Mapishi – Mchemsho wa Samaki

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,280
Leo jikoni tunaangalia mapishi ya mchemsho wa samaki. Mchemsho huu ni kwa ajili ya watu wawili.





Mahitaji
. Samaki wakubwa kiasi 2 (Hapa natumia changu)
. Viazi mviringo 5
. Bamia, karoti, pilipili hoho na kitunguu maji
. Tangawizi
. Ndimu 2
. Chumvi

Matayarisho
1. Andaa samaki na kisha ukamulie ndimu moja.
2. Menya viazi na ukate vipande vinne kila kiazi.
3. Katakata bamia, karoti, kitunguu na pilipilh hoho.
4. Menya tangawizi na uitwange.
5. Bandika viazi na maji kiasi kisha weka chumvi na vitunguu.
6. Vikianza kuiva weka tangawizi, hoho, karoti, bamia na samaki. Hakikisha kuna supu ya kutosha ila isiwe nyingi sana.
7. Acha vichemke kwa dakika kumi hadi 15 kisha epua.

Andaa mezani ukiweka kipande cha ndimu, nyanya na tango.
 
Binafsi huwa sipendi bamia,kuna umuhimu wa kuweka bamia katika hiyo soup?
 
Yaani bamia zinapigwa vita balaa
Hahaahhah mie wala sijafika huko ulipo

Mi nimesemea bamia hizi blog-image-okra.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom