Mapenzi yana run dunia

pwilo

JF-Expert Member
May 27, 2015
10,076
12,389
Mery Christmas to everyone,

Mapenzi yana run dunia sio neno geni miongoni mwetu neno ambalo linatumika mara nyingi kuonyesha nguvu ya mapenzi katika maisha yetu ya kila siku.

Baada ya kusikiliza interview za watu watatu maarufu za hivi karibuni nimeamini mapenzi yana watesa watu wengi sana hata ambao hatuwadhanii kuwa kwenye hali hiyo kutokana na status zao kwenye jamii kama ifuatavyo;

MILLARD AYO: licha ya umaarufu na ukwasi alio nao lakini suala la mapenzi kwake ni changamoto, kama ambavyo alielezea kwenye moja ya interview zake alizo fanya kwamba alikuwa na mchumba wake anaishi mwanza na walikuwa wanakutana kila weekend. MILLARD ilikuwa anasafiri kumfuata mwanza ila alipotea hewani ikawa hapatikani na alipofuatilia watu wa karibu wakamwambia huyo binti ameshaolewa mda, MILLARD anasema ni moja kati ya vitu ambavyo vilimuumiza sana kichwa na alichukuwa mda kukaa sawa kutokana na tukio hilo.

Pia katika tukio jingine alishawahi kumfumania demu wake akiwa na jamaa mwingine live.

MWAKINYO: katika kipindi cha salama alichofanya na mwakinyo ameelezea kwamba kipindi hajawa maarufu alikuwa na mchumba wake,
ambae walipendana sana ila mwakinyo ilikuwa hajajipinga kimaisha demu akaolewa na wenye nazo hiyo hali ilimtesa sana na ndio moja ya vitu vilivyompa mzuka wa kupambana mpaka akatoboa.

ALI KAMWE : huyu ni mchambuzi wa soka katika kituo cha AZAM TV katika moja ya interview yake aliyofanya na shafii dauda hivi karibuni alithibitisha kwamba alishawahi kuachwa na demu na kuolewa na jamaa mwingine hicho kitu anadai hakijatoka kichwani kwake mpaka leo.

Mapenzi ni pesa ila mbona MILLARD ana kila kitu ila mpaka leo mapenzi yanamtesa kweli mapenzi yana run dunia.

N:B vitabu vinasema tuishi nao kwa akili.
 
"Women are incapable of loving men in a way that a man idealizes is possible, in a way he thinks she should be capable of." - Rational Male
 
A woman will love her man deeply & indefinitely just from the moment she realizes her '3 vital insecurities' are SERIOUSLY taken care of (considered), even if she clearly understands that somehow, sometimes, he may be incapable of solving them all.~ Aristotle
 
"Women are incapable of loving men in a way that a man idealizes is possible, in a way he thinks she should be capable of." - Rational Male
Love is a gift that is spontaneously & generously offered; she cannot give it because she doesn't have it. She cannot withhold it if she has it. She can have it if she seeks it.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom