Mapenzi yananiua

Long'ututi

Member
Dec 5, 2010
41
4
Ndugu zangu,naombeni ushauri,kweli nakiri nimekosea. Suala langu lipo hivi,mimi nilizaa na mwanamke mmoja japo sikumpenda kwani nilijipa moyo nampenda kumbe ilikuwa si kweli kwani nilikutana naye nikiwa na wawazo mengi kutokana na kuachana na mpenzi wangu wa kabla yake,niliyezaa naye huyu tuna uhusiano wa mwaka na zaidi hivi,akiwa mjamzito nikapata mwanamke niliyempenda kwa dhati,kutokana na ujana nikamvisha pete ya uchumba, naye nipo naye kwenye uhusiano yapata miezi tisa sasa,wote wanajuana na hakuna anayekubali kuachana nami,mwenye mtoto hakubali na mwenye pete anasema hawezi kubaki na pete,ndugu zake na jamaa washajua namuoa. Wote wanataka kutumia nguvu hadi za jadi nisimwache hata mmoja na najua ipo siku mambo yatakuwa makubwa sana na wote wanipenda kwa dhati japo mimi toka moyoni nampenda niliyemvisha pete ila mara zote namfikiria mwanangu ataishije bila baba? naombeni ushauri,mimi ni mkristo siwezi kuoa wake wawili,nipo tayari kurudi kwa mwenye mtoto ili niilee familia yangu ila mwenye pete naye hakubali,nifanyeje ndugu zangu?
 
Oa wote wawili

tafsiri ya ndoa ni kubwa kuliko harusi
mpaka hapo wewe una wake wawili
na hata ukimuoa huyo wa pete,na huku unamtunza
aliekuzalia mtoto,itakuwa sawa na kuwa na wake wawili...

Sio watu wote wanaoitwa mke na mume
wamefunga ndoa kanisani
 
Pole sana. Mimi ushauri wangu umuoe yule ambaye unampenda. Kama unayempenda zaidi ni huyo uliyemvisha pete basi umchukue mtoto ili umlee wewe na mke mtarajiwa kama yupo tayari kumlea huyo mtoto bila pingamizi lolote. Kama mwenye mtoto hataki basi uwe una peleka pesa za matunzo na pia kumchukua mtoto kwa siku chache kila wiki ili nawe umlee tangu akiwa mdogo hata kama ni kwa hizo siku chache kila wiki.
 
Kufa hufi ila cha moto utakiona, angalia moyo wako ndugu, huna haja ya kuoa sababu ya kumuonea mtu yeyote huruma, ila jiulize sana sana kama unampenda mpenzi wako wa sasa, huwezi jua nae labda ulimpenda kuwa nae baada ya huyo mwingine kuwa tu mjamzito.... uamuzi ni wako, fanya haraka kabla hujachelewa, mtoto unaweza mpa matunzo mazuri tu akiwa hata kwa mama yake
 
Mhhhhhhhhhhhhhh!!!!!!
 
Long'ututi, mimi nashangaa unaposema unalazimishwa. Ndoa hailazimishwi ni hiari yako. Hakuna mtu ambaye anatakiwa ku-control maisha yako ila ni wewe mwenyewe. Hakuna anayeweza lazimisha kuoa mke ila ni wewe mwenyewe, sio baba, mama, uchawi, mahakama etc.. Kitu ambacho sheria itachukua mkondo wake ni matunzo ya huyo mtoto asiye na hatia.

Tafuta suluhu na mama wa huyo mtoto. Lazima umtunze hata kama utaoa mara 100. Kosa si kufanya kosa ila kurudia kosa.
 
umekoroga mwenyewe kunywa,
kwanini lakini eti humpendi huyo uliyempa mimba na hapo nikisoma vizuri inaonyesha hao watu wote umekuwa na uhusiano noa within one year,
just image ni maumivu ya kiasi gani umemsababishia huyo dada mjamzito na ni jinsi gani unavyo utesa moyo wa uliyemvisha pete?
umefanya jambo lisilojema hata kidogo ,hakuna mwanamke anayependa kuzaa bila kuishi na family together(baba na mtotowe)
Mie hata sikuonei huruma wacha wote wakunganganie ili wengine wajifunze matumizi ya kinga kama huna malengo ya kuzaa.
 
mambo ya jadi tena? and u still wanna keep being involved? kweli ndo maana ww ni ww na mm ni mie!
 
Oa wote wawilitafsiri ya ndoa ni kubwa kuliko harusimpaka hapo wewe una wake wawilina hata ukimuoa huyo wa pete,na huku unamtunzaaliekuzalia mtoto,itakuwa sawa na kuwa na wake wawili...Sio watu wote wanaoitwa mke na mumewamefunga ndoa kanisani
nimekuelewa ndugu yangu. Ila kuwa na wake wawili tena kisheria kiukweli siwezi,niliteleza tu ndugu yangu.
 
Pole sana. Mimi ushauri wangu umuoe yule ambaye unampenda. Kama unayempenda zaidi ni huyo uliyemvisha pete basi umchukue mtoto ili umlee wewe na mke mtarajiwa kama yupo tayari kumlea huyo mtoto bila pingamizi lolote. Kama mwenye mtoto hataki basi uwe una peleka pesa za matunzo na pia kumchukua mtoto kwa siku chache kila wiki ili nawe umlee tangu akiwa mdogo hata kama ni kwa hizo siku chache kila wiki.
nashukuru sana ndugu yangu,matunzo mpaka sasa napeleka,ila kwa siri kwani kati yao hakuna aneyejua kipato changu halisi kwa mwezi,namudu gharama ila niliyemvisha pete yeye hataki nipeleke matumizi kwa mtoto ila in future yupo tayari kuishi na huyo mtoto bila kipingamizi chochote.
 
Kufa hufi ila cha moto utakiona, angalia moyo wako ndugu, huna haja ya kuoa sababu ya kumuonea mtu yeyote huruma, ila jiulize sana sana kama unampenda mpenzi wako wa sasa, huwezi jua nae labda ulimpenda kuwa nae baada ya huyo mwingine kuwa tu mjamzito.... uamuzi ni wako, fanya haraka kabla hujachelewa, mtoto unaweza mpa matunzo mazuri tu akiwa hata kwa mama yake
nashukuru Shantel,sasa kwenye nguvu za jadi ndio sijui itakuwaaje. Mimi siamini mambo hayo ila wao wanaamini na wanataka wadhuriane wao kwa wao,nimejaribu kuwasihi wasifanye hivyo ila kila mmoja anaapa kumwendea mwenzie kwa waganga kama nikionesha upendeleo kwa yoyote. Kati yetu watatu kila mtu anaishi kwake ila kila mmoja kati yao wawili kaweka wapambe wa kutoa taarifa kama nimekwenda nyumbani kwa mmojawapo na tifu linafumuka hapo.
 
umekoroga mwenyewe kunywa, kwanini lakini eti humpendi huyo uliyempa mimba na hapo nikisoma vizuri inaonyesha hao watu wote umekuwa na uhusiano noa within one year,just image ni maumivu ya kiasi gani umemsababishia huyo dada mjamzito na ni jinsi gani unavyo utesa moyo wa uliyemvisha pete?umefanya jambo lisilojema hata kidogo ,hakuna mwanamke anayependa kuzaa bila kuishi na family together(baba na mtotowe)Mie hata sikuonei huruma wacha wote wakunganganie ili wengine wajifunze matumizi ya kinga kama huna malengo ya kuzaa.
nimekuelewa ndugu yangu,mimi mwenyewe najuta ndio nikaona niombe ushauri kwenu ndugu zangu. Kuoa wote siwezi na kwa sasa nipo nao kwa kuwa sijapata suluhisho la kudumu,mawazo ya wadau nayoyapata nayachuja ili niyafanyie kazi.
 
Tupo pamoja ndugu zangu,mpaka sasa hakuna ninayeishi naye,kila mtu kwake,na wote wanataka ndoa na mimi niende kwao kujitambulisha rasmi. Kiukweli mawazo yananitesa mpaka naota ndoto mbaya,wazazi wangu hawanielewi kwasababu tangu mtoto nilikuwa mpole na mcha Mungu,wanajuta kwa mimi kusoma wanadhani uhuru uliopo vyuo vikuu ndio umebadili tabia yangu. Kweli najuta.
 
nimekuelewa ndugu yangu. Ila kuwa na wake wawili tena kisheria kiukweli siwezi,niliteleza tu ndugu yangu.

sasa ndugu unataka usaidiwaje,maana una option mbili ya kwanza kuoa wote wawili au kumchagua unaye mpenda.
Honestly ss wanawake nowdayz tumepoteza mwelekeo kisa kuolewa yani mwanaume anakuonesha mpo wengi wewe unang'ang'ania tu jamani mm nakwazika kweli.
 
Tupo pamoja ndugu zangu,mpaka sasa hakuna ninayeishi naye,kila mtu kwake,na wote wanataka ndoa na mimi niende kwao kujitambulisha rasmi. Kiukweli mawazo yananitesa mpaka naota ndoto mbaya,wazazi wangu hawanielewi kwasababu tangu mtoto nilikuwa mpole na mcha Mungu,wanajuta kwa mimi kusoma wanadhani uhuru uliopo vyuo vikuu ndio umebadili tabia yangu. Kweli najuta.

Fanya maamuzi najua kati ya hao kuna mmoja unampenda zaidi, na anafaa kuwa mke maana hiyo nayo ni factor angalia na vigezo vya mwanamke kuwa mke. Alafu mm najiuliza sana wacha Mungu wakigeuka upande wa pili wanakuwaga kama wamechanganyikiwa ndio maana wazazi wanawsws tele.
FANYA MAAMUZI SASA
 
mambo ya jadi tena? and u still wanna keep being involved? kweli ndo maana ww ni ww na mm ni mie!
hahahaha!!!!King'asti jana ulinicheka sana ukaniambia ni msiba wa kujitakia. ona sasa nduguyo ameanza zake...nakuambia huu ni mwanzo tu ngoma bado kuchezwa. hata THE BOSS najua analo ambalo amelificha. am fully prepared to console everyone of you'

Long'ututi, pole babaaa, usilazimishe mapenzi utayajutia baadae. subiri ajifungue umtunze mwanao akimaliza kunyonya mchukue akaishi na yule umpendae. isipokuwa kabla hujamchukua mtoto mfahamishe huyo mwingine kama yuko radhi kuishi na mtoto wa nje..akikataa mteme huyo hakupendi na umwendee mama mtoto. kuna msemo usemao ukipenda ngombe mpende pia na ndama wake.
 
Back
Top Bottom