Mapigano makali baina ya Syria na Turkey yatokea

Mapigano makali baina ya Syria na Turkey yatokea

STRUGGLE MAN

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2018
Posts
8,633
Reaction score
16,601
Mapigano yashtadi kati ya majeshi ya Uturuki na Syria, askari kadhaa wa pande mbili wauawa

Feb 04, 2020 07:40 UTC

[https://media]

Askari kadhaa wameuawa na kujeruhiwa katika mapigano kati ya majeshi ya Syria na Uturuki yaliyotokea kwenye eneo la kaskazini ya ardhi ya Syria.

Mapigano hayo yalitokea jana baada ya msafara wa majeshi ya Uturuki kuingia kwenye mkoa wa Idlib kaskazini magharibi mwa Syria.

Kufuatia hatua hiyo ya jeshi la Uturuki ya kuingia kinyume cha sheria mkoani Idlib, jeshi la Syria lilishambulia kwa makombora ya mizinga ngome za jeshi hilo na kuwaua askari sita na kuwajeruhi wengine wapatao 20.

Kwa upande mwingine, askari wasiopungua sita wa Syria wameuawa katika mashambulio yaliyofanywa na jeshi la Uturuki dhidi ya ngome za jeshi hilo.

Tangu siku kadhaa nyuma, jeshi la Syria limeanzisha operesheni ya kuukomboa mji wa Idlib kutoka kwenye makucha ya magaidi.

Sambamba na hatua hiyo, Rais Recep Tayyip Erdoğan wa Uturuki alitangaza: 'Kuanzia sasa, na sisi pia tutazilenga ngome za vikosi vya Syria.' Aidha, Erdogan ameitaka Russia, ambayo ni muitifaki wa Syria, isiingilie mashambulio ya Uturuki dhidi ya jeshi la Syria.

[https://media]

Uturuki inadai kuwa wanajeshi wake wako katika eneo la Idlib kwa lengo la kusimamia usitishaji vita.

Hii ni pamoja na kuwa, makundi ya kigaidi yaliyopo katika eneo hilo yamekiuka usitishaji mapigano mara kadhaa na kutenda anuai za jinai katika eneo hilo.

Kufuatia kushambuliwa ngome za jeshi la Uturuki ndani ya ardhi ya Syria, maafisa kadhaa wa serikali ya Ankara akiwemo waziri wa mambo ya nje na msemaji wa rais wamedai kuwa, kushambuliwa ngome za jeshi la Uturuki kumekiuka hati ya makubaliano ya Idlib na kwamba waliohusika na shambulio hilo watakabiliwa na jibu la nchi hiyo.

Ikumbukwe kuwa serikali ya Syria ilishatahadharisha mara kadhaa kuhusu matokeo hasi ya uingiaji kinyume sheria ndani ya ardhi ya nchi hiyo unaofanywa na askari wa Uturuki; na ikatangaza kuwa, uvamizi huo unakiuka mamlaka yake ya kujitawala, hivyo ni lazima Uturuki iondoke katika ardhi ya Syria haraka iwezekanavyo.../



4bv6f8bd1e99801laxt_800C450.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Majeshi ya Syria na Rais wao wamepumbazwa na Russia kiasi kwamba wamesahau malengo yao.
Turkey atawanyoosha ni panya huyo anauma na kupuliza
 
Jeshi la Syria lina uzoefu wa mapambano, Uturuki itapoteza askari wengi sana maana haina msuli wa full scale war ndani ya Syria
Hata mim ndicho nachokiona, uturuk wanaweza kuwa na vifaa vya kisasa zaid ila jeshi la syria lina uzoefu sana wa vita, mwaka wa nane hui wanapigana, uturuk ijiandae kupoteza askari wengi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom