Mapigano dhidi yako mwenyewe ๐Ÿ’ช

Umewaza nini dear.๐Ÿ˜๐Ÿ˜

Nimepigana aina hii ya vita.
Nahisi nimeshinda vita japo adui yangu kumuua kabisa nahisi haiwezekani ila hanisumbui baada ya kujua kinachompa nguvu na ninahakikisha hakipati.
 
Mapambano magumu zaidi huwa yapo kichwani, adui mkubwa wa mtu ni yale mazoea aliyoyahalalisha kwa miaka mingi.

Kuna kipindi niligundua kuwa watu wengi huwa wanatumia nguvu nyingi sana kupambana na wengine, lakini wanashindwa kupambana na nafsi zao wenyewe, mfano rahisi, kila siku mtu anasema anataka kufanikiwa lakini kila kukicha anapoteza masaa mengi kufuatilia maisha ya watu wengine, nani kaingia online, nani katoka, nani kamjibu nani, hii ni silent addiction mbaya sana, unakuwa mtu wa kujenga maisha ya wengine kichwani kwako huku ya kwako yakiwa hayaeleweki zaidi.

Mapigano dhidi yako mwenyewe ni maamuzi unayoyafanya kila siku hata pale ambapo hakuna yeyote anayekuona, discipline is choosing what you want most over what you want now.

Kuna msemo unasema, until you conquer yourself, every other victory is temporary, unaweza ukawashinda watu kwenye mabishano, ukaonekana mjanja, lakini kuna vitu vidogo tu kukuhusu vikakushinda mfano kushindwa kudhibiti hasira yako, kushindwa kudhibiti matumizi mabaya ya fedha n.k

Kwa mtazamo wangu, ushindi wa kweli unapimwa kwa ile idadi ya tabia mbaya ulizoweza kuzizuia ndani yako, mtu anayejitawala ni hatari mno kuliko anayewatawala wengine, kwa sababu hakuna yeyote anayeweza kumzuia kufika popote anapotaka.

Ukiweza kuzishinda tabia ambazo zinakurudisha nyuma mara kwa mara,dunia itakuwa na kazi ngumu sana kukushinda.
 
Mi napigana sana njaaa mpaka tumbo linatahamaki

Sawa umesema unatupenda wote je zamu yangu itakua lini tukutane?๐Ÿ˜
 
Umewaza nini dear.๐Ÿ˜๐Ÿ˜
Babe ni wazo tu limekuja
lakini pia nimewahi kupigana pia dhidi yangu mwenyewe na kuibuka mshindi
Nimepigana aina hii ya vita.
Nahisi nimeshinda vita japo adui yangu kumuua kabisa nahisi haiwezekani ila hanisumbui baada ya kujua kinachompa nguvu na ninahakikisha hakipati.
Baada ya kundua aina ya silaha anayotumia adui yako dhidi yako huo ndio ushindi kamili

Na unamuacha adui ajifie mwenyewe kwa kumfanya akose target zake kwako maana tayari unafahamu silaha yake na mapigo yake

Hongera karibu tena๐Ÿ˜Š
 
Hongera kwa ushindi.๐Ÿ’ช

Adui wangu nimezaliwa nae kujifia labda sayansi iniunge mkono ila so far so better.Hana nguvu.Yupo coma,ni nusu mfu๐Ÿ™ƒ.Kazi yangu kuhakikisha hazinduki.
 
I have fallen in love with your writing skills.
 
Unaambiwa una mapigano yako binafsi unataka kupigana na mimi, hem kwanza pigana na huyo aliyeko kwa bongo yako, mimi tutapigana ukishapata mshindi huko.
Mi nawaangalia tu ๐Ÿ˜
 
Mapambano magumu zaidi huwa yapo kichwani, adui mkubwa wa mtu ni yale mazoea aliyoyahalalisha kwa miaka mingi.
Ni kweli naunga mkono
๐Ÿ’ฏ๐Ÿ’ฏ๐Ÿ’ฏ๐Ÿ’ฏ
Mapigano dhidi yako mwenyewe ni maamuzi unayoyafanya kila siku hata pale ambapo hakuna yeyote anayekuona, discipline is choosing what you want most over what you want now.
Hakika
Nakubari The Thinker
Kwa mtazamo wangu, ushindi wa kweli unapimwa kwa ile idadi ya tabia mbaya ulizoweza kuzizuia ndani yako, mtu anayejitawala ni hatari mno kuliko anayewatawala wengine, kwa sababu hakuna yeyote anayeweza kumzuia kufika popote anapotaka.
โค๏ธ
Ukiweza kuzishinda tabia ambazo zinakurudisha nyuma mara kwa mara,dunia itakuwa na kazi ngumu sana kukushinda.
The Thinker ๐Ÿ“Œ
 
Vita ya ndani ni ile unajua unapaswa kufanya nini lakini unaogopa watakuonaje.

Wengi hawana filter ya kujua nini wanahitaji, wanafwata maneno ya viumbe wengine wanaishia kuwa ma zombie tu humu duniani

It's funny but true. Kama unajua wewe ni nani basi vita umeishinda nusu ila kulifanya lile unalotaka ndo mtihani thabiti
 
Mimi nilikuwa napigana na tabia ya pombe,Nina mwezi nimeishinda yaani nilikuwa Niko radhi nishinde na Njaa ili nibugie konyagi, Mungu Mwema nimeishinda Mwenyewe!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ