Mapenzi, yapo kweli? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mapenzi, yapo kweli?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by TANMO, Jan 19, 2010.

 1. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #1
  Jan 19, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,868
  Likes Received: 156
  Trophy Points: 160
  Wanajamii kwa mtazamo wangu nimeona kuwa mapenzi kwa sasa yanachanganya sana kiasi kwamba mtu ukifikiria sana unaweza kuibuka na uamuzi kuwa ni bora usijiingize kabisa kwenye huo ulimwengu wa kimapenzi. Utamkuta mwanadada ana mtu ambaye anampenda sana (siku hizi inasemwa anam-feel) huyo ndiye anakuwa dream husband wake wakati huo huo pembeni kuna kibosile anayemtatulia matatizo yake ya kiuchumi, pembeni tena kuna mwingine ambaye anamfikisha vyema kwenye tendo (kwa mujibu wao) wengine wanadiriki humu jamvini kusema kuwa wanapenda kujiexpress lakini si na waume zao (wapo wanaosaidia) n.k n.k n.k……

  Tukija kwa upande wa wanaume, utakuta kuna mwanadada ambaye anakuwa anam-feel kiasi cha kumchukulia kama wife wake (kama hawajaoana). Wakati huo huo kuna mwingine kwa ajili ya kumpatia huduma ya mtandao (Wasiliana na Chrispin au Fidel kama hujui hii ni nini) wakati huo huo naye anataka aukemee uzee (kwa mujibu wa Annina), miongoni mwa tetezi wanazotumia mabinti wanaoamua kujiingiza kwenye usagaji ni pamoja na wanaume kutokujali hisia zao, kutokuwa waaminifu, kutowaridhisha vyema kwenye tendo (kwa mujibu wa maelezo niliyopata kwa baadhi yao) n.k n.k n.k…..

  Kwa hali hii, wanajamii wenzangu, tunaelekea wapi hasa? Na ni upi mtazamo wako kama mwanajamii mwenzangu, nini hasa kifanyike ili kunusuru kizazi kijacho?
  Jiulize...............................................
   
 2. arnolds

  arnolds Senior Member

  #2
  Jan 19, 2010
  Joined: Oct 10, 2009
  Messages: 105
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  kweli ndugu hyo ishu imekua very serious, cha ajabu ni kwamba inachukuliwa kama kitu cha kawaida kabisa! Huku ni kujidhalilisha ndugu zangu, na ni mwanzo wa kueneza magonjwa hatari kama ukimwi..kwa mtazamo wangu naona hapa hakuna mapenzi bali ni tamaa tu! mapenzi na ngono ni vitu viwili tofauti kabisa..Tunahitaji kubadilika na kujiheshimu, pia kuwaheshimu wapendwa wetu kwa kuwa waaminifu na kuji commit kiukweli!!

  amani kwenu.
   
 3. Masaki

  Masaki JF-Expert Member

  #3
  Jan 19, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,465
  Likes Received: 162
  Trophy Points: 160
  Wapo wanaume na wanawake ambao wana ''full package'' ya hizo sababu zinazopelekea watu kuna mpenzi zaidi ya mmoja! Ukimpata huyo mambo tamabarare. Lakini haina maana kwamba usimpopata huyo basi uendekeze vijisababu visivyokuwa na msingi ili ku-justify cheating!
   
 4. arnolds

  arnolds Senior Member

  #4
  Jan 19, 2010
  Joined: Oct 10, 2009
  Messages: 105
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  seriously, kama unaelewa thamani ya utu wako huwezi fanya huu upumbavu!!
   
 5. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #5
  Jan 19, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  mapenzi yapo bwana mkubwa!
  unayoyajadili ni ''human weaknesses''
   
 6. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #6
  Jan 19, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,564
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  jamani tusidanganyane hizi ni siku za mwisho watuwataka tamaa za kila aina wabinafsi wenyekupenda kupenda pesa na mengine mengi ila ktk hayo yote wapo wenye mapenzi ya kweli na ya dhati kabisa na zaidi wenye hofu ya mungu
   
 7. Shagiguku

  Shagiguku JF-Expert Member

  #7
  Jan 19, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 401
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 45

  ni kweli nakubaliana na wewe kuwa mapenzi ya kweli yapo tena wakinadada ndo wanaoweza kuonesha mapenzi ya kweli.
  sisi wanaume mara nyingi huwa tunaonesha mapenzi ya kutamani, wanume tunapenda kutokea mdomoni lakini wanawake wanapenda kutokea moyoni.
  REMEMBER: When a Woman is walking, She always walk to Communicate...!!!

  But when a Man is walking He walks juSt to COVER a Distance...!!!
   
 8. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #8
  Jan 19, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  ....mmh!
   
Loading...