Mapenzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mapenzi

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by happy lusajo, Oct 17, 2012.

 1. h

  happy lusajo New Member

  #1
  Oct 17, 2012
  Joined: Oct 17, 2012
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani naombeni ushauli wenu , wanawake kwa wanaume, Mimi nina mchumba wangu ambaye tunatarajia kufunga ndoa mwezi wa kumi na moja ktk mkoa wa Morogoro, sasa uyu mwanaume sasaiv amekuwa mkali kila nikimuuliza labda uko wap ananiambia kwan lazma nijue, akiwa na wenzie ananikatia cm anasema alikuwa anaongea na marafiki zake,amekuwa ni mtu w kufoka kila wkt,akinikosea hata msamaha aniombi, na ndio tunakalibia kufunga ndoa, nifanyeje wapendwa
   
 2. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #2
  Oct 17, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Kabla hatujaenda mbali Happy... Ni vigezo gani unatumia kusema ni mchumba? Alishakwambia kuwa mahusiano yenu ni uchumba ama tu ushiriki? ama ni wewe uliechukulia kuwa ni mchumba... Kama hutajali huo uchumba alitamka kabla ama baada ya nyie kukutana kimwili (for nachukulia kuwa tayari mshapita huko...)

  Hii inaweza toa picha walau kama anakupotezea wakati ama ni phase tu anapita ijulikanayo kama 'rut stage'
   
 3. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #3
  Oct 17, 2012
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Pole sana Happy hilo ni Tatizo.....Jibu maswali ya AshaDii kwanza ili tujue pa kuanzia
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #4
  Oct 17, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  dalili ya mvua ni mawingu lol
   
 5. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #5
  Oct 17, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 14,175
  Likes Received: 2,136
  Trophy Points: 280
  ASHA dii,happy anafunhga ndoa mwezi wa kumi na moja hebu msome vizuri tena!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #6
  Oct 17, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 14,175
  Likes Received: 2,136
  Trophy Points: 280
  mh!
  nahisi kuna kitu hakio sawa hapa !lakini pengine amepata a second thought ,hili la migogoro kuibuka kipindi cha kukaribia ndoa hili nalo ni very common i see!sijui huwa ni kktu gani kwa kweli!
   
 7. m

  mzabzab JF-Expert Member

  #7
  Oct 17, 2012
  Joined: Aug 18, 2011
  Messages: 6,981
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  kha! pole sana happy ila inaonekana kabisa that guy arent ready for marriage kabisa. nasema hivyo kwa sababu ukiamua kuoa lazima ukubali freedom yako itapungua na mke ana kila haki ya kujua upo wapi na unfanya nini. this is just basic nashangaa sana wanaume wanamaindi mke/fiance/gf kuuliza upo wapi na unafanya nini
   
 8. mdida

  mdida JF-Expert Member

  #8
  Oct 17, 2012
  Joined: Jul 14, 2011
  Messages: 1,608
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Duh uchumba mwingine labda umemlazimisha muoane sasa anataka akulidhishe afu akuache, haiwezekani mtu kuchange ghafla kama milikuwa mnapendana hapo awali, au jiangalie labda umemkosea.
   
 9. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #9
  Oct 17, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180

  Asante Snowhite, nikiri nilimsoma kuwa wanakaribia kuoana ila sikumsoma kuwa ni mwezi wa 11... Hapa kaazi kweli kweli...

  Kwa mukatadha huo naweza sema haya... KAMA KWELI mmeshafanya process zote za Kutambulisha na tayari mpo katika harakati za maandalizi then hapo sio tatizo sana, inaweza tu kuwa mwanaume yupo katika phase ya woga wa kujiuliza kama anafanya the right thing.. Huo woga unaweza ukawa umesababishwa na kusongwa, kujazwa maneno ama yeye mwenyewe.

  Kama hapo nyuma hakuwahi fanya hivo there is hope kuwa atarudi katika hali yake, kikubwa umvumilie na kujaribu kumsoma hasa nini anachojaribu ku prove badala ya kuchukua maamuzi ya haraka. Hata hivo kukatiwa simu na mpenzi wako ni kitendo kikubwa sana na cha kukemea kabisaa... Kwa kweli onesha msimamo wako else atakuchezea sana.
   
 10. Edgartz

  Edgartz JF-Expert Member

  #10
  Oct 17, 2012
  Joined: Feb 26, 2010
  Messages: 241
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Yote uliza ila swali linaloboa kuliko yote unafanya nini m2 kakuuliza uko wapi umejibu swali lingine unafanya nini hapo me ndo uwa nauzika kinoma
   
 11. Joseph

  Joseph JF-Expert Member

  #11
  Oct 17, 2012
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 3,527
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Leo nitatoa ushauri tofauti na kawaida yangu,unajua siku hizi maisha yamebadilika sana kiasi kwamba kila mtu anajaribu kuhangaika kwa namna anavyojua mwenyewe ili mradi mwisho wa siku maendeleo yanapatikana katika familia husika au jamii husika.

  Mtoa mada ametuambia mchumba wake amekuwa mkali,hebu jiulize ukali unatokana na nini?
  Anasema kuwa akimpigia simu akiwa na marafiki zake anamkatia,mtoa mada hujatuambia kabla ya hapo ilikuaje?

  Pia ukiuliza swali la yupo wapi anakujibu hpaswi kujua,tuambie maisha yenu ya kimapenzi yapoje maana inawezekana tangu mwanzo hukuwa unamuuliza maswali hayo.

  Wachumba wengi wanapopata nafasi ya kuelekea kwenye ndoa hubadilika na kuvaa tabia ambazo wakati wa urafiki huwezi kukutana nazo,mfano kama mwanaume alikuwa hamfuatilii mwenza wake basi kipindi hiki ndio anataka kuonesha yeye ni nani kwake,vivo hivyo kwa mwanamke nae anataka kujua kila anachofanya mpenzi wake kiasi kwamba ule mfumo mzima wa maisha ambayo walikuwa wanaishi kabla unabadilika na inaonekana mahusiano yanayumba kwani kila mmoja anaona mambo mapya toka kwa mwenza wake.

  Ushauri wangu ni kuwa rudini kwenye maisha yenu ya kawaida na kufunga ndoa isiwe kigezo cha kubadilika na kuacha maisha yenu ya kimapenzi mliyoyazoea kubadilika,ukiona kipele kinawasha kikune,ukikikuna sana ujue kitatoa damu lakini unaweza usifike huko na kipele kikaisha bila matatizo.
   
 12. Mu-Israeli

  Mu-Israeli JF-Expert Member

  #12
  Oct 17, 2012
  Joined: Mar 21, 2012
  Messages: 2,456
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 160
  Angalia sana hapo kwenye blue,
  Huyo mchumba wako atakuwa amefuata ushauri potofu hapa JF kama huo hapo kwenye red !!!
  Hapa JF kuna kila aina ya 'ushauri' !!
   
 13. Autorun

  Autorun JF-Expert Member

  #13
  Oct 17, 2012
  Joined: Mar 21, 2008
  Messages: 556
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Fanya kupost pon tukio uone responce yake iko vip kwa uamuzi wako huo
   
 14. h

  happy lusajo New Member

  #14
  Oct 17, 2012
  Joined: Oct 17, 2012
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Asanten kwa Ushauli, nasema mchumba wangu ,kwanza ameshatoa mahali,na pili ndoa yetu ni tarehe 20 November natayali vikao vinakaliwa, Zamani ktk uchumba wetu alikuwa anapenda tuchati kila wkt kwa njia ya msg, na ukikaa kimya kidog anakuuliza mbona kimya unafanya nn,au akipiga sim ikiita mala mbili,na mimi nikija kupiga anaiacha kama vile makusudi mpk niangaike wee ndio anapokea, lkn saivi nikimpigia simu wkt mwingine inaita sana ,kama hata mala4 ,akija kupokea nikimuuliza mbona cm inaitasana anasema alikuwa na washkaj kunavitu walikuwa wakiongea, wkt uo mimi akinipigia cm labda bahat mbaya nilikuwa mbali nayo,anaanza kunigombeza ,na hata wkt mwingine akinipigia cm akikuta cm yangu inatumika anaanza kunifokea ulikuwa unaongea n nani wkt mimi nilikuwa napiga cm,nikimwambia labda nilikuwa naongea na rafik yangu anasema kwahiyo rfk yako bola kuliko mmi, wakati mimi nikimuuliza ivyo anajibu tu nilikuwa naongea na mtu asemi nani
   
 15. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #15
  Oct 17, 2012
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  je huoni dalili za ndoa kusitishwa?
  Kama hazipo basi labda mambo ya fedha yanamchanganya na mengineyo
  kama ujuavyo pesa ilivyo ngumu sasa na ni jukumu lake kufanikisha kila kitu ..labda kapanic na harusi
  Hebu chunguza mwaya
   
 16. nyaucho

  nyaucho Member

  #16
  Oct 17, 2012
  Joined: Apr 24, 2011
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Pengine jamaa anakupima kwanza, jaribu kuchunguza ujue tatizo liko wapi kabla hujafanya uamuzi mwingine.
   
 17. charger

  charger JF-Expert Member

  #17
  Oct 17, 2012
  Joined: Nov 21, 2010
  Messages: 2,327
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Unaegemea mlango wa jela ndugu,ukifunguka tu upo ndani halafu jina lako lina change unaanza na UN.......
   
 18. JICHO LA TATU

  JICHO LA TATU JF-Expert Member

  #18
  Oct 18, 2012
  Joined: Sep 28, 2012
  Messages: 307
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Eeeeeeeeeeh dada piga maombi Shetani kisha ingilia kati hivyo siyo bure
   
 19. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #19
  Oct 19, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,754
  Likes Received: 82,698
  Trophy Points: 280
  Haya uliyaandika ndio inastahili kuwa hivi kwa wachumba ambao wanakaribia kufunga pingu za maisha. Tafuta nafasi umueleze kwamba mabadiliko yake kitabia kama ulivyoandika hapo juu huyapendi kabisa na yanakupa wasiwasi mkubwa hasa ukitilia maanani umebaki mwezi tu kabla ya kufunga pingu za maisha. Kama maelezo yako hayatakuridhisha basi sitisha vikao vya harusi na uwaeleze wahusika wa pande zote mbili sababu zako za kuamua kufanya hivyo kuliko kujiingiza kwenye ndoa ambayo ina kila dalili kwamba haitakuwa ndoa nzuri.

   
 20. Catherine

  Catherine JF-Expert Member

  #20
  Oct 19, 2012
  Joined: Jun 30, 2012
  Messages: 1,263
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  umeona eeh! Abebe mwamvuli kabisa. Lol.
  Mi namshauri ajaribu kumrekebisha hivyo vitabia vipya akishindwa akimbie mapema au akubali kuolewa ila awe tayari kwa vimbwanga mbele ya safari.
   
Loading...