Mapenzi yananitesa sababu ya huruma ya upendo: msaada

Mapenzi yananitesa sababu ya huruma ya upendo: msaada

Mimtamu

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2012
Posts
368
Reaction score
105
Hakika mapenzi hayana kanuni.

Kwa mwenye mapenzi ya kusoma thrd ndefu karibu..

Nina best yangu (Cecil) ambaye ninamkubali sana hasa katika umakini wa maisha yake but Hebu sikiliza kisa hiki cha jamaa yangu anaehitaji msaada.

Jamaa anaumri wa miaka ipatayo 30 hivi, hajaoa. Amesoma mpaka elimu ya juu but amejiendeleza sana katika ujasiliamali ambapo anamiliki kampuni yake binafsi. kiukweli jamaa ni mchapa kazi, mcheshi na mwenye kujali watu sana. Tatizo lake kubwa huyu kaka, hakuwahi kabisa kuhisi kupenda mtu kwa mapenzi, yaani kudate na mwanamke. hali hii ilimpelekea kukaa kwa muda wa miaka 3. bila kuwa na mahusiano (ilikuwa akipata matamanio mara mojamoja ana do na wapitaji tu).

Mnamo mwaka juzi mwishoni aliwaza sana juu ya hatma yake kwani hakuhisi kabs kumpenda mwanamke kimapenzi. Ila kuna binti (grace) mmoja ambaye alitokea kuwa nae karibu sana ikatokea huyo binti kumpenda kupita kiasi na alimjali na kumthamini sana jamaa. Kwa hali aliyonayo akaamua kujiweka kwa Grace. Jamaa kwakuwa ni mstaarabu sana akaamua kuliweka jambo peupe na hata kujulikana nyumbani kwa Grace. walishirikiana mambo mengi yaani kwa ufupi waliishi maisha ya uchumba. Jambo moja lililomtesa alijitahidi sana kumpenda lakini aliambulia patupu.

Jaka la moyo linaanzia hapa. Mwaka jana mwezi wa 7. alipata matatizo ya kuvamiwa na kujeruhiwa vibaya, kila mtu alisikitika sana pamoja na binti mmoja (magreth) ambaye ni mteja wake wa siku nyingi. Mage amekuwa akija dsm toka arusha kibiashara. kutokana na jambo hilo aliamua kuja dsm na kukaa kwa ndugu yake kwa muda wa mwezi mmoja huku akimhudumia rafiki yake wakati huo cecil alikuwa amelazwa hospitali ya tumaini. kitu cha ajabu kwa huyo binti anampenda sana wifi yake grace na amekuwa akichangia hela ya matibabu na kushirikiana na grace katika kumuuguza cecil mpaka alipopona.

Cecil alihisi moyo wake kufunguka na kuhisi upendo wenye nguvu juu ya mage ambapo ulimtesa sana. ilimchukua wakati mgumu kufikisha ujumbe kwa mlengwa.

Siku moja (wiki 3 zilizopita) wakiwa katika shughuli za hapa na pale mage akawa analalamika simu yake kusumbua ilikuwa ina tatizo la speaker, so alihitaji fundi mwaminifu. Cecil akamuomba amwachie aipeleke kwa fundi kisha jioni ampatie. Ilipofika jioni simu ipo tayari lakini mage hakutokea tena tena kwa siku mbili zaidi hali iliyompelekea apate hofu kidogo.

Katika kukagua simu akajikuta katumbukia katika uwanja wa sms, jambo lililomshangaza hakukuta ujumbe wowote wa kuashiria kama ana mahusiano ya kimapenzi. jambo hilo likampa mshawasha wa kutaka kumhoji, ndipo alipokutana nae na kumhoji mage akakiri kuwa ni kweli hayupo katika mahusiano, na cecil akaamua kuweka wazi hisia zake na alijihisi kutua mzigo mkubwa lakini jambo hilo lilipokelewa tofauti na mage kwani anajua cecil tayali ana grace.

Hitimisho,
Cecil anampenda sana Grace lakini si kimapenzi lakini pia ameishi nae katika maisha ya mapenzi kwa muda mrefu, pia Grace hana dosari yoyote ya kumfanya cecil. amchukie. Kwa upande mwengine Cecil kafa kaoza kwa Mage nae ni mwanamke mwenye vigezo vyote na ndiye anaeona kuwa faraja yake.

Sasa tunaomba tumshauri Cecil, anaogopa kumtema dada yetu wa awali kwani hataki kumuumiza kwani hajawahi kumtenda kwa lolote (hapati sababu stahiki za kumueleza kwanini amuache), wakati huohuo ataidhurumu sana nafsi yake kwa kumkosa huyu binti anayempenda kwa dhati Mage ambaye ana sifa zote za kuwa mke wa Cecil
 
Cijaielewa hii story yako kabisa ... naona kama kuna chembe chembe za ukameruni. Anyway ngoja waje wengine labda watakuelewa.
 
Cijaielewa hii story yako kabisa ... naona kama kuna chembe chembe za ukameruni. Anyway ngoja waje wengine labda watakuelewa.

Hahaha ukameruni tena? Jamaa yupo sawa. kifupi ni kwamba Bro yupo ktk mahusiano ya muda mrefu na binti ambaye hajawahi kufeel love kabisa yaani alijilazimisha tu ili aweke heshima kwa jamii but ametokea binti mwengine ambaye jamaa ametokea kumpenda sana yaani sana.

sasa jamaa anaogopa kumtema dada yetu wa awali kwani hataki kumuumiza kwani hajawahi kumtenda kwa lolote (hapati sababu stahiki za kumueleza kwanini amuache), wakati huohuo ataidhurumu sana nafsi yake kwa kumkosa huyu binti anayempenda kwa dhati..

nadhani utaelewa sasa
 
Cecil....Grace....Margreth.
Cecil yupo na Grace kimapenzi ila ame fall kwa Margreth, Mage nae anaogopa vile anajua Grace yupo na Cecil....

Hitimisho, Cecil ana hamu ya kumlala Margreth vile tunajua hana mapenzi ya kweli tangu mwanzo.
 
  • Thanks
Reactions: amu
Watanzania ni wavivu wa kusoma ukileta story ndefu hivi...tunapitisha macho tu
 
Cecil....Grace....Margreth.
Cecil yupo na Grace kimapenzi ila ame fall kwa Margreth, Mage nae anaogopa vile anajua Grace yupo na Cecil....

Hitimisho, Cecil ana hamu ya kumlala Margreth vile tunajua hana mapenzi ya kweli tangu mwanzo.

Hilo alilipinga kabisa.. alisema kwamba tatizo kwake sio hisia za kusex (matamanio).. ila jambo la kumpenda mwanamke tu ndio shida kwake sasa imetokea kapenda ambapo tangu azaliwe haijawahi kumtokea hiyo hali
 
Cecil....Grace....Margreth.
Cecil yupo na Grace kimapenzi ila ame fall kwa Margreth, Mage nae anaogopa vile anajua Grace yupo na Cecil....

Hitimisho, Cecil ana hamu ya kumlala Margreth vile tunajua hana mapenzi ya kweli tangu mwanzo.

Hahahahah nmekuelewa mkuu..kula LIKE
 
Duuuh.. Hii.story.nitakuwa.naijua.vyema kwani.huyo.mwenye.jina.la.cecil.namfahamu.kutokana.na.stori.hii.pamoja.na.grace.mtoto.wa.kipare. kwani.hapo.pa.kuvamiwa.na.kulazwa.tumaini.nimepata.kumfahamu

kama.ndiyo.hivyo.jamaa.kakamatika.maana.namjua.he.is.very.smart.
kwa.ushauri.tu.jamaa.afate.moyo.wake.kwani.kuna.hatihati.ya.kuja.kusaliti.ndoa.yake.tena.kwa.makusudi.na.kuridhika.ktk.moyo.wake.
pia.awe.makini.yawezekana.ugonjwa.wa.kupenda.ukapenda.wengi.maana.ndio.umemuanza.
pole.zake.cecil.aka.bosi.ulaya
 
Sasa nimekuelewa mkuu. Thanx

Hahaha ukameruni tena? Jamaa yupo sawa. kifupi ni kwamba Bro yupo ktk mahusiano ya muda mrefu na binti ambaye hajawahi kufeel love kabisa yaani alijilazimisha tu ili aweke heshima kwa jamii but ametokea binti mwengine ambaye jamaa ametokea kumpenda sana yaani sana.

sasa jamaa anaogopa kumtema dada yetu wa awali kwani hataki kumuumiza kwani hajawahi kumtenda kwa lolote (hapati sababu stahiki za kumueleza kwanini amuache), wakati huohuo ataidhurumu sana nafsi yake kwa kumkosa huyu binti anayempenda kwa dhati..

nadhani utaelewa sasa
 
Hii tunaita ni kuchezea maisha na kutojitambua..upo miaka 30 bado unachagua chagua..hivi sisi vijana tunafokiri unaweza kumpata mtu ambae amekamilika kila kitu au mtu unampenda na yy anakupenda hivyo hivyo..ni kujidanganya..
 
Mnadiskasheni nini? Naona harufu ya. Haki za makundi madogo.
 
Duuuh.. Hii.story.nitakuwa.naijua.vyema kwani.huyo.mwenye.jina.la.cecil.namfahamu.kutokana.na.stori.hii.pamoja.na.grace.mtoto.wa.kipare. kwani.hapo.pa.kuvamiwa.na.kulazwa.tumaini.nimepata.kumfahamu

kama.ndiyo.hivyo.jamaa.kakamatika.maana.namjua.he.is.very.smart.
kwa.ushauri.tu.jamaa.afate.moyo.wake.kwani.kuna.hatihati.ya.kuja.kusaliti.ndoa.yake.tena.kwa.makusudi.na.kuridhika.ktk.moyo.wake.
pia.awe.makini.yawezekana.ugonjwa.wa.kupenda.ukapenda.wengi.maana.ndio.umemuanza.
pole.zake.cecil.aka.bosi.ulaya

Una mwandiko mzuri.
 
daaah baada ya space ni mwendo wa nukta tu....kweli hii ni digitale
 
Aendelee na ampendaye . me sioni haja ya cecil kung'ang'ania sipopenda.
 
Back
Top Bottom