Mapinduzi ndani ya kizimba... (CCC)

Mapinduzi ndani ya kizimba... (CCC)

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
360,169
Reaction score
829,112
Kuna kitu kinaitwa Closed Circuit Coup. Ama CCC. Mambo ni mengi muda mchache.

Teknolojia ya upashanaji Habari, mawasiliano, majadiliano na hata malumbano ya hoja sasa vinaweza kufanyika kwa ufanisi mkubwa bila watu kuonana wala kufahamiana kabisa....!!!

Hapo kabla taarifa za kaya nzima zilikuwa zinamfikia mtemi mkuu kupitia taratibu maalum za ngazi za kiuongozi toka chini mpaka juu kabisa.

Na taarifa za usalama wa kaya zinapaswa kufika juu kabisa kabla ya saa 5 asubuhi kila siku iendayo kwa Mungu
Mambo kwasasa yamebadilika mno.

Ndani ya kaya kubwa habari zake zinaweza kuenea kote ndani ya muda mchache na bila hata kuzingatia ule utaratibu rasmi. Kuna athari zake kwenye hili.

Kuna baadhi ya habari ama taarifa kaya inazipata mapema kabisa kabla bila hata kuhakikiwa, kuhaririwa ama kuchujwa. Kiusalama hili ni jambo hatari sana.

Zingatio la kwamba jamii ipate nini ama ilishwe nini kwa wakati gani lina umuhimu wake mkubwa sana.

Lakini kwa maendeleo haya ya upashanaji habari enzi hizi yamevunja taratibu na miiko mingi.

Ndio maana kwa wenzetu waliojiandaa wamedhibiti kwa kiasi kikubwa hili lakini bado wakizingatia haki ya msingi ya kupeana taarifa kwa wanakaya wote na kati ya mtu na mtu, mtu na kikundi na kinyume chake.

Ni kwa muktadha huo basi, mwaliko wa mtemi kwenye boma la kabumbu ama shughuli fulani ya kaya.

Unaweza kuwa kiama kikubwa kwa kujikuta nyie wote na mtemi wenu mnawekwa chini ya karantini na kushikiliwa mateka. Na wanakijiji waliochoka na wenye wenye kuchukua magumu....!!!!

Kwa jinsi dunia inavyokwenda kwa kasi na akili za kizazi kipya zinavyochanganya haraka na zenye maamuzi ya papo kwa papo.

Siku hizi hawasubiri kuvamia kizimba cha korokoroni wa kaya ili wajitwalie marungu pinde na mishale....!

Ama hawaendi kuzingira pale kwenye bango la habari na kuandika kwa maandiko makubwa.

KUANZIA SASA TUMESHIKA HATAMU, la hasha wala hawamvizia mtemi Chifu akiwa kwenye boma lake, wamtie kabari na kumlazimisha kutamka kuwa hataki tena kuwa chifu wa kaya.

Maboma na vizimba visivyo wazi pande zote vinaweza kutumika vibaya kwa nyakati hizi kuwalazimisha watemi na machifu wakimbie kaya zao huku wakikimbizwa na kutaabika hasa.

Hawa korokoroni na wasungusungu wetu wakichoka kutaabika na kukutana wale magangwe waganga njaa huko na huko.
Moyo wa mtu ni kiza kinene.
 
.
IMG_20190529_104323.jpeg
 
mshana unaandaa mapinduzi nini
Mbunge Nape : Kuna ugonjwa wa Dengue na vifo vimeanza kuripotiwa,Serikali inachukua hatua gani, DSM hali ni mbaya?

Naibu Waziri Ulega : Kweli kuna Dengue hasa DSM, Serikali imeguundua moja ya tatizo ni gharama kubwa inayolipwa na wagonjwa wa Dengue, gharama zitapungua.

#Bungeni
UMEELEWA?

Kaya inaumwa.... Tukiweza tukajirembe tujitwalie warembo waliorembeka tusahau shida zetu
IMG-20190529-WA0020.jpeg
 
Aliyeelewa anieleweshe!
Mbunge Nape : Kuna ugonjwa wa Dengue na vifo vimeanza kuripotiwa,Serikali inachukua hatua gani, DSM hali ni mbaya?

Naibu Waziri Ulega : Kweli kuna Dengue hasa DSM, Serikali imeguundua moja ya tatizo ni gharama kubwa inayolipwa na wagonjwa wa Dengue, gharama zitapungua.

#Bungeni
UMEELEWA?

Kaya inaumwa.... Tukiweza tukajirembe tujitwalie warembo waliorembeka tusahau shida zetu
 
Kuna kitu kinaitwa Closed Circuit Coup... Ama CCC.... Mambo ni mengi muda mchache.... Teknolojia ya upashanaji Habari, mawasiliano, majadiliano na hata malumbano ya hoja sasa vinaweza kufanyika kwa ufanisi mkubwa bila watu kuonana wala kufahamiana kabisa....!!!
Hapo kabla taarifa za kaya nzima zilikuwa zinamfikia mtemi mkuu kupitia taratibu maalum za ngazi za kiuongozi toka chini mpaka juu kabisa... Na taarifa za usalama wa kaya zinapaswa kufika juu kabisa kabla ya saa 5 asubuhi kila siku iendayo kwa Mungu
Mambo kwasasa yamebadilika mno... Ndani ya kaya kubwa habari zake zinaweza kuenea kote ndani ya muda mchache na bila hata kuzingatia ule utaratibu rasmi.... Kuna athari zake kwenye hili.... Kuna baadhi ya habari ama taarifa kaya inazipata mapema kabisa kabla bila hata kuhakikiwa, kuhaririwa ama kuchujwa.... Kiusalama hili ni jambo hatari sana...
Zingatio la kwamba jamii ipate nini ama ilishwe nini kwa wakati gani lina umuhimu wake mkubwa sana.... Lakini kwa maendeleo haya ya upashanaji habari enzi hizi yamevunja taratibu na miiko mingi... Ndio maana kwa wenzetu waliojiandaa wamedhibiti kwa kiasi kikubwa hili lakini bado wakizingatia haki ya msingi ya kupeana taarifa kwa wanakaya wote na kati ya mtu na mtu, mtu na kikundi na kinyume chake....
Ni kwa muktadha huo basi, mwaliko wa mtemi kwenye boma la kabumbu ama shughuli fulani ya kaya.... Unaweza kuwa kiama kikubwa kwa kujikuta nyie wote na mtemi wenu mnawekwa chini ya karantini na kushikiliwa mateka.... Na wanakijiji waliochoka na wenye wenye kuchukua magumu....!!!!
Kwa jinsi dunia inavyokwenda kwa kasi na akili za kizazi kipya zinavyochanganya haraka na zenye maamuzi ya papo kwa papo.... Siku hizi hawasubiri kuvamia kizimba cha korokoroni wa kaya ili wajitwalie marungu pinde na mishale....! Ama hawaendi kuzingira pale kwenye bango la habari na kuandika kwa maandiko makubwa... KUANZIA SASA TUMESHIKA HATAMU... la hasha.....wala hawamvizia mtemi chifu akiwa kwenye boma lake, wamtie kabari na kumlazimisha kutamka kuwa hataki tena kuwa chifu wa kaya...
Maboma na vizimba visivyo wazi pande zote vinaweza kutumika vibaya kwa nyakati hizi kuwalazimisha watemi na machifu wakimbie kaya zao huku wakikimbizwa na kutaabika hasa....
Hawa korokoroni na wasungusungu wetu wakichoka kutaabika na kukutana wale magangwe waganga njaa huko na huko.... Moyo wa mtu ni kiza kinene....
@Mshana Jr umeniacha
Hoja ina mianya mingi tu
kuna fumbo kadha wa kadha
Njia kufumbua yawa ngumu
Kujua lengolo hasa nini tabu
Kikomoto na njiaze zabuma

Wamaanisha mapinduzi yetu
Kumtoa kilingeni mtemi wetu
Kumleta asiyewetu kilingeni
Nje ya mfumo kuntu maishani

Wamaanisha wanaharakati
Mfanole wa kibabe wa Mkiru
Kuchukua yetu sirikali kiutata
Kuwafanya wababe wahanga
Wahanga wa mawasiliano tu

Mfumo wa kuwasiliana utata
Hakuna mfumo imara kizaman
Mangaka hadi Mlele vurugu tu
Wawasiliana kubashana habari
Hakuna uchujaji wala uhariri
Hakuna ukweli wala uwongo
Zote zasambaa; naam moto
Moto kichaa wakati wa hari
Majani makavu upeponi mkali

Oooops Mungu tunusuru waja

Bazazi
 
Back
Top Bottom