Mapenzi yananitesa, naombeni ushauri

Jan 2, 2012
43
6
MAPENZI YANANITESA NIPENI USHAURI

Nimefikiria kwa muda mrefu naona nazidi kupoteza muelekeo. Naombeni ushauri wenu wa mawazo naweza kufarijika kwani nipo njia panda. Ninampenzi ambaye kwa kiasi kikubwa ninampenda , mwanzao wa mapenzi yetu alinieleza kuwa anampenzi lakini hawawezi kuwa pamoja kwasababu ya imani ya dini zao hivyo uwezekano wakuishi pamoja hautaendelea kuwepo. Mimi nilikubali kwani nilikuwa tayari nimeshampenza sana.

Hivi sasa mimi nina mimba, na yeye ananiambia na yule aliyekuwa mpenzi wake pia ana mimba sikujali. Tatizo lilokuwepo kila siku ananilazimisha nikatoe mimba mimi nimemwambia sipo tayari kufanya hivyo kwani mimi nina kazi yangu nimemwambia sitamsumbua lakini haelewi anatafuta mpaka watu waje wanishauri nikatoe. Pia ananiambia hataweza kuwa na mm bora aendelee na mpenzi wake wa mwanzo. Naombeni ushauri nifanyaje kwani bado nampenda sana.
 
Hapo kwenye red, panaonyesha wazi kuwa huyo mpenzio hana mpango kabisa wa kuwa na wewe ingawa wewe unampenda. Inaoneka aliaanzisha mahusiano na wewe kwa faida zake mwenyewe na siyo ugomvi wa tofauti za kidini kama alivyokwambia.
Mimba yako anaona inaweza ikamsababishia yeye agombane na mpenziwe wa zamani hali ya kuwa hana mpango wa kumuacha (which is Logic-Si busara kumuacha mpenzi wa zamani bila sababu ya msingi,wakati tayari ameshampotezea muda)
Cha msingi nafikiria uanze mapema kujipanga kujihudumia mwenyewe na mtoto wako, suala la kutoa mimba ni hatari kwani unaweza kupoteza maisha, na pengine yumkini ulipangiwa kuwa na mototo mmoja ambaye ndiyo huyo unayemuua.
Tafakari.
 
zaa mtoto wako mwambie haya iyo mimba si yake.ili akuache kwa amani maana hakupendi hata kidogo
na kwanini umnganganie mtu jamani? wanaume waliisha au huuziki wewe?
mtu kakuambia hakutaki wewe unamganda kaa kupe,ona sasa.wanaume mbona wengi tu jamani? ushaniharibia siku wallah.ungekuwa karibu ningekuzaba kibao
 
Pole Kwa Yaliyokukuta Ingawa Haujabainisha Kama Huyo Mpenz Wako Mliish Naye Kama Mke Na Mume(kujulikana Kwa Wazaz Pande Zote)
Nakushaur Jaribu Kushirikisha Wazee Wake Au Wa2 Wake wa Karibu Il Kumweka Sawa.
kama Hatajirekebisha Kubal Kuwa Mbali Naye Ila c Kukubal Kutoa Mimba Ni Hatari Vilvle Ataendelea Kuku2mia Kwa Maslah Yake.
 
Huyu mpenzi wako hakupendi bali alikuwa anakutumia
Ila aniacha hoi ina maana hajali afya yake yaani anado na kila mmoja bila kutumia protection
kweli kuna watu wamejitoa fahamu hapa duniani
Cha msingi usitoe mimba zaa,na tunza mwanao ila huyo mpenzi wako hana mapenzi ya kweli kwako
Jipange upya Miriam
 
pole nilichotaka sema kaongea namba 2 na 3.
i hope utajikaza, ndio mapenzi usijali utapata mtu ukija mfikiria huyu utajicheka.
 
ya nini muendelee kubishana?

mimba si unayo wewe na wwa kuamua kutoa ni wewe sio yeye.
 
1. Dada zangu wengi hufanya makosa ya kiufundi wakidhani ukizaa na mtu ndio utakuwa nae daima.
2. Mtoto ni muhimu sana katika maisha,maadamu Mungu kakujalia,utunze mimba,mtoto ni asset yako ya baadae ila habari
ya maendeleo ya mimba na mtoto usiache kumjulisha baba yake hata kama ni jambazi wa roho changa(mimba)
3. Usitoe mimba...labda kama umechoka kula chips na mayai na unatamani KIFO.
4. Mwisho wanaume wengi ukituondoa sisi wa JF ni waongo sana. Hizo ni mbinu za uwindaji.....ALIKUDANGANYA. Lakini
hata wewe ulishawahi kudanganya......ndio hali ilivyo na maisha yanaendelea.
USITOE....USIGOMBANE NAE.
 
Why did u put his name in your heart?? Ddnt u knw that heart always breaks?? Just put his name in a ring and not in a heart coz ring always circulates!! May b its so easy to fall in love bt hardly enough to find sm1 who will catch you. By the way dont do abortion...sawa???

hapo kwenye red, panaonyesha wazi kuwa huyo mpenzio hana mpango kabisa wa kuwa na wewe ingawa wewe unampenda. Inaoneka aliaanzisha mahusiano na wewe kwa faida zake mwenyewe na siyo ugomvi wa tofauti za kidini kama alivyokwambia.
Mimba yako anaona inaweza ikamsababishia yeye agombane na mpenziwe wa zamani hali ya kuwa hana mpango wa kumuacha (which is logic-si busara kumuacha mpenzi wa zamani bila sababu ya msingi,wakati tayari ameshampotezea muda)
cha msingi nafikiria uanze mapema kujipanga kujihudumia mwenyewe na mtoto wako, suala la kutoa mimba ni hatari kwani unaweza kupoteza maisha, na pengine yumkini ulipangiwa kuwa na mototo mmoja ambaye ndiyo huyo unayemuua.
Tafakari.

na chukua hatua
 
pole sana dada,kwa kuwa una kazi yako,na una kazi yako ambayo itakusaidia kumlea mwanao,achana na huyo tapeli.inaonekana huyo jamaa alikuwa anakutamani tu.baada ya kumkubalia na kufaidi penzi lako sasa kaota mbawa.ditch him,endelea na mambo yako.
 
Pole ndio baadhi ya viumbe hivi vya kiume walivo,
Hata km unampenda kiasi ganindio keshakwambia hakupendi tena na hana mda na ww,
Chakufanya songa mbele na maisha yako na kujipanga namna ya kulea mwanao,
Ili kupunguza usumbufu mwambie mimba ushatoa na uachane naye,then lea mwanao na usiruhusu tena ajea akusumbue,
Najua utaumia but mshukuru mungu kwa yote na ipo siku atakupatia aliye wako!
 
inakuaje watu hamjali afya zenu jamani yani mtu kakuambia alikua na msichana na we ukakubali kudo nae
pekupeku huogopi wewe?aah hata nikikulaumu ndio yashatokea hata hivyo pole sana.kama una kazi yako
huna haja ya kumfatilia huyo mwanaume tunza mimba yako na jiwekee akiba ya kutosha ili ikusaidie wakati utakapojifungua
huna haja ya kumfatafata achana nae japo inauma.pole my dear lkn usitoe mimba.
 
Yaan dada angu imeniuma sana,kwann ameamua kukupotezea muda lakini daah anyway we mimba uctoe wala nn, cha muhimu jipange upya lea mimba yako na Allah atakutangulia, na hyo mwanaume mwnyzmungu atampa malipo yake inshaalla!h!
 
Asante sana nashukuru kwa kunipa moyo

Yaan dada angu imeniuma sana,kwann ameamua kukupotezea muda lakini daah anyway we mimba uctoe wala nn, cha muhimu jipange upya lea mimba yako na Allah atakutangulia, na hyo mwanaume mwnyzmungu atampa malipo yake inshaalla!h!
 
1. Dada zangu wengi hufanya makosa ya kiufundi wakidhani ukizaa na mtu ndio utakuwa nae daima.
2. Mtoto ni muhimu sana katika maisha,maadamu Mungu kakujalia,utunze mimba,mtoto ni asset yako ya baadae ila habari
ya maendeleo ya mimba na mtoto usiache kumjulisha baba yake hata kama ni jambazi wa roho changa(mimba)
3. Usitoe mimba...labda kama umechoka kula chips na mayai na unatamani KIFO.
4. Mwisho wanaume wengi ukituondoa sisi wa JF ni waongo sana. Hizo ni mbinu za uwindaji.....ALIKUDANGANYA. Lakini
hata wewe ulishawahi kudanganya......ndio hali ilivyo na maisha yanaendelea.
USITOE....USIGOMBANE NAE.
mmmh,jisemee nafsi yako tu.una uhakika gani kwa hayo niliyopigia mstari mwekundu?wanaume ni wanaume tu
 
mmmh,jisemee nafsi yako tu.una uhakika gani kwa hayo niliyopigia mstari mwekundu?wanaume ni wanaume tu
Kwa uzoefu wangu finyu wa forums nimegundua wadada wanasema sana kuwa wanaume ni waongo. Pia tena kwa mda ule mfupi nliokaa vijiweni nikaambiwa sana kuwa wanawake ni waongo. Sasa nikaconclude both of them r liers! tusinyoosheane vidole coz najua dada yetu kadanganywa na hata akija m2 kanishikia panga hapa ntazidi kusisitiza kuwa na yeye alimdanganya jamaa pia kwenye mambo kadha wa kadha. Uctoe mimba(ni kuua kwa kukusudia kabisa-tena macho makavuuu! na huyo kiumbe unayemuua hana hata uwezo wa kupiga kelele kuomba msaada), lea mtoto. Its not over- na he who laughs last laughs the best! Yani huko baadae nna uhakika wewe ndo utacheka wa mwisho. Best of lucks!
 
1. Dada zangu wengi hufanya makosa ya kiufundi wakidhani ukizaa na mtu ndio utakuwa nae daima.
2. Mtoto ni muhimu sana katika maisha,maadamu Mungu kakujalia,utunze mimba,mtoto ni asset yako ya baadae ila habari
ya maendeleo ya mimba na mtoto usiache kumjulisha baba yake hata kama ni jambazi wa roho changa(mimba)
3. Usitoe mimba...labda kama umechoka kula chips na mayai na unatamani KIFO.
4. Mwisho wanaume wengi ukituondoa sisi wa JF ni waongo sana. Hizo ni mbinu za uwindaji.....ALIKUDANGANYA. Lakini
hata wewe ulishawahi kudanganya......ndio hali ilivyo na maisha yanaendelea.
USITOE....USIGOMBANE NAE.

Hapo umenifanya nicheke sana.....Uko tayari kuitunza hiyo mimba??

Babu DC!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom