Mapichapicha ya CUF Tanganyika (Mungiki)

Mapichapicha ya CUF Tanganyika (Mungiki)

Sudysoko

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2015
Posts
449
Reaction score
180
Yaliyoandikwa na Abdul Kambaya aliyekuwa naibu mkurugenzi wa Habari na Uenezi cuf leo mtandaoni(FB)

"SIJAMBO GENI, HATA FIRAUN ALIPOSHINDWA KUJIBU HOJA ZA MUSSA ALITUMIA JESHI

Nimekua napigiwa simu nyingi toka kwa Wanachama wenzangu na Waandishi wa habari kuhusu Taarifa zilizozagaa kwenye Mitandao. Majibu yangu ya awali Kuhusu Taarifa hizo ni

1 Moja Baraza Kuu lina Mamlaka ya kufanya hivyo kwa mujibu wa Katiba na kwa kwa kufuata Katiba jinsi inavyoeleza kwenye hizo taratibu za kuchukua hatua za Kinidhamu.

2 Mimi na wenzangu tunaotajwa kwenye kadhia hiyo ikiwa ni Pamoja na Wabunge wa Mtwara Mjini (Maftaha Nachuma) na Magdalena Sakaya Mbunge wa Jimbo la Kaliua na Diwani wa Kata ya Misima Wilayani Handeni,pamoja na wale ambao sikuwataja hatukuwepo wakati hukumu hiyo inatolewa na Baraza Kuu lilofanyika jana Mjini Unguja katika Visiwa vya Zanzibar.

3 Baada ya kuahirishwa kwa Mkutano Mkuu uliofanyika pale Ubungo Plaza Tarehe 21 /08 /2016 kutokana na Wajumbe 324 kutoridhishwa na ukiukwaji wa Katiba ya Chama chetu ikiwa ni pamoja na kuingizwa kwa Wajumbe wasio halali kwenye Mkutano Mkuu, mimi ni miongoni mwa Wajumbe tuliojiorodhesha na kuandika barua ya Malalamiko na kupeleka Ofisi ya Msajili wa Vyama.

Kutokana na Mambo hayo Matatu, nawaomba Wanacuf msifadhahike na wala msihuzunike waliotufukuza kabla hata ya kutoa majibu ya hoja zetu tulizowasilisha kwa Msajili, bila shaka hawana Majibu ya sahihi ya hoja zetu. Na jambo hili sio geni kwa hapa Duaniani, Firaun aliposhindwa kuthibitisha kua yeye ndie Mungu, alitumia Jeshi lake (Baraza Kuu) kutaka kumuangamiza Mussa na Wafuasi wake waliokua wanaamini katika Haki na Mungu wa kweli.

Kilichoendelea Zanzibar ni Mfano wa Firaun na Jeshi lake dhidi ya Mussa na Wafuasi wake.

Kauli yangu ya Mwisho ni kwamba hatoki mtu kwenye Cuf hii kwakua sio ya Mtu bali ni ya watu, sijambo jema kujifananisha na Firaun, jibu hoja usitumie Jeshi kujibu hoja. Hakuna kukataa Tamaa wala kukimbia Cuf. Harakati za kutafuta Uhuru ndani ya Cuf kwa Watanganyika ndio kwanza umezifungulia Geti, sasa ni hoja za Makabwela dhidi ya Vibaraka wa Mabepari wa Tanganyika."

Je?Kama Mussa ni Prof. Lipumba na Firauni ni Nani!
'Hakika Mfa Maji Aishi Kutapatapa......'
 
Kumbe huyu Kijana na mimi sikujua, yaani na yeye amepewa hela na kukubali kutumiwa?,
 
Hana akili huyu,anampigania Lipumba alieondoka CAF kwa akili zake timamu,watu wengine bure kabisa
Hee Hee hee mtaji wake wa Usaliti haukumlipa vizuri sasa ameamua kuja na mbinu mpya ya kung'ang'ania chama
 
Hovyo kabisa. Lupumba alikiacha chama kwa ajili ya chumia tumbo. Tena ikiwa ni wakati mgumu wapinzani wakijipanga. Arudi kule alikokimbilia kujificha akila kuku kwa mrija wakati wenzao wakipigania uchaguzi.
 
Vijana punguzeni kutumika,dhambi ya Usaliti ni kubwa inayoweza kukutia Aibu na ukaonekana wa ovyo Katika jamii
 
1472454777681.jpg

Maelezo yake yamenikanganya kidogo. Kwanza anakiri kwamba Baraza Kuu la CUF linayo hayo mamlaka ya kuwatimua chamani, lakini mwisho anadai "hatoki mtu CUF" halafu anakoleza kibwagizo chake kwa kuandika "Sasa ni hoja za mkabwela, dhidi ya vibaraka wa mabepari wa Tanganyika".

Tuliambiwa kwamba tatizo ni CUF Zanzibar kutowasikiliza wenzao wa Tanganyika, kuwaita watanganyika wenzako ni vibaraka wa mabepari wa Tanganyika, unaleta utata. Maana kama ungeandika ni vibaraka wa mabepari wa Zanzibar ingekuwa na maana, ama tuambiwe kwamba hata wao wa Tanganyika wamegawanyika kati ya hao "Makabwela" na "Vibaraka wa mabepari".Chama ambacho enzi za Lipumba kilikuwa kinahubiri sera za utajirisho kinakuwaje tena na chuki na Mabepari?
 
Hivi kama CUF ingeambulia Mbunge mmoja au wawili baada ya kuondoka Lipumba jee Lipumba angetumia hizi mbinu kutaka kurudi?
Lipumba alifanya jambo la kisaliti na kijinga sana na hao wanaomuunga mkono sasa kuwa arudi ndio wajinga zaidi. Hayo ya Uzanzibar na utanganyika ni propaganda tuu, mbona hawakusema kabla hajaondoka?
 
Tatizo dhambi ya Usaliti inamtafuna LIPUMBA na timu yake(Kambaya,sakaya +mungiki)waliyoifanya wakati wa kampeni Mwaka Jana.
 
Hivi kama CUF ingeambulia Mbunge mmoja au wawili baada ya kuondoka Lipumba jee Lipumba angetumia hizi mbinu kutaka kurudi?
Lipumba alifanya jambo la kisaliti na kijinga sana na hao wanaomuunga mkono sasa kuwa arudi ndio wajinga zaidi. Hayo ya Uzanzibar na utanganyika ni propaganda tuu, mbona hawakusema kabla hajaondoka?
Nimekuelewa Sana.....
 
Hana akili huyu,anampigania Lipumba alieondoka CAF kwa akili zake timamu,watu wengine bure kabisa
Tatizo watu wanaingia kwenye vyama hivi vya siasa bila ya kuangalia Katiba za vyama hivyo zinasemaje. Kwanza kwenye CUF Zanzibar ina uwakilishi sawa kwenye vikao na Tanganyika, kwa ivo si rahisi kukwamisha mambo yao kama wanayataka kwani siku zote Akidi itatimia tu. Halafu wajumbe wengi wa Tanganyika ni wa kuokkoteza mitaani wengi wao hawatoke kwenye hiyo mikoa wala Wilaya wanazodai wanaziwakilisha.
 
Hivi mtu ukiandika barua ya kuacha kazi ukakubaliwa kuacha kazi kazini kwako baada ya kwenda mtaani ukaona maisha sio ukajutia uwamuzi wako ukataka kurudi kwenye ofisi yako kwann usifate taratibu utalazimishaje urudie kwenye kiti ulichokikalia, kwann asifate taribu kama anajiami anauwezo mkuwa si angechukua fomu za kugombea anagombea nafasi yake kujitetea. binafsi naona Prof hatumii vizuri akili zake na uprofesa wake aliomba kuachia madaraka mwenye kwasababu anazozijua na akasema atabakia mwanachama wa kawaida sawa, fata basi sheria za chama chako kwa kuchukua fomu na kugombea tena au ulizuiwa kuchukua fomu, kwani chama ni chake useme baba alikwenda kwa mchepuko now anarudi nyumbani anarejea kwenye nafasi yake ya ubaba.
Mambo mengine naona ni ujinga tu wa kuvuruga kwa maksudi angefata taratibu sidhani kama wangekuwa na malumbano kambi ya prof wanasema maalim anafanya chama kama mali yake na wa maalim wakisema prof anafanya chama kama maliake nani ataonekama mkweli.

Acheni kuvuruga watu.....
 
Hovyo kabisa. Lupumba alikiacha chama kwa ajili ya chumia tumbo. Tena ikiwa ni wakati mgumu wapinzani wakijipanga. Arudi kule alikokimbilia kujificha akila kuku kwa mrija wakati wenzao wakipigania uchaguzi.
Aliaidiwa fungu kubwa akapewa advance akajiuzulu ili watu washinde nyingine hakumaliziwa na kudai hawezi kwa kuwa hakuna maandishi hivyo anataka kurudi nafasi yake ili ajikimu kimaisha njaa jamani tuseme nayo
 
Back
Top Bottom