ACHINJEMERE
Member
- Oct 19, 2014
- 42
- 19
Wengi ni wagonjwa WA akili wanaojiua kwenye mapenzi!
Mpaka kanikata pozi la masikitiko.........sijui hata nilikuwa nataka kusema nini..........
Najua mapenzi yanauma ila kwa kweli huwa nawashangaa sana watu wanajitoa uhai kwa ajili ya maumivu.
elewa mada kabla ya kuamua ujibu nini? hapa nimeripoti tukio, na nimeongelea watu watatu tu hapaa, mwanamke(aliyekunywa sumu),mwanaume(aliyesaliti) na mtoto(aliyefiwa mama yake akiwa mdogo sana kisa usaliti wa baba yake)
hii mada sikuwa nawaongelewa wanaume.
na mwisho nikatoa ushauri kuwa wanaochepuka wapunguze kama si kuacha {huu ushauri ndio general kwa team mchepuko bila kujali jinsia }
from messages of my phone
" mida mida tu kuna mdada hapa jirani kafa kanywa sumu, kafunga harusi mwaka Jana mwezi wa saba na ameacha mtoto mdogo sana, haya yote yanasabishwa mapenzi."
taarifa zimeeleza huyo mwanamke kasalitiwa na mume wake na akaamua kujiua mapema leo huko ARACHUGA.
nyinyi wazee wa michepuko punguzeni kama siyo kuacha, sasa huyu mtoto mdogo atakikua atakuwa anamuonaje baba yake akijua usaliti wa baba yake ndio ulipelekea kifo cha mama yake?
inauma sana japo simfahamu aliyefariki.