Mapigano kusitishwa Sudan Kusini

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Pande mbili zinazohasimiana na kusababisha kuzuka upya kwa vurugu nchini Sudan Kusini zimetangaza kusitishwa kwa mapigano,baada ya kuwepo kwa siku kaadhaa za machafuko mjini Juba zilizosababisha vifo vya mamia ya watu.

Mapigano baina ya majeshi yanayomtii Rais Salva Kiir na yale yanayoongozwa na Makamu wa Rais wa kwanza Riek Machar yanatishia kuharibu mkataba wa amani uliosainiwa mwaka jana kumaliza miaka miwili ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Machar ameiambia BBC machafuko ya hivi karibuni yamesababishwa na watu wasiotaka kuona amani ikiwepo nchini humo.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon ametoa wito wa kuimarishwakwa ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini.

Chanzo: BBC
 
Back
Top Bottom