Mapenzi yananitesa, naombeni ushauri

Naomba nitoe ushauri kwa Miriam kama Babu DC!!

1. Kama unapenda mwenyewe kutoa mimba..basi katoe (at your own risk)! Ila kama hupendi basi usithubutu. Akizidi kukulazimisha chukua pesa uzitie ndani kwani hiyo itakuwa ndiyo pay yako ya mwisho toka kwake!!

Na kama umeamua kutokubaliana na matakwa yake ya kutoa mimba, basi kaa mbali naye...Wengine ni wataalamu sana. Anaweza kukodisha vijana wa kazi na ukija kuamka ukajikuta huna hiyo mimba tena...Tumeyaona na kuyashuhudia kwa macho yetu haya haya, ingawa sasa yanaona kwa kutumia msaada wa watu wa marekani!!

2. Futa maneno yako hayo eti bado unampenda....Naomba niishie hapo kwani inakaribia kunitia hasira.

Mtu keshakutumia kiasi cha kutosha na mwisho kakueleza kuwa wewe ulikuwa ni shea ya nyongeza...halafu unadai eti bado unampenda. Tena bila aibu unasema unampenda sana!! Duniani hakuna kupenda...kuna suala la kuangalia maslahi.. Sasa imeshakula kula kwako..Anza upya na Mungu akiwa upande wako basi utapata mtu mwingine muanze tena mchakato wa kudanganya!!

3. Jaribu kujiandaa kwa kadhia ya kuwa single parent...Sitaki kueleza mengi ila uwe tayari hata kutoolewa kwa sababu ya mtoto wako.

Pole sana na nakutakia kila la heri,

Babu DC
 
Huna haja ya kutoa hiyo mimba. Its your gift from God.

Tunza mimba zaa mtoto wako, wanaume ndivyo walivyo, ni sekunde tu wao kubadilika, na hawana huruma hawa. So usiumize kichwa sana.

Mushukuru Munu na endelea na maisha yako, na maandalizi ya ajae.

HE WAS NOT MAN ENOUGH FOR YOU
 
Laiti angekuwa anafikiria hivyo badala ya kuendelea kumlilia mtu ambaye keshatamka tena kinywani mwake kwamba hamtaki, hamuhitaji na hana shida ya kumbukumbu yake (hataki kuzaa naye)!!

Wakati mwingine mabinti mnaniudhi kwa kushindwa kutumia stadi za maisha tunazowafundisha kila siku kupembua kati ya mchele na chuya!!

Babu DC!!
 
Kwa uzoefu wangu finyu wa forums nimegundua wadada wanasema sana kuwa wanaume ni waongo. Pia tena kwa mda ule mfupi nliokaa vijiweni nikaambiwa sana kuwa wanawake ni waongo. Sasa nikaconclude both of them r liers! tusinyoosheane vidole coz najua dada yetu kadanganywa na hata akija m2 kanishikia panga hapa ntazidi kusisitiza kuwa na yeye alimdanganya jamaa pia kwenye mambo kadha wa kadha. Uctoe mimba(ni kuua kwa kukusudia kabisa-tena macho makavuuu! na huyo kiumbe unayemuua hana hata uwezo wa kupiga kelele kuomba msaada), lea mtoto. Its not over- na he who laughs last laughs the best! Yani huko baadae nna uhakika wewe ndo utacheka wa mwisho. Best of lucks!
nafikiri hujanielewa,niliyoyapigia mstari ni yale uliyoyosema,"wanaume wengi ukituondoa sisi wa jf ni waongo sana"jee una uhakika na hayo?mbona kuna watu humu walilalamika waliwahi kudanganywa na wanaume wa jf
 
MAPENZI YANANITESA NIPENI USHAURI

Nimefikiria kwa muda mrefu naona nazidi kupoteza muelekeo. Naombeni ushauri wenu wa mawazo naweza kufarijika kwani nipo njia panda. Ninampenzi ambaye kwa kiasi kikubwa ninampenda , mwanzao wa mapenzi yetu alinieleza kuwa anampenzi lakini hawawezi kuwa pamoja kwasababu ya imani ya dini zao hivyo uwezekano wakuishi pamoja hautaendelea kuwepo. Mimi nilikubali kwani nilikuwa tayari nimeshampenza sana.

Hivi sasa mimi nina mimba, na yeye ananiambia na yule aliyekuwa mpenzi wake pia ana mimba sikujali. Tatizo lilokuwepo kila siku ananilazimisha nikatoe mimba mimi nimemwambia sipo tayari kufanya hivyo kwani mimi nina kazi yangu nimemwambia sitamsumbua lakini haelewi anatafuta mpaka watu waje wanishauri nikatoe. Pia ananiambia hataweza kuwa na mm bora aendelee na mpenzi wake wa mwanzo. Naombeni ushauri nifanyaje kwani bado nampenda sana.
Mtengenezee LIMBWATAAAA!!!
 
And i dedicate this song to u Single boy/single girl by Ally Kiba feat Lady Jaydee!!!!
 
Laiti angekuwa anafikiria hivyo badala ya kuendelea kumlilia mtu ambaye keshatamka tena kinywani mwake kwamba hamtaki, hamuhitaji na hana shida ya kumbukumbu yake (hataki kuzaa naye)!!

Wakati mwingine mabinti mnaniudhi kwa kushindwa kutumia stadi za maisha tunazowafundisha kila siku kupembua kati ya mchele na chuya!!

Babu DC!!

Tatizo tukipenda tunapenda kweli, tunakuwa km wajinga.

Mimi siku hzi mwanaume haniumizi kichwa hata kidogo. Mwanaume wangu ni kazi yangu na maisha yangu FULL STOP.

Pole pole ataelewa tu kuwa he was not made for her, time will tell.

Agalia babu na huku kusije kukupandisha pressure.
 
Kitu chochote kikikutesa achana nacho so kama mapenzi yanakutesa achana nayo
 
Hayo ndo matatizo yakupenda mwanaume sio halali yako...Hivi angekuwa mme wako ungekuja uliza swali kama hili.
 
mapenzi yananitesa nipeni ushauri

nimefikiria kwa muda mrefu naona nazidi kupoteza muelekeo. Naombeni ushauri wenu wa mawazo naweza kufarijika kwani nipo njia panda. Ninampenzi ambaye kwa kiasi kikubwa ninampenda , mwanzao wa mapenzi yetu alinieleza kuwa anampenzi lakini hawawezi kuwa pamoja kwasababu ya imani ya dini zao hivyo uwezekano wakuishi pamoja hautaendelea kuwepo. Mimi nilikubali kwani nilikuwa tayari nimeshampenza sana.

Hivi sasa mimi nina mimba, na yeye ananiambia na yule aliyekuwa mpenzi wake pia ana mimba sikujali. Tatizo lilokuwepo kila siku ananilazimisha nikatoe mimba mimi nimemwambia sipo tayari kufanya hivyo kwani mimi nina kazi yangu nimemwambia sitamsumbua lakini haelewi anatafuta mpaka watu waje wanishauri nikatoe. Pia ananiambia hataweza kuwa na mm bora aendelee na mpenzi wake wa mwanzo. Naombeni ushauri nifanyaje kwani bado nampenda sana.

kabla hujashauriwa ni vizuri ulijue kosa lako. Kumpenda mtu asiyekupenda ni moja ya makosa makubwa katika ulimwengu wa mapenzi. Usilazimishe mapenzi ili mtu akupende ukiamini kuwa siku moja naye atakupenda. Ni dhahiri kabisa, huyu mwanamume hakukupenda toka mwanzo, ila wewe ulichukulia powa tu huku ukijua yupo ampendae tatizo ni dini. Nani kwakwambia dini inapingana na wapendanao kwa dhati?????? Dini inaweza kuonekana ni tatizo kwa muda tu, lakini kwa jinsi mapenzi ya dhati yalivyo na nguvu, mambo huenda yakapangika; maamuzi yakachukuliwa na penzi likaendelea.

Uliamua kupata mimba (maana hili ni uamuzi wako) eti kwa kuwa unampenda sana, rohoni mwako ukiamini ndio kigezo cha kumpata. Pole sana. Yeye hakukupenda ndio maana haoni uchungu kuua hata hicho kilichomo tumboni mwako! Na hataki kuwe na kumbukumbu kama alishakuwa na wewe!

Kubali kuvuna ulichopanda. Nakushauri usitoe mimba; na usiendelee kulazimisha kuwa naye; maana hakupendi. Wewe zaa, na kwa kuwa unauwezo wa kulea mimba na mtoto; endelea na mungu atakuwa na wewe. Kumbuka kudai matunzo na haki za mtoto.
 
Hana Mapenzi ya kweli na wewe
huyo Bwana
Jambo la msingi ni wewe Zaa Huyo Mwano na ujipange kumlea

Vumilia maumivu ya mapenzi yako kwake yataisha

Usijaribu kutoa hiyo mimba

Mrudie Muumba Wako , yeye ATAKUWEZESHA KTK YOTE
 
kwa ushauri kama aliotoa smile ni sahihi dada za mtoto wako na uachane nae hakupendi huyo anataka akutumie tu!
 
Hapa ndipo wanawake mnapo kosea kulazimisha upendo kwa mtu asiye kupenda
 
Huyo anaonekana hana mpango na wewe. Cha kufanya lea mimba yako tu. Kazi unayo utamudu kulea mtoto. Hizo ni changamoto za maisha hata kwetu wapo wa namna hiyo hata usiumize kichwa na kujipa presha yeye afurahie maisha wewe uteseke kwa lipi?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom