Mapigano ya wakulima na wafugaji Morogoro: Rutengwe alitenguliwa ukuu wa mkoa, Kebwe anapeta tu

Modibo

JF-Expert Member
Apr 20, 2016
425
700
Ni takribani mwaka mzima sasa tangu tutangaziwe kwa mbwembwe sana mabadiliko ya mikuu wa mikoa.

Miongoni mwa waliotenguliwa ni mkuu wa mkoa wa morogoro Dr Rajab Rutengwe.

Rais alituambia hawezi kuwa na mkuu wa mkoa aliyeshindwa kushughulikia na kusuluhisha migogoro ya wakulima na wafugaji. Akamteua Dr. Steven Kebwe badala yake.

Ni karibu ya mwaka sasa , lakini tunashuhudia mapigano ndo yanazidi! watu wanakatwa mapanga, wanauana, wanachomana visu na mikuki!

Mapigano yameshika kasi kKilosa, Kilombero na Morogoro vijijini lakini mkuu wa mkoa wa sasa bado anapeta tu!

Najiuliza hivi ni kweli kutumbuliwa kwa Rutengwe ilikuwa ni sababu hii au kuna lililojificha?
 
Usiamshe vilivyolala... Hata hivyo yule alikua hawezi alikua mchumia tumbo..Dr mzima analialia njaa
 
Dr Kebwe akitenguliwa utapata faida gani wewe.Ungekuwa mkazi wa Morogoro ungekuwa unajua juhudi anazochukua Dr Kebwe ktk jambo hilo lkn ni ukweli usiopingika kuwa maovu na waovu havitaisha hata kiongozi awe mkali kiasi gani
 
Dr Kebwe akitenguliwa utapata faida gani wewe.Ungekuwa mkazi wa Morogoro ungekuwa unajua juhudi anazochukua Dr Kebwe ktk jambo hilo lkn ni ukweli usiopingika kuwa maovu na waovu havitaisha hata kiongozi awe mkali kiasi gani
una uhakika dr rutengwe alikuwa hafanyi juhudi?acha biasness
 
Wateule wa Mtukufu Huwa hawakosei bwana,waliokuwa wanakosea ni wale wa zamani
 
Una uhakika Rutengwe alitimuliwa shauri ya mapigano ya wakulima na wafugaji?
 
Back
Top Bottom