mara nyingi utahitaji kuongeza maji maana kisamvu kina sumu ambayo huondoshwa kwa joto)
2. Chukua sifuria nyingine, weka mafuta na kaanga vitunguu vyako mpaka vilainike na kuanza kubadili rangi.
3: Weka kisamvu kwenye vitunguu, kaanga kwa dakika 3-5.
4: Weka karanga na changanya kama unasonga ugali vile mpaka ichanganyikane vizuri ongeza na chumvi kwa ladha.
NB:
Waweza weka nyanya wakati unakaanga vitunguu.
Kisamvu cha Kinyamwezi hakina mchuzi hivyo hakikisha maji yamepungua au kukauka wakati unaweka kwenye vitunguu vyako.
Karanga nyingi ni siri ya kisamvu cha kinyamwezi
Ngoja watumia nazi waje watoe namna yao.