Mapinduzi NCCR Mageuzi

Mzito Kabwela

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2009
Messages
18,114
Points
2,000

Mzito Kabwela

JF-Expert Member
Joined Nov 28, 2009
18,114 2,000
- Mbatia kung'olewa uenyekiti September
- Aponzwa na Halima Mdee
- Yadaiwa alihongwa 2010, utajiri wake wahojiwa

Mpango wa kumng'oa madarakani Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia kwa madai kuwa ni pandikizi wa CCM ndani ya chama hicho sasa umekamilika na kinachosubiriwa ni siku ya kumpindua ambayo inatarajiwa kuwa katikati ya mwezi September.
Habari za kuaminika zilizoifikia gazeti la Dira ya Mtanzania kutoka ndani ya chama hicho zinzeleza kuwa hatua hiyo imefikiwa baada ya jopo la wazee kuibuka na hoja kuwa mbali ya Mbatia kuwa pandikizi la CCM pia amekosa mvuto wa kisiasa na amekuwa akitofautiana na wanamageuzi wenzake katika mambo ya msingi yanayokihusu chama hicho kitaifa.
Mmoja wa makada wa chama hicho znzyeingia katika vikao vya juu vya maamuzi alisema kuwa mpango wa kutaka kumpindua Mbatia ulianza baada ya kumalizika kwa uchaguzi wa 2010 ambapo chama hicho kilifanikiwa kupata wabunge wanne. Anasema kabla ya kufanyika kwa uchaguzi kulikuwa na tetesi miongoni mwa watanzania wengi kuwa Mbatia alihongwa ili kudhoofisha nguvu ya upinzani jambo ambalo lilipunguza imani ya wananchi kwa chama hicho. Kada huyo alisema tathmini ya uchaguzi mkuu iliyofanywa na chama hicho ilibaini kuwa ingawa chama hicho kilifanikiwa kupata wabunge wanne lakini HAKIKUWA na mvuto kwa wananchi nq pia kimekuwa kikihusishwa na ushirika na CCM jambo ambalo linazidi kukididimiza.
Wakati kada huyo akiyaeleza hayo taarifa zaidi zinasema tayari vikao vitatu vya kumshinikiza vimekwishafanyika na kwamba baada ya kutaarifiwa kuhusu hatua hiyo ALIUGUA na baadae akawa ANATOKWA NA DAMU PUANI. Hata hivyo Mbatia anadaiwa kupambana katika vikao hivyo ambapo baada ya kushinikizwa aachie ngazi katika kikao kilichoketi Agosti 13 mwaka huu jijini Dark es salaam alilalamika kwa wajumbe kuwa wameamua kumwonea na kumdhalilisha na shinikizo lilipozidi alisimama na kupiga meza ngumi huku akivunja glass za maji kabla ya kudhibitiwa na wajumbe wenzake wa kikao. Ingawa amekuwa akishindwa kila uchaguzi lakini kushindwa na mwanamke tena kwa tofauti ya kura 33,000 kuliwasikitisha sana wanachama ikizingatiwa kuwa wenyeviti wenzake wote wa vyama vya upinzani waligombea ubunge wakashinda. Wanachama hasa vijana wanahoji sababu ya Mbatia kukimbilia mahakamani baada ya kushindwa na Mdee kwa sababu hatua hiyo ni sawa na kutaka kupunguza idadi ya wabunge wa upinzani jambo ambalo limekuwa likipiganiwa na wanamageuzi wengi nchini.
mbatia anamiliki magari manne ya kifahari na anadhaniwa kuwa na mali nyingine zaidi lakini kuna shaka kuhusu kazi inayomwezesha kuweza kumiliki magari hayo na hizo mali zingine jambo linalozua shaka kwamba inawezekana anatumiwa kwa mapato manono na baadh ya wanasiasa kwa maslahi yao binafsi au hata ya vyama vyao
source Dira ya Mtanzania
 

Mwita25

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2011
Messages
3,838
Points
0

Mwita25

JF-Expert Member
Joined Apr 15, 2011
3,838 0
Waache wafu wazikane, vita vya panzi kama hawa Chadema, NCCR, TLP etc ndiyo furaha ya kunguru CCM. Sasa tunasubiri CHADEMA nao watoane ngeu juu ya Shibuda na Zitto. Yetu (CCM) macho tu.
 

Raimundo

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2009
Messages
13,510
Points
2,000

Raimundo

JF-Expert Member
Joined May 23, 2009
13,510 2,000
Waache wafu wazikane, vita vya panzi kama hawa Chadema, NCCR, TLP etc ndiyo furaha ya kunguru CCM. Sasa tunasubiri CHADEMA nao watoane ngeu juu ya Shibuda na Zitto. Yetu (CCM) macho tu.
Subiri nyumba ya THT na studio virudi mikononi mwa wananchi ndio utaj.ua kama CCM si watu, kwa sasa kwa sababu bado wanakudhamini nemeeka.
 

Wanitakiani

JF-Expert Member
Joined
Apr 18, 2008
Messages
641
Points
0

Wanitakiani

JF-Expert Member
Joined Apr 18, 2008
641 0
News from a fake source.
Very very unreliable source! si ni hili gazeti la Dira lilituambia Prof. Mwandosya kaandika barua ya kujiuzulu? Ikulu wamekanusha, Naibu Waziri Maji amakanusha na jana Prof. ameongea toka India na ikarushwa live kwenye runinga akizishangaa hizo habari? Achaneni na kanjanja Charles Mulinda jamani!
 

The Magnificent

JF-Expert Member
Joined
Jan 6, 2011
Messages
2,695
Points
1,500

The Magnificent

JF-Expert Member
Joined Jan 6, 2011
2,695 1,500
Waache wafu wazikane, vita vya panzi kama hawa Chadema, NCCR, TLP etc ndiyo furaha ya kunguru CCM. Sasa tunasubiri CHADEMA nao watoane ngeu juu ya Shibuda na Zitto. Yetu (CCM) macho tu.
<br />
<br />
plz badilisha id,wakurya ni Watu wenye msimamo na siyo mashoga kama wewe,unalidhalilisha kabila langu
 

Forum statistics

Threads 1,355,629
Members 518,708
Posts 33,114,195
Top