Mapishi Mbalimbali ya Muhogo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mapishi Mbalimbali ya Muhogo

Discussion in 'JF Chef' started by ndetichia, Aug 19, 2011.

 1. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #1
  Aug 19, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  TAMBI ZA MIHOGO


  Mahitaji

  a) vikombe 3 vya unga wa mihogo
  b) kikombe 1 ½ cha unga wa soya
  c) yai 1
  d) kijiko 1 cha unga wa curry
  e) chumvi kiasi kidogo kwa ladha
  f) maji
  g) mafuta ya kupikia


  Jinsi ya kupika
  chuja unga wa mihogo changanya unga wa mihogo na unga wa soya kwa pamoja koroga yai kando kabla ya kuchanganya weka yai, chunvi na unga wa curry katika unga wa mihogo na soya uliochanganywa changanya kwa mikono ongeza maji kidogo kidogo mpaka ichanganyike vizuri weka mafuta kidogo katika mchanganiko tengeneza kwa mikono mfano wa tambi pika tambi kwenye mafuta yaliyochemka vizuri
  CASSAVA DONATS
  Mahitaji

  a) kikombe 1 cha unga wa mihogo
  b) kikombe 1 cha unga wa ngano
  c) kijiko 1 cha mdalasini
  d) vijiko 2 vya baking powder
  e) kikombe 1 ½ cha sukari
  f) mayai 2
  g) kikombe 1 cha maziwa
  h) kikombe 1 cha blue band (siagi)
  i) limau/chungwa 1
  l) chunvi kidogo
  m) mafuta ya kupikia


  Jinsi ya kupika
  chuja unga changanya unga wa mihogo na wa ngano kwa pamoja kwenye sufuria koroga siagi na sukari, alafu mayai kando kabla ya kuchanganya na unga weka mdalasini, maji ya limau/orange na baking powder changanya vyote ukitumia mikono, ongeza maziwa pole pole mpaka mchanganyiko uwe laini

  1

  kanda mchanganyiko juu ya meza na skuma tengeneza umbo la mviringo (unaweza kutumia kikombe) na katikati tengeneza umbo la mvringo
  ndogo (unaweza kutumia kifuniko cha chupa) pika kwenye mafuta yaliyochemka.
  POPED CASSAVA

  Mahitaji

  a) kikombe 1 cha unga wa mihogo
  b) kikombe 1 cha maji
  c) mafuta ya kupikia
  d) chumvi au sukari

  Jinsi ya kupika
  chemsha maji halafu weka kwenye karai weka unga wa mihogo kidogo kidogo kwa maji mpaka mchanganiko uwe nyepesi ongeza chumvi au sukari ukishashikana gawanya vipande vidogo vidogo kama umbo la duara weka kwenye mafuta yaliyochemka, pika mpaka ziwe na rangi ya kupendeza (kama ya mchanga) andaa mikate hii na chai.  MKATE WA MIHOGO

  Vitu vinavyohitajika na vipimo

  a) kikombe 1 cha unga wa mihogo
  b) vikombe 3 vya unga wa ngano
  c) kijiko 1 ½ cha hamira
  d) kijiko 1 cha sukari
  e) vijiko 3 vya siagi/blue band
  f) vijiko 2 vya chumvi
  g) kikombe ½ cha maziwa
  h) kikombe 1 cha maji


  Jinsi ya kupika
  weka hamira kwenye kikombe cha maji ya vugovugo, ongeza sukari, changanya kisha acha
  kwa dakika kumi chuja unga wa ngano na unga wa mihogo, weka kwenye karai, weka chumvi ongeza siagi na maziwa changanya vyote kwa pamoja, kisha katika mchanganyiko huu tengeza shimo katikati weka yale maji ya vugovugo yaliochanganywa na hamira na sukari changanya vyote kwa pamoja, na unaweza kuongeza maziwa mpaka mchanganyiko uwe
  sawasawa, yaani usiwe gumu zaidi au nyepesi zaidi

  2

  funika kwa kitambaa, weka nje kwenye jua kwa dakika kumi mpaka umuke ikishaumuka, kanda tena, paka siagi kidogo juu na kwenye chombo utakachotumia kuoka
  mkate weka karibu na moto kwa dakika chache ili imuke tena ikishamuka oka mkate ndani ya tanuri(oven)
  MIKATE MIDOGO (SCONES)

  Vitu vinavyohitajika na vipimo

  a) kikombe 1 ½ cha unga wa mihogo
  b) kikombe ½ wa unga wa ngano
  c) kikombe 1 ½ cha sukari
  d) vijiko 4 vya siagi
  e) yai nyeupe 1
  f) kijiko 1 cha hamira
  g) kijiko 1 cha mdalasini
  h) kikombe ½ cha maziwa
  i) iliki
  j) simsim au ufuta

  Jinsi ya kupika
  weka hamira kwenye kikombe cha maji ya vugovugo, ongeza kijiko kimoja cha sukari,
  changanya, kisha acha kwa dakika kumi chuja unga wa ngano na unga wa mihogo, weka kwenye karai, weka sukari na changanya
  pamoja weka siagi na iliki weka yai nyeupe pekee, simsim au ufuta, mdalasini na maziwa kiasi mwisho weka yale maji ya vugovugo, halafu changanya vyote kwa pamoja ukitumia mikono ukishachanganya, paka siagi kidogo kwenye sinia utakayotumia kuoka mikate tengeza umbo la duara au umbo aina nyingine, bora yawe madogo weka kwenye sinia paka yai nyeupe juu, halafu weka simsim au ufuta juu weka kwenye jua kwa dakika chache mwisho yakishaumuka weka ndani ya oven kwa dakika kumi
  CHAPATI ZA MAJI ZA MUHUGO

  Vitu vinavyohitajika na vipimo

  a) mihogo 2
  b) kijiko 1 cha tangawizi
  c) yai 1
  d) kikombe 1 cha mafuta
  e) vijiko 2 vya sukari

  3


  Jinsi ya kupika
  osha halafu chambua na menya mihogo futa ukitumia kitambaa kisafi chonga mihogo kwa vipande vidogo, weka kwenye sufuria au karai, ongeza sukari, yai na
  tangawizi changanya uwe mchanganyiko sawasawa, kanda, kisha skuma, kata vipande vile
  unavyopenda pika kwenye mafuta yanayochemka.
  KEKI YA MIHOGO

  Vitu vinavyohitajika na vipimo

  a) vikombe 4 vya mihogo iliyokunwa
  b) vikombe 2 vya unga wa ngano
  c) kikombe 1 cha sukari
  d) kikombe 1 cha siagi
  e) mayai 2
  f) kikombe 1 cha maziwa
  g) vijiko vidogo 4 vya baking powder
  h) chumvi kidogo
  i) chungwa/limau/mdalasini/zabibu

  Jinsi ya kupika
  weka sukari na siagi, changaya mpaka ilainike weka mihogo iliokunwa kwenye karai ongeza mayai na maziwa, changanya weka unga wa ngano kwenye karai, weka baking powder changanya mchanganyiko wote kwa pamoja mpaka ushikane na uwe laini, usiwe majimaji au
  ngumu paka siagi kidogo kwenye sufuria ya kuoka na unga juu, kisha weka mchanganyiko wote mwisho kabisa oka kwa kutumia oven yenye moto kidogo kwa dakika kumi na tano.
  KEKI YA UNGA WA MIHOGO

  Vitu vinavyohitajika na vipimo

  a) vikombe 2 vya unga wa mihogo
  b) kikombe 1 cha sukari
  c) kikombe 1 cha blue band/siagi
  d) kijiko 1 ½ cha baking powder
  e) mayai 5
  f) mdalasini

  4

  g) chumvi kiasi kidogo
  h) chungwa 1

  Jinsi ya kupika
  changanya sukari na siagi mpaka iwe laini, na koroga, pia weka mayai, maji ya chungwa
  (ukipenda unaweza kuongeza maganda ya chungwa vipande vidogo vidogo ) chuja unga, changanya unga wa mihogo, baking powder, mdalasini, chumvi kidogo kwa
  bakuli nyingine changanya vyote kwa pamoja na koroga paka siagi na unga kidogo kwenye sinia utakayopikia keki yako weka mchanganyiko wote ndani ya sinia oka kwenye tanuri (oven)  KEKI YA UNGA WA WIMBI, MTAMA NA MIHOGO

  (QUEEN CAKE)

  Vitu vinavyohitajika na vipimo

  a) kikombe 1 cha mtama/wimbi
  b) kikombe 1 cha mihogo
  c) vikombe 2 vya unga wa ngano
  d) vikombe 2 vya sukari
  e) vikombe 2 vya siagi
  f) mayai 6
  g) kikombe ½ cha korosho
  h) kikombe ½ cha maziwa
  i) chumvi kidogo
  j) vijiko 3 vya baking powder
  k) kijiko 1 cha maganda ya limau yalioparuzwa/yaliokunwa

  Jinsi ya kupika
  changanya sukari na siagi pamoja mpaka iwe laini ongeza mayai, maziwa, korosho na maganda ya limau, changanya mpaka mchanganyiko uwe
  laini kwenye bakuli nyingine chuja unga, changanya unga wote tatu, weka baking powder na
  chumvi kidogo changanya vyote kwa pamoja na koroga paka siagi na unga kidogo kwenye sufuria ya kupikia weka mchanganyiko ndani ya sufuria na oka kwa oven


  Kwa wale wapendao mihogo mshindwe wenyewe na ukifanikiwa usisahau kunipa thanks asubuhi njema..
   
 2. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #2
  Aug 19, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  halafu hiyo article imekuwa ndefu kidogo msishangae..
   
 3. farkhina

  farkhina Platinum Member

  #3
  Dec 16, 2014
  Joined: Mar 14, 2012
  Messages: 12,831
  Likes Received: 775
  Trophy Points: 280
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. Angel Nylon

  Angel Nylon JF-Expert Member

  #4
  Dec 19, 2014
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 4,471
  Likes Received: 1,472
  Trophy Points: 280
  Lol,

  Naona sijaona mihogo ya Nazi wala makopa. Lol.

  Kuna visheti vya muhogo pia, uji. Tushindwe wenyewe tu
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...