Fanya mazoezi na kula vizuri
jiweke bize na kazi au hata vi shughuli vidogovidogo home, kama kupika, kufua, usafi wa nyumba au bustani.
Fanya vitu ambavyo vinakufurahisha, kama kuangalia movie, kusikiliza music, kucheza, kuchora, kuandika n.k.
Jitahidi kutoka out na marafiki ambao wana furaha na epuka kutoka out na marafiki ambao na wenyewe wana matatizo kama yako maana story zenu zitakuwa moja na mtaishia kuumizana tu.
Na kama wewe ni mpenz wa mitandao ya kijamii pia ni fulsa nzuri kuitumia kwa kujikita kushare ideas na marafiki ila epuka kutupia matatizo yako yanayokusibu maana kutakusababishia uwe nakumbukumbu ya kuumizwa
vaa vizuri, kuwa nadhifu muda wote na ujikubali kuwa mapenzi hayawezi kukunyima pumzi ya kuishi
kama upo karibu na familia yenu jitahidi uwe karibu na wadogo zako ili kushea furaha walizo nazo kwani huwa naamini watoto sikuzote huwa na furaha na hawana stress na kama unawadogo wanaosoma jitahidi kuwatembelea na kuwapa tuition hii husaidia sana kupunguza mawazo
uwapo peke yako jitahidi kujenga imagination ya vitu au mambo mazuri huku ukitabasamu.
Samehe na usijilaumu na kumlaumu anae kusababishia maumivui, ona kama upepo uvumao na ipo siku utatulia
epuka kulipiza kisasi kwa namna yoyote ile.
Pia kuhudhuria nyumba ya ibada nayenye husaidia na si tu kuudhuria siku ya Jumapili au Ijumaa tu... La hasha! Ninavyo amini kwa waislam na wa kristo kila siku ibada zipo asubuhi na jioni so kazi kwako kulia na Mungu wako hadi kieleweke
Epuka kuanzisha mahusiano mapya kwaajili ya kupata tulizo la moyo wako.
Furahia kuwa alone na ujifunze kutokupenda mwanamme kimapenzi na katu usimuamini mwanaume wa aina yoyote na usimchukie pia muone kama kiumbe cha kawaida...!
Mwisho.... JIPE MOYO,,,,,, usisubiri KUPEWA MOYO!!!!!!!!!!