Mapenzi Yanapozidi.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mapenzi Yanapozidi..

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by MziziMkavu, Jun 4, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 4, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  :eyeroll2:
  [​IMG]
  Thursday, June 03, 2010 9:08 PM
  Mwanaume mmoja wa nchini Uingereza kwa uchungu aliokuwa nao wa kuondokewa na mpenzi wake, aliamua kuishi na maiti ya mpenzi wake ndani ya nyumba yake akiimwagia pafyumu nyingi sana ili kuzuia harufu isitoke nje. Gabriel Brown, 54, aliishi na maiti ya mpenzi wake akiiweka kwenye kochi na kuyanyunyuzia pafyumu mabaki yake ya mwili wake ambao uliendelea kuoza ili kuzuia harufu isitoke nje ya nyumba yake.

  Gabriel aliishi hivyo kwa takribani miezi 10 hadi alipotiwa mbaroni mwezi disemba mwaka jana baada ya maiti ya mpenzi wake Lynn Warman, 37, ilipokutwa kwenye kochi nyumbani kwake ikiwa imezungukwa na makopo ya pafyumu.

  Brown aliwaambia polisi kuwa mpenzi wake alifariki februari 9, 2009 lakini kutokana na majonzi aliyokuwa nayo hakutaka kutoa taarifa polisi.

  Brown alishikiliwa na polisi kama mtuhumiwa wa kifo cha mpenzi wake lakini aliachiwa kwa dhamana wakati polisi wakiendelea na uchunguzi.

  Wakati polisi wakiendelea na uchunguzi kutafuta ukweli wa kifo cha mpenzi wake, Brown naye alikutwa amefariki baada ya kupoteza damu nyingi wakati alipopata ajali.

  Uchunguzi wa maiti ya Lynn ulionyesha kuwa hakuuliwa na alifariki akiwa amekaa kwenye kochi ambalo maiti yake ilikutwa.

  Mmoja wa majirani zake alisema: "Brown na Lynn walikuwa wakipendana sana, inasikitisha kusikia kwamba maiti ya Lynn ililala kwenye kochi karibia mwaka huku Brown akiishi nyumba hiyo hiyo".

  "Sijui aliwezaje kuishi kwenye harufu mbaya ya maiti iliyoharibika, Natumaini watapumzika kwa amani huko waliko", aliongeza kusema jirani huyo.
   
 2. JS

  JS JF-Expert Member

  #2
  Jun 4, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 2,065
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kaazi kwelikweli
   
 3. ngonzi zomukama

  ngonzi zomukama Senior Member

  #3
  Jun 4, 2010
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 170
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Duh! hayo ni mapenzi ya dhait kweli
   
 4. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #4
  Jun 4, 2010
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Love is blind....
  For Real....
   
 5. P

  Pierre III Member

  #5
  Jun 4, 2010
  Joined: Jun 1, 2010
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dhuu! ndo kufa na kuzikana
   
Loading...